Baba Mtakatifu atasali katika sanamu ya Bikira  Maria mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania tarehe 8 Desemba 2018 Baba Mtakatifu atasali katika sanamu ya Bikira Maria mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania tarehe 8 Desemba 2018 

Papa Francisko: Awakumbuka Wenyeheri wapya 19 kutoka Algeria

Mara baada ya tafakari ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kutangazwa Wenyeheri wapya 19 nchini Algeria.Kadhalika amkumbusha juu ya ajali huko Ancona;upyaisho wa wanachama wa Chama cha Vijana Wakatoliki Italia na mwisho, juu ya safari katika uwanja wa Hispania kutoa heshima katika picha ya Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo katika Madhabahu ya Mama yetu wa Mtakatifu Cruz huko Oran, nchini Algeria, wametangazwa Wenyeheri wapya Askofu Pietro Claverie na wenzake kumi na nane, watawa wa kike na kiume, waliouwawa kwa ajili ya kutetea imani yao. Mashihidi 19. Mashahidi wa nyakati zetu, wamekuwa waaminifu wa kutangaza Injili, wanyenyekevu wa amani na mashujaa wa ushuhuda wa upendo kikristo. Ni Askofu, mapadre, watawa kike na kume na walei… Ujasiri wao wa kushuhudia ni kisima cha matumaini kwa ajili ya jumuiya ya wakatoliki wa Algeria na mbegu ya mazungumzo kwa ajili ya jamii nzima. Kutangazwa kwa wenye heri hawa, iwe kwa wote chachu ya kujenga pamoja dunia ya kidigu na mshikamano. Tuwashangilie Wenyeheri wapya!

Papa anawakumbuka waathirika wa ajali huko Ancona, Italia

Ninawakikishia kumbukumbu ya sala kwa vijana na mama amba oleo hii usiku wameaga dunia wakiwa katika muziji huko Corinaldo, karibu na Ancona, kama vile idadi kubwa ya majeruhi. Kwa wote ninawaoma kwa Mama Maria. Ndiyo mwanzo wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 8 Desemba 2018, mara baada ya tafakari ya neno la Mungu katika Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Sikukuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili ambapo amewambia waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican. 

Miaka 150 ya Chama cha matendo katoliki nchini Italia

Akiendelea na salama zake, amezielekeza kwa wanahujaji wote kutoka nchini Italia na nchi mbali mbali, kwa namna ya pekee wanafamilia, makundi ya maporokia na vyama vingine. Katika Sikukuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili, katika maporokia ya Italia, Chama cha matendo katoliki, wanajipyaishwa hasa katika chama hiki ambacho kwa miaka 150 ni zawadi na rasilimali kwa ajili ya safari ya Kanisa la Italia. Baba Mtakatifu anawatakia moyo makundi yote ya majimbo na maparokia ili wajikite kwa dhati katika mazungumzo ya walei wenye uwezo wa kushuhudia Injili na kuwa chachu katika jamii ya haki na mshikamano.

Baraka kwa waamini wa Rocca di Papa

Anawabariki kwa moyo wote, waamini wa Rocca di Papa nchini Italia na ambao watawasha nyota kubwa juu ya ngome yao nzuri, kwa ajili ya kutoa heshima ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili.

Sala kwa Mama Maria katika Kanisa kuu la Mtakatifu Maria na uwanja wa Hispania

Kadhalika Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini juu ya safari yake kwenda katika kwanza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kusali kwa Mama Maria na baadaye atakwenda katika uwanja wa Hispania, ili kupyaisha kwa mara nyingine, utamaduni wa kutoa heshima na sala  chini ya miguu ya kumbusho la Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili, aliwaomba waungane pamoja kiroho katika ishara hiyo ya kuonesha ibada kuu ya kuwa wana wa Mama yetu wa Mbinguni. Kwa wote aliwtakiwa sikukuu njema na safari ya Majilio, kwa maongozi ya Bikira Maria.

08 December 2018, 13:01