Katekesi ya Papa Francisko tarehe 5 Desemba 2018 Katekesi ya Papa Francisko tarehe 5 Desemba 2018 

Papa ameanza mzunguko mpya wa katekesi kuhusu Baba Yetu

Wote tunaweza kusali zaidi na vema; lakini lazima kuomba Bwana. Bwana nifundishe kusali. Tufanye hivyo, katika kipindi cha Majilio na kwa hakika Yeye hatatuacha tuangukie katika utupu wa sala zetu. Ndiyo ushauri wa mwisho wa Baba Mtakatifu wakati wa katekesi yake kuhusu mzunguko mpya wa sala ya Baba Yetu, tarehe 5 Desemba 2018 katika ukumbi wa Paulo VI

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu kaka na dada habari za asubuhi. Leo hii katika mzungumo wa Katekesi tunaanza “Baba Yetu”. Injili zimetuonesha picha hai ya Yesu kama mtu wa sala: Yesu alikuwa anasali. Licha ya dharura ya utume wake na msongamano wa watu wengi ambao walikuwa wanamtafuta, Yesu alihisi mahitaji ya kwenda faragha, katika upweke na kusali. Injili ya Marko inasimulia jambo hili tangu sura ya kwanza ya huduma ya Yesu kwa watu (Mk 1,35). Ni mwanzo wa tafakari ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 5 Desemba 2018, kwa waamini na mahijaji wote katika ukumbi wa Paulo VI. Baba Mtakatifu ameanza tafakari mpya mara baada ya kumaliza mzunguko wa tafakari ya Amri za Mungu.

Na kwa maana hiyo katika kuelezea mzunguko mpya juu ya Sala ya, “Baba Yetu” anasema: Siku ya kwanza ya Yesu huko Kafaranaum ilikuwa imemalizika kwa njia ya ushindi. Jua lilipo zama, watu wengi wagonjwa, walifika katika mlango aliokuwa anaishi Yesu: Masiha, alikuwa anahubiri na kuponya. Ilitimia maneno ya kinabii yaliyosema zamani na matarajio mengi ya watu waliokuwa wanateseka. Yesu ni Mungu wa karibu, ni Mungu anayetoa uhuru. Lakini watu wengi walikuwa ni wachache ukilinganisha na wingi wa watu ambao wangemzuka masiha wa Nazareth; wakati mwingine ulikuwa ni mkutano kandoni mwa bahari na Yesu akiwa katikati ya yote, anayetarajiwa na watu na sababu ya matumaini ya Waisraeli.

Hatari ya viongozi kushikilia watu au maeneo

Baba Mtakatifu anasema kuwa licha ya hayo Yeye hakuweza kuweka vizingiti; japokuwa hakubali kuwekwa mateka na wengine, waliokuwa na matarajio ya muda mrefu kumchagua awe kiongozi. Hiyo ni hatari kwa viongozi kushikilia sana watu, bila kuwa na umbali nao. Yesu alitambua wanavyotaka na baadaye aweze kuishia mateka ya watu. Tangu mwanzo wa usiku wa Kafaranaum, anaonesha kuwa ni Masiha halisi. Sehemu ya mwisho wa usiku ambayo ilikuwa karibia alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Lakini wafuasi wake wanamtafuta tena na kwa maana  hawajuhi mahali halipo. Je yuko wapi? Hatimaye Petro alipomwona akiwa peke yake anasali akamwambia, “Watu wote wanakutafuta” (Mk 1,37).

“Sauti ya namna hiyo imewekwa makusudi ili kuonesha ushindi wa jaribio la kufanikiwa katika utume. Baba Mtakatifu amethibitisha. Lakini Yesu akawaambia, “Twendeni mahali pengine”. Na hiyo ina maana kwamba, siyo watu wanaomtafuta Yeye, bali hawali ya yote ni Yeye anatafuta wengine. Hiyo ina maana asisimike mizizi yake, bali abaki daima kama mhujaji katika njia ya kwenda Galilaya (Mk 1,38-39) pia hata ni mhujaji kuelekea kwa Baba,yaani kwa kusali. Katika safari ya sala, Yesu anasali. Na yote yalitukia wakati wa usiku.

Yote yalitukia wakati wa usiku

Katika sura nyingini za Maandiko Matakatifu, Baba Mtakatifu anabainisha kwamaba: “utafikiri sala ya Yesu awali ya yote ni katika kukaa kiundani na Baba, na undani huo unao tawala yote. Hiyo itajionesha kwa mfano katika usiku wa mateso kwenye bustani ya Getsemani. Hatua za mwisho wa Safari ya Yesu Baba Mtakatifu anasisitiza  ni ngumu kabisa zaidi ya zile zote alizowahi kufanya. Ni kama kupata maana yake ya kuendelea kusikiliza kwamba, Yesu anamshukuru Baba yke. Sala ambayo kwa hakika siyo rahisi na zaidi ni ukweli na binafsi wa machungu kwa maana, kama vile ya mazoezi ya wanariadha au sala yenye uwezo wa kusaidia katika njia ya msalaba.

Hatua msingi ni kwamba Yesu alikuwa anasali

Akiendelea na ufafanuzi zaidi wa hatua nyingine Baba Mtakatifu anathibitisha: Tazama hatua msingi ni ile ambayo Yesu  alikuwa anasali. Alikuwa anasali kwa kina wakati akiwa na watu na kushirikishana liturujia kwa watu wake, lakini pia alikuwa anatafuta sehemu za faragha, zilizotengena na dunia, mahali ambapo palimsaidia kushuka katika siri ya roho yake. Yeye ni nabii anayejua mawe ya jangwani na kupanda juu ya mlima.  Maneno ya mwisho ya Yesu kabla ya kukata roho msalabani ni maneno ya zaburi, yaani sala na sala ya wayahudi. Yeye alikuwa anasali sala ambazo alifundishwa na mama yake.

Yesu alikuwa anasali kama vile kila binadamu duniani. Hata hivyo namna yake ya kusali ilikuwa inajikita ndani ya fumbo yaani katika jambo fulani ambalo kwa hakika lilikuwa linajificha machoni pa mitume wake. Hiyo inajionesha wazi tunapo kutana katika Injili na mambo rahisi na ya haraka kama vile: Bwana tufundishe kusali (Lk 11,1).  Wao walikuwa wanamwona Yesu akisali na walikuwa na shauku ya kujifunza jinsi gani ya kufanya hivyo. “Bwana tufundishe kusali”. Yesu hakukataa, hana wivu na undani na Baba yake, bali alikuja kwa ajili ya kutufundisha ili tuwe na uhusiano na Baba, na kwa njia hiyo anageuka kuwa mwalimu wa sala kwa mitume, kama ilivyo kwa hakika sisi sote.Hata sisi tunapaswa kusema: “Bwana nifundishe kusali. Nifundishe”

Hata kama unasali kwa miaka mingi daima ujifunze

Hataka kama miaka mingi tunasali, Baba Mtakatifu anahimiza, tunapasa daima kujifunza:Sala ya binadamu ndiyo msingi unaotokana na  asili na katika roho yake, na labda ndiyo moja ya  fumbo nyeti la ulimwengu. Lakini hatujuhi kama sala ambayo tunasali kwa Mungu ndiyo ambayo kwa hakika anaisikiliza. Biblia inatoa ushuhuda wa maombi ambayo mwisho wake yanakataliwa. Mfano wa kukumbuka ni ule wa watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: Mfarisayo na mtoza ushuru : “Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; Hiyo ni kwa sababu gani? Baba Mtakatifu anongeza: mfarisayo alikuwa na kiburi na alipenda watu wamwone akisali na kujifanya kama vile anasali kijujuu. Moyo wake ulikuwa wa baridi. Yesu anasema kuwa, “kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”(Lk18,14).

Hatua ya kwanza ya kusali ni unyenyekevu

Hatua ya kwanza ya kusali ni kuwa mnyenyekevu, Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi, kwa maana ya kwenda kwa Baba na kusema Baba tazana mimi ni mdhambi, mimi mdhaifu na makatili… kila mmoja anajua jinsi ya kusema. Ni lazima kuanza kwa unyenyekevu na Bwana anasikiliza na Sala nyenyekevu unasikilizwa na Bwana.

Katika kuanza mzunguko wa katekesi kuhusu sala ya Yesu, jambo zuri zaidi na la hali ambalo wote tunatakiwa kufanya ni kurudia maneno na mitume wake: Mwalimu tufundishe kusali! Itakuwa vema katika kipindi cha Majilio kurudia: Bwana nifundishe kusali. Wote tunaweza kwenda kidogo zaidi ya hayo na kusali vema; lakini lazima kuomba Bwana. Bwana nifundishe kusali. Tufanye hivyo, katika kipindi cha Majilio na kwa hakika Yeye hatatuacha tuangukie katika utupu wa sala zetu. Amehitimisha Baba Mtakatifu.

 

 

 

 

 

05 December 2018, 15:00