Tafuta

Vatican News
Papa Francisko: Mshikamano wa Kanisa na familia ya Mungu nchini Indonesia iliyoathirika kwa Tsunami, 2018 Papa Francisko: Mshikamano wa Kanisa na familia ya Mungu nchini Indonesia iliyoathirika kwa Tsunami, 2018  (AFP or licensors)

Mshikamano wa Papa Francisko kwa watu wa Indonesia!

Baraza la Kipapa la Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, linajiandaa kupeleka awamu ya kwanza ya msaada kwa ajili ya familia ya Mungu nchini Indonesia kama kielelezo cha mshikamano wa udugu hasa katika kipindi hiki kigumu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Tsunami iliyotokea hivi karibuni  huko nchini Indonesia imesababisha zaidi ya watu 430 kupoteza maisha, watu 1500 kupata majeraha makubwa na wengine 16,000 kulazimika kuyahama makazi yao,  kutokana na athari kubwa zilizojitokeza kadiri ya takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa. Sehemu zilizoathirika zaidi ni Jakarta na Kisiwa na Sumatra. Baraza la Kipapa la Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, linajiandaa kupeleka awamu ya kwanza ya msaada kwa ajili ya familia ya Mungu nchini Indonesia kama kielelezo cha mshikamano wa udugu hasa katika kipindi hiki kigumu!

Msaada huu unasindikizwa na sala ya Baba Mtakatifu kwa ajili ya waathirika, juhudi ambazo pia zinatekelezwa na Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Kiasi cha fedha kinachotarajiwa kutolewa, kitatangazwa hivi karibuni kama kielelezo cha mshikamano wa huduma ya upendo na uwepo wa Karibu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa familia ya Mungu nchini Indonesia.

Papa: Tsunami 2018
31 December 2018, 10:31