Tafuta

Bikira Maria na Yosefu mchumba wake walifanya  uzoefu wa huzuni na mshangao katika Familia Takatifu ya Nazareth Bikira Maria na Yosefu mchumba wake walifanya uzoefu wa huzuni na mshangao katika Familia Takatifu ya Nazareth 

Papa:Familia ni tunu lazima kuitunza na kuilinda!

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 30 Desemba 2018 Baba Mtakatifu Francisko ametafakari Sikukuu ya Familia Takatifu ya Nazareth kuhusu uzoefu wa Yesu Maria na Yosefu walivyokuwa wameungana kwa upendo wa kina na kuongozwa na imani kubwa kwa Mungu na mwisho amesema familia ni tunu na hivyo lazima kuitunza na kuilinda

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mshangao na huzuni ndiyo maneno mawili yamejikita katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko na kuweka umakini  waamini waliokuwa wamekusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 30 Desemba 2018, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu. Baba Mtatifu akiongozwa na Injili ya siku kutoka ( Lk 2,41-52) inayosimulia safari ya familia ya Nazareth kueleka Yesrusalemu kwenye sikukuu ya Pasaka na kutafutwa kwa Yesu wakati wa kurudi nyumbani, anaweka bayana juu ya kiini cha Mwana wa Mungu katika Familia Takatifu, mahali ambamo leo hii Kanisa linaadhimisha sikukuu hiyo.

Maisha bila Yesu

Wakati wa safari ya kurudi toka Yerusalem, Maria na Yosefu wanajikuta katika msafara hawana mtoto wao wa miaka 12; na baada ya siku tatu wanamtafuta kwa hofu, wanamkuta katika hekalu amekaa katikati ya walimu na waandishi, akiwa makini anawasikiliza na kuwauliza maswali. Akitafakari suala hili Baba Mtakatifu ameonesha neno la huzuni ambao Bikira Maria alifanya uzoefu na mchumba wake, kwa manaa wao wwalikuwa wamempokea Mtoto,walikuwa wanamtunza na walikuwa wanamuona anakua kwa hekima na neema katikati yao, uwepo ambao ulikuwa unakua hata ndani ya mioyo yao. Huzuni walio kuwa nao kwa siku tatu kutokana na  kupotea kwa Yesu, unapaswa uwe huzuni wetu, hasa tunapokuwa mbali na Yesu. Tunapaswa kuhisi huzuni iwapo kwa siku tatu tunamsahau Yesu, bila kusali, bila kusoma Injili, bila kuhisi mahitaji ya uwepo wake na faraja ya urafiki wake. Na mara nyingi zinapita siku kadhaa bila kumkumbuka Yesu, lakini hiyo ni mbaya na mbaya sana amesisitiza Baba Mtakatifu!

Tuhisi huzuni ndani ya maisha yetu tunapomsahau Yesu

Tunapaswa kuhisi huzuni iwapo mambo hayo yanatokea, Baba Mtakatifu amesisitiza kwa mara nyingine tena. Maria na Yosefu walimtafuta Yesu na wakamkuta katika hekalu akiwa anafundisha, na kwa maana hiyo hata  kila mwaamini anaweza kukutana na Mungu Mwalimu katika nyumba ya Mungu na kupokea ujumbe wa wokovu. Katika maadhimisho ya Ekaristi, Baba Mtakatifu anabainisha, tunafanya uzoefu hai wa Kristo; Yeye anazungumza nasi, anatoa Neno lake kwetu sisi na linatuangazia safari yetu, anatupatia Mwili wake katika Ekaristi Takatifu na ambayo tunachota ile nguvu hai ya kukabiliana na matatizo ya kila siku.

Mshangao unatufungulia dunia

Kwa familia zote ambazo kwa sababu mbalimbali, wanakosa amani na umoja, Baba Mtakatifu anaelekeza mfano na ulinzi wa Familia Takatifu ya Nazareth mahali ambamo, hapakukosekana kamwe mshangao na hata wakati wa hali ngumu kama ile ya kupotea kwa Yesu. Kustaajabu na kushangaa, ni mambo yanayozuia kutafsiri hali halisi na matukio ya historia kwa urahisi tu katika misingi ya matakwa na mantiki binafsi. Kustaajabu ni kujifungulia wengine, kuwa na uwelewa wa sababu za wengine. Tabia hii ni muhimu kwa ajili ya kuponya mahusiano yasiyo mazuri kati ya watu na inahitajika hata kwa ajili ya kuponya majeraha yaliyo funguka kwa mantiki ya kifamilia. Iwapo hatujali na kuona kuwa tunayo sababu, Baba Mtakatifu anasisitiza, ni kuwafungia mlango wengine, kinyume chake ni msingi wa kustaajabu na kukushanga kwa kile kilicho chema na ambacho kimo ndani ya mtu hasa hasa kulinda umoja wa familia.

31 December 2018, 09:05