Cerca

Vatican News
Tarehe 17 Desemba ni kumbukumbu ya kuazaliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko Tarehe 17 Desemba ni kumbukumbu ya kuazaliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko  (Vatican Media)

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Papa Francisko!

Baba Mtakatifu Francisko, amehitimisha mika 82 ya kuzaliwa. Ni mwaka wake wa 6 akisheherekea akiwa kama Papa. Katika Siku hii maalum, salam za matashi mema zimefika kutoka duniani kote

Sr. Angela Rwezaula

Imepita miaka 82 tangu tarehe 17 Desemba 1936, siku ambayo alizaliwa katika mji wa Buenos Aires nchini Argentina, mwanaume kwa jina Jorge Mario Bergogli (Papa FRancisko). Ni mtoto wa mhamiaji kutoka mkoa wa Piemonte nchini Italia. Akiwa mtoto mdogo anasema alikuwa anashauku ya kufanya kazi machinjioni.

Papa ni mtaalam wa kemia

Amekumbusha hayo akijibu swali la mtoto mmoja tarehe 31 Desemba 2016. Yeye pia anapendelea sana nyimbo, kwani alizaliwa katika familia yenye tabia ya kusikiliza  radio  kila wiki wakiwa na ndugu na mama,na hasa kusikiliza vipindi vya nyimbo ya sauti nzuri. Baba yake alimfundisha tangu akiwa kijana, umuhimu wa kazi. Na katika ujana wake ameweza kufanya kazi mbalimbali wakati huo huo akapata hata diploma ya utaalam wa kemia.

Wito wake

Lakini pamoja na hayo kuna kipindoimuhimu zaidi cha upeo wa maisha yake na nasaha za imani zilizotokana na bibi yake Rosa Margherita Vassalli,  na ambazo ziliweza kumfanya achanue katika wito wake. Kunako mwaka 1958 alijiunga na Seminari na kuchagua kuanza unovisi katika Shirika la Yesu (Wajesuit). Ni katika wakati huo, ambapo nesi mmoja Sista, Cornelia Caraglio, alimwokoa maisha yake kwa kumsihi Daktari akubali kumpa dozi ya dawa ya kutibu ugojwa wa pumu. Mwanamke huyo alikuwa mwenye akili, hata jasiri, hadi kufikia kujadiliana na madaktari. Hay ni kwa mujibu wa Baba Mtakatifu akimsifu sista huyo wakati alipokutana na wawakilishi wa waugizi katika mkutano wa tarehe 3 Machi 2018 na kuwaleza shukrani zake.

Ukuhani na barua ya bibi yake

Kunako mwaka 1969 alipewa daraja Takatifu la upadre. Siku hiyo bibi yake alimkabidhi barua, ambayo alikuwa inawalenga wajukuu wake na kwamba kijana Jorge Mario ndiyo aweze kuitunza katika kitabu chake cha sala. Katika barua hiyo bibi aliandika kuwa: “muwe na maisha marefu na ya furaha. Lakini kama siku moja kuna uchungu, kutokana na magonjwa au kupoteza mtu mpendwa na kukata tamaa, wakumbuke kupumua mbele ya Tabernakulo,mahali ambapo kuna shahidi aliye mkubwa zaidi  na mwenye hali ya juu akiwa na macho ya Maria ambaye yupo chini ya miguu ya msalaba kwa maana wanaweza kuangusha tome la dwa katika majeraha ya kina na katika uchungu”.

Askofu Mkuu wa Buenos Aires

Kunako mwaka 1973 alichaguliwa kuwa mkuu wa kanda ya wajesut wa Argentina. Na mwaka 1992 alipokea daraja ya uaskofu, na tarehe 28 Februari 1998 akatangazwa kuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires na kama  Mkuu wa Kanisa Argentina. Katika Mkutano wa tarehe 21 Februari 2001 Mtakatifu Yohane Paulo wa II alimteua kuwa Kardinali. Katika fursa hiyo, Mtakatifu Yohane Paulo II alisema: “leo hii  Kanisa katoliki la Roma, linakusanyika kwa pamoja kuzungukia makardinali wapya na kuwakumbatia kwa shange kuu, kwa utambuzi wa kuandika  katika sura mpya yenye ya maana katika  historia. Sura mpya ya historia inajirudia tena ya kugeuza kurasa, ambapo kunako mwaka 2013, iliandikwa Papa wa Kwanza kutoka katika Bara la Amerika na Mjesuit wa Kwanza kuwa Papa.

Uchaguzi katika kiti cha mtume Petro

Mara baada ya Baba Mtakatifu Mstaafu kuomba kung’atuka katika kiti cha Petro, waliunganika katika uchaguzi kwa mara nyingine tena Makardinali. Tarehe 13 Machi 2013, akachaguliwa kuwa Baba Mtakatifu. Wakati wa ziara yake ya kitume katika Parokia moja kunako tarehe 19 Februari 2017, mtoto mmoja alimuuliza swali, kwanini aliamua kuwa papa? Yeye alijibu: “Kile wanacho chagua, si lazima kiwe na akili nyingi.  Bali ni kile ambacho Mungu anapendelea kuwapa Kanisa kwa kipindi hicho”. Kama Papa, alichagua jina la Francisko. Siku chache baada ya uchaguzi, alipokutana na wawakilishi wa vyombo vya habari, alielezea kwa nini alichagua jina baada ya kumfikiria Mtakatifu Francis wa Assisi. Baba Mtakatifu alisema: “mtu wa maskini, mtu wa amani, mtu anayependa na kulinda mazingiria. Na ndiyo ishara hai ya maeneleo kama kiongozi kwa wosia wake  wa Laudato Si , unaojikita kutazama ungozi wake kama Papa Francisko.

17 December 2018, 16:40