Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na Wawakilishi wa Tume ya Kimataifa dhidi ya hukumu ya kifo Papa amekutana na Wawakilishi wa Tume ya Kimataifa dhidi ya hukumu ya kifo   (ANSA)

Papa:Hukumu ya kifo siyo ya kibinadamu na maisha ni matakatifu!

Tarehe 17 Desemba, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wawakilishi wa Tume ya Kimataifa dhidi ya hukumu ya kifo na amewashukuru wote kwa kazi wanayoifanya ili kuweza kuisitisha kabisa hukumu ya kikatili

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kila maisha ni matakatifu na hadhi ya binadamu. lazima ilindwa bila ubaguzi. Amesema hayo Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena alipowapokea wawakilishi ujumbe kutoka Tume ya Kimataifa dhidi ya adhabu ya kifo. Hotuba yake kwa lugha ya kispanyola amewakabidhi ambayo inasema kwamba: Katekisimu ya a Kanisa Katoliki inakataa adhabu ambayo hudhuru sana hadhi ya utu wa binadamu, adhabu ambayo ni kinyume na Injili yenyewe, kwa sababu inahusisha kukandamiza maisha ambayo ni daima ni matakatifu mbele ya Muumba na ambayo Mungu peke yake ndiye hakimu wa kweli na mdhamini wa maisha hayo.

Ni aina ya adhabu isiyo ya kawaida kwa binadamu

Katika karne zilizopita, kwa mujibu wa maandiko ya baba Mtakatifu, matumizi ya adhabu ya kifo  kwa mara nyingine yamewasilishwa kama matokeo ya mantiki na ya haki; hata katika utaratibu wa Serikali ya Kipapa zamani ilifanya mchakato wa aina hii ya adhabu isiyo ya kibinadamu kwa kupuuza uwazi wa huruma juu ya haki.

Hii ndiyo sababu ya uundaji mpya wa Katekisimu,Baba Mtakatifu Francisko anaandika,  pia ina maana hata ya  kuchukua uwajibikaji wetu kwa siku za nyuma na kutambua kwamba kukubalika kwa aina hii ya adhabu ilikuwa ni matokeo ya mawazo ya wakati ule kufuatila zaidi  sheria kuliko ukristo, ambapo ilikuwa inathamanisha sheria, lakini bila kuwa na ubinadamu na huruma.

Kuelekea kusitishwa duniani

Baba Mtakatifu Francisko anawatakia matashi mema ya kuwa nchi zote zinaweza kupitisha suala hili ili kufikia kukomesha aina hii ya adhabu ya ukatili, licha ya mchakato mgumu wa kisiasa. Wakati huo huo, anatoa wito kwa mara nyingine tena kuwa makini na tahadhari ya mahakimu katika  mchakato wa kuta uamuzi wa maangamizi, au wa kiholela, ambayo kwa bahati mbaya amethibitisha ni tukio la kisasa. Hata hivyo Baba Mtakatifu pia anaandika kuhusu nafasi katika suala la kudhaminiwa ambalo linafaa liwe sawa.

Haki sawa iwe kwa baba au mama

Katika hotuba aliyoikabidhi Baba Mtakatifu anatumaini, hatimaye kuwa na  haki ambayo, pamoja na kuwa baba, pia iwe kama mama. Ishara za utunzaji wa pamoja na  kwa dhati, ni mfano wa upendo ambao pia ni wa kiraia na wa kisiasa, unaoneshwa katika vitendo vyote vinavyotaka kujenga ulimwengu ulio bora zaidi.  Upendo kwa jamii na wajibu wa kujitolea kwa ajili ya wema wa wote, Baba Mtakatifu anaandika  ni aina bora za upendo, ambao hauhusishi mahusiano tu kati ya watu binafsi, bali ha mahusiano mazuri, kama mahusiano ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

17 December 2018, 16:18