Tafuta

Vatican News
Wawakilishi wa chama cha vijana Katoliki Italia wamekutana na Baba ;takatifu Francisko Wawakilishi wa chama cha vijana Katoliki Italia wamekutana na Baba ;takatifu Francisko   (Vatican Media)

Papa:Chama cha vijana katoliki nchini Italia, kuweni mfereji!

Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 20 Desemba 2018, amekutana na wawakilishi wa Chama cha vijana Katoliki nchini Italia. Katika hotuba yake anawahimiza wawe wakarimu, wawe mfereji wa wema na mapokezi ili kuweza kujenga dunia ya kidugu, yenye mshikamano zaidi na kuwa wakristo zaidi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Daima ni vizuri kukutana nanyi wakati inakaribia Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Ninawasalimia kwa upendo. Salam pia kwa wote wanaowasindikiza; Rais wa Kitaifa wa Chama Cha vijana Katoliki, Italia, Dk Matteo Trufelli, Msiamamizi Mkuu, Askofu Gualtiero Sigismond, na viongozi wenu na wwote wanaoshirikishana nanyi kwa ngazi ya kitaifa. Ni zawadi ya Mungu ambaye ni wa kumshukuru daima kwa ajili ya kuwa na watu wazima, mapadre na walei ambao wanajali kwa upendo mkuu kuhusu mafunzo yenu ya kibinadamu na kikristo; na kwa maana hiyo mnapaswa kusali kwa ajili yao, ili wawe na hekima ya katenda vema huduma hiyo!

Kukutana na Yesu kila siku katika sala ili kuweze kuwa kweli wamisionari wake

Huo ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 20 Desemba 2018, alipokutana na wawakilishi wa chama cha vijana Katoliki nchini Italia. Katika hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amewaeleza vijana jinsi gani anatambua juu ya safari yao ya mafunzo ambayo kwa mwaka huu inaongozwa na mada ya makutano ya Yesu na dada ndugu wawili, Marta na Maria huko Betania kwa mujibu wa Injili ya Mtakatifu Luka. Na kwa maana hiyo anasema katika tukio hilo kama vijana wa majimbo yote ya Italia wanajikita kugundua wito wa kuwa marafiki wa Yesu na kuzidi kumtambua vema, wakati wanakutana naye kila siku katika sala ili waweze kuwa kweli wamisionari wake.

Baba Mtakatifu anasema: Hiyo ni hali ya kutangaza habari njema, Ujumbe wa wokovu kwa vijana wenzao, hata kwa watu wazima. Je ni ishara ipi hiyo, Baba Mtakatifu amewauliza. Ishara ni kwamba wote tunapendwa na Bwana na ndiyo habari njema kubwa ya Mungu aliyotoa katika dunia kwa njia ya ujio wa Mwanae Yesu Kristo kati yetu. Sisi sote tumependwa na Bwana, kila mmoja, Baba Mtakatifu anasisitiza na kusema ni kitu kizuri sana!

Wanapeleka daima mbele ishara ya kuanzishwa kwa upendo

Aidha ameelezea ameonesha furaha yake, kusikia kwamba, kuunganika huko katika hija ya mafunzo yao, wao wanapeleka daima mbele ishara ya kuanzishwa kwa upendo. Mwaka huu wanasaidia haki ya chakula na hadhi ya wale wanaofanya kazi ardhini yaani wakulima, hivyo amewapongeza kwa kufanya uchaguzi huo na kwa ujasiri. Anawashukuru kwa zawadi waliyoitoa na ambayo itakwenda katika Mfuko wa Kitume kwa ajili ya wahitaji. Baba ;takatifu anaongeza: Ni jambo muhimu sana, kwa maana ya vifaa muhimu ambayo vinahitaji kwa watu wengi maskini. “Asanteni sana kwa ajili ya kufikiria hivyo”.

Vijana wawe wakarimu, wawe mfereji wa wema na mapokezi ili kuweza kujenga dunia ya kidugu

Wapendwa vijana, Baba Mtakatifu ansema: Kuzaliwa kwa Bwana kwa mara nyingine, Yesu anataka kuzaliwa ndani mwenu, katika mioyo yenu na ili kuwajaza furaha ya kweli ambapo hakuna yoyote anaweza kuwajalia. Na ninyi pia toeni furaha hiyo kwa vijana wengine wanaoishi katika hali ya mateso na labda wanapata suluba. Baba Mtakatifu anawaomba watoto hao wawe wakarimu, wawe mfereji wa wema na mapokezi ili kuweza kujenga dunia ya kidugu, yenye mshikamano zaidi na kuwa wakristo zaidi. Hatimaye amewatakia Sikukuu njema, kwa ajili ya familia yao na Chama cha Kitume Katoliki. Bwana amewabariki na kuwaombea wasali kwa ajili yake.

 

20 December 2018, 15:01