Cerca

Vatican News
Sala ya Baba Mtakatifu kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili Sala ya Baba Mtakatifu kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili 

Papa anaomba Mama Maria akae karibu na familia zenye matatizo!

Kabla ya kutimiza tendo la kiutamaduni wa ibada ya bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania, Baba Mtakatifu Francisko ametoa heshima kwa Mama Maria Afya wa watu wa Roma, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu. Na katika sala ya Baba Mtakatifu anombea mji wa Roma ili kila mmoja aweze kujikita katika ustawi wa pamoja na mji uweze kuwa mzuri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili iliyowekwa na Papa Pio IX kunako tarehe 8 Desemba 1854, hata mwaka huu Baba Mtakatifu Francisko amekwenda kutoa heshima  kwa Bikira katika moyo wa Roma, kwa kupeleka maisha na matatizo ya wakazi wa mji . Tendo la kutoa heshima kwa Mama Maria kwa Mapapa katika historia limekuwa likifanya hivyo kila mwaka. Kabla ya kutimiza tendo la kiutamaduni la ibada ya bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania mjini Roma, Baba Mtakatifu Francisko ametoa heshima kwanza  kwa Mama Maria, Afya ya watu wa Roma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu. Alipofika katika uwanja wa Hispania, Baba Mtakatifu Francisko amepokelewa na Kardinali Angelo De Donatis Makamu wake na viongozi wa raia. Chini ya Mnara mkuu wa sanamu ya Bikira Maria kulikuwa na shada la maua ambalo  kama utamaduni, upandishwa juu na kikundi maalum cha wazima moto.

Kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku kwa uvumilivu

Umati mkubwa umempokea Baba Mtakatifu Francisko, akiwa anatemeba kwa ukimya. Na wakati wa kuanza sala yake, mawazo ya kwanza yamewaendea wagonjwa wote na wale wenye shida ya kwenda mbele katika maisha yao;  wale ambao kwa neema ya kawaida Bikira Maria anawatendea watu  wanaoishi Roma. Wale wote ambao wanakabiliana na  matatizo kila siku kwa uvumilivu, kwa wote hao, Baba Mtakatifu anasema: "nikuomba nguvu ili wasikate tamaa, kinyume chake kila mmoja katika nafasi yake aweze kuboresha mambo, kwa sababu kila mmoja anaweza kutunza na kulinda mji wa Roma ili uweze kuwa nzuri na wa kuishi watu wote.

Kusali kwa ajili ya wenye nafasi ya uwajibikaji

Baba Mtakatifu akifikiria ustawi wa wote katika mji, ameongeza kusema: " tusali kwa ajili ya wale wenye nafasi kuu ya uwajibikiaji, ili wawe na hekima ya kudumu na roho ya huduma na kushirikiana. Kwa ajili ya mapadre wote wa Jimbo anaombea  kwa Bikira wawe na utamu wa furaha; na kwa ajili ya watawa wa kike na wale wa kisekulari, ambapo amekumbusha kuwa, "kwa neema ya Mungu mjini Roma ni wengi sana zaidi ya miji mingine duniani".  Na kwa pamoja hao wanaunda jambo  zuri linalopendaza, la kimataifa na utamaduni. Kwa ajili yao, anawaombea furaha ili waweze kutoa matunda katika sala, upendo wa dhati na huruma.

Kulinda haki za familia wanaoishi katika hali ya sintofahamu

Baba Mtakatifu akitazama tukio la Bikira Maria na Yosefu ambao walikwenda kujiandikisha na waliacha Nazareth kwenda Betlehemu, amekumbuka katika sala zake familia zote na kusali: “Wewe unajua nini maana ya kubeba maisha katika umbu na kuhisi utofauti au sintofahamu, kukataliwa na wakati mwingine kudharauliwa. Kwa njia hiyo ninakuomba ukae karibu na familia ambazo leo hii mjini  Roma, Italia na katika dunia nzima wanaishi katika hali sawa na hiyo, ili wasiachwe peke yao,bali walindwe haki zao na  haki za kibinadamu ziweze kupewa kipaumbele licha ya dharura za kesheria.

Urithi wa Yesu pendaneni ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi

Akihitimisha Baba Mtakatifu Francisko, anamwomba Bikira Maria alinde mji kama vile asimamie nyumba, mashule, maofisi, maduka, viwanda, mahospitali na magereza. Pasiwepo ukosefu wa tunu msingi kama zilizopo Roma mahali  popote na kuhifadhi katika  dunia nzima ule urithi wa Yesu ambao aliutoa na kusema: “pendaneni nyinyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda”. Na baada ya sala hiyo, Baba Mtakatifu Francisko wakati akirudi Vatican, amesimama kidogo katika makao ya Gazetti la kila siku  “Messagero”, yaliyopo  mtaa wa Tritone, ili kusalimia viongozi wakuu na wahudumu wake.

08 December 2018, 17:21