Cerca

Vatican News
Uzuri wa milele ndilo tumaini linalotuongoza kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko Uzuri wa milele ndilo tumaini linalotuongoza kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko  (Maurizio Grandi)

Papa:uzuri wa milele ndiyo tumaini linalotuongoza

Katika ujumbe ulio tumwa katika fursa ya Mkutano wa XXIII wa Baraza la Kipapa la Utamaduni, Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza kwamba mada ya milele ni mantiki ambayo imesahauliwa katika utafiti wa kitaalimungu katika kipindi cha miaka ya mwisho na kwenye mafunzo na katekesi kwa waamini

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkutano wa XXIII wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya utamaduni ambayo imeanza  kwa kuongoza na madaya ya “umilele ni sura nyingine ya maisha” ni chachu ya kutafakari kwa mara nyingine  tena ukuu na  juu ya maisha ya milele, kiungo msingi cha imani ya kikristo. Ndivyo ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko unavyoanza aliomtumia Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni wakati wa kufungu mkutano wao tarehe 4 Desmba 2018.

Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba mada ya umilele ni mantiki ambayo imesahauliwa katika utafiti wa kitaalimungu katika kipindi cha miaka ya mwisho na kwenye mafunzo ya waamini kwani “Tafakari hiyo katika nyakati za mwisho maono yake hayapati nafasi na umakini unaostahili katika Katekesi na maadhimisho kwa waamini. Baba Mtakatifu anahisi kuwa mada juu ya maisha ya milele kwa kupenda imesahuliwa na kuachiliwa mbali au kutojali katika maisha ya kila siku na uelewa wa sasa.

Wakati ujao zaidi ya kifo unaonesha kutoshikika

Ukosefu wa umakini katika mada ya umilele inaweza kutokana na mantiki nyingi. Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, moja ya matokeo ambayo yanaonesha katika utamaduni wa sasa ni hasa kufunga upeo wa yule aliye juu, kujijifungia binafsi, kwa kushikilia tu wakati uliopona kusahamu au kuondoa ukuu wa wakati uliopita  na zaidi wakati endelevu, ambapo kwa namna ya pekee, vijana wanautambua kama giza na mzigo usio kuwa na uhakika. Wakati endelevu zaidi ya mauti unaonekana katika mantiki hiyo ambayo siyo rahisi kuzuia kwa jinisi ilivyo mbali na haiwezi kuishikilia au kutokuwapo kabisa.

Lugha lazima iwe na upyaisho

Mantiki nyingine ambayo ni kizingiti cha umakini juu ya maisha ya milele inajikita juu ya lugha ya utamaduni, ambayo unatumika katika mahubiri au katika katekesi ya kutangaza ukweli huo wa imani. Baba Mtakatifua anasisitiza kuwa lugha kama hiyo karibia inaweza kutoeleweka na kuonesha wakati mwingine, uchanya kidogo wa sura na kuvutia Maisha ya Milele.

Uzuri wa umilele

Ushauri wa Baba Mtakatifu ni kwamba: Tafakari ya Mababa wa Kanisa na wataalimungu, wanapaswa watusaidie na kukututia moyo ili kupendekeza kwa dhati shauku iwe ya lugha inayostahili katika maisha yetu ya kiila siku na iwe na fursa ya kina katika moyo wa imani, matumaini ambayo yanaongeza roho na kutupatia nguvu za kushuhudia ukristo duniani ule uzuri wa umilele.

05 December 2018, 16:01