Baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 30 Desemba 2018, Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya uchaguzi wa Congo DRC Baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 30 Desemba 2018, Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya uchaguzi wa Congo DRC 

Papa amesali kwa ajili ya uchaguzi Mkuu nchini Congo DRC

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 30 Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisiko ameomba kusali kwa pamoja kwa ajili ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao wanateseka kwa sababu ya vurugu na mlipuko wa Ebola

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 30 Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisiko ameomba kusali kwa pamoja kwa ajili ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao wanateseka kwa sababu ya vurugu na mlipuko wa Ebola. Maombi yake ni kwamba wote wajibidishe na kuweza kutunza hali ya amani katika kurudia hali ya  ukawaida na amani katika mchakato wa uchaguzi. Kutokana na hiyo amesali sala ya salam Maria…

Salam kwa mahujaji wote

Na baada ya kusali salam Maria, Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia waamini na mahujaji wote toka pande zote za dunia ikiwemo ni watu wa Roma, mahujaji makundi ya kiparokia, vyama na vijana, kwa namna ya pekee familia waliokuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Ameomba kuwapigia makofu familia zote, hata wale wanaotazama kwa njia ya luninga na kusikiliza kwa njia ya radio.  Baba Mtakatifu amesema Familia ni tunu, lazima kuitunza na kuilinda daima. Familia Takatifu ya Nazareth iwalinde na kuwaangazia daima katika safari yao. Na hatimaye kwa mahujaji wote amewatakia Dominika njema na utulivu wakati wa kumaliza mwisho wa mwaka. Anawahimia wamalize mwaka kwa utulivu. Kadhalika amewashukuru kwa mara nyingine tena kwa matashi mema waliyomtakia na sala zao na kuwaomba wandelee kumwombea!

31 December 2018, 09:15