Vatican News
Papa Francisko ametuma salam na matashi mema ya Noeli kwa Mwaka 2018 kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Italia Papa Francisko ametuma salam na matashi mema ya Noeli kwa Mwaka 2018 kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Italia  (AFP or licensors)

Papa Francisko atuma salam za Noeli kwa wanajeshi wa Italia!

Baba Mtakatifu anawataka wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama nchini Italia kuwa hodari na jasiri na kwamba, yuko karibu nao kwa njia ya sala na sadaka. Anawakumbuka na kuwaombea kwani hii ni sadaka ya maisha, lakini zaidi ni huduma ya upendo kwa nchi yao! Baba Mtakatifu anawataka wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama kukuza na kudumisha ari na moyo wa huduma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli anakumbusha kwamba, Mtoto Yesu ndiye kiini na kilele cha Sherehe za Noeli, asaidie kukuza na kudumisha: umoja, udugu, ushirikiano na mshikamano katika familia na jumuiya mbali mbali za waamini! Baba Mtakatifu amewatumia salam na matashi mema ya Noeli na Mwaka Mpya 2019 wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama vya Italia na kuvipongeza kwa kazi kubwa vinavyotekeleza katika ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Baba Mtakatifu anasema, si rahisi sana kusherehekea Noeli nje ya viunga na upendo wa kifamilia, lakini wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama, kutokana na dhamana na wajibu wao, mara nyingi wanajikuta wakisherehekea Noeli nje ya familia na hata wakati mwingine nje ya nchi yao. Baba Mtakatifu anawataka wanajeshi hawa kuwa hodari na jasiri na kwamba, yuko karibu nao kwa njia ya sala na sadaka yake. Anawakumbuka na kuwaombea kwani hii ni sadaka ya maisha, lakini zaidi ni huduma ya upendo kwa nchi yao! Baba Mtakatifu anawataka wanajeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama kukuza na kudumisha ari na moyo wa huduma.

Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha ujumbe wake wa Noeli kwa kuwatakia baraka tele, katika huduma ya ukarimu kwa ndugu zao. Anawakumbusha kwamba, hata wakiwa mbali na nyumba pamoja na familia zao, bado wanaweza kuthubutu kuwatakia wengine salam na matashi mema ya Noeli na Mwaka Mpya wa 2019.

Papa: Wanajeshi wa Italia
27 December 2018, 10:48