Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na kikundi cha wanakwaya waitwao wanafunzi wa mbingu wakiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chama hicho Baba Mtakatifu amekutana na kikundi cha wanakwaya waitwao wanafunzi wa mbingu wakiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chama hicho  (Vatican Media)

Papa:wimbo na muziki ni lugha za kushuhudia Injili!

Baba Mtakatifu Francesco amekutana na “wanafunzi wa mbingu”, ni kikundi cha vijana kilichoundwa tangu mwaka 1968 kwa ajili ya kutangaza Injili kwa njia ya muziki na wimbo na ili kushinda kila aina ya vizingiti. Wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanza kwa chama hicho na amewahimiza waeneze ujumbe wa amani na undugu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, amekutana mjini Vatican na kikundi wanakwaya waitwao “Wanafunzi wa mbingu”, tarehe 10 Novemba 2018. Hiki ni kikundi cha vijana ambacho tangu mwaka 1968 wanatangaza Injili kwa njia ya muziki, nyimbo na tamasha katika nchi yote Italia  na Ulaya kwa ujumla. Mwaka huu wanatimiza miaka 50 tangu kuanza kwa chama hiki.

Maadhimisho ya miaka 50 ya chama; miaka 10 ya kifo cha mwanzilishi wa kikundi

Wakati wa kuanza hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko ameonesha furaha kubwa ya kuwapokea katika fursa yao ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chama hicho na miaka 10 tangu kifo cha mwanzilishi wao ambaye alikuwa ni Mjesuit, Padre Giuseppe Arione. Pia kuonesha furaha kubwa kuhusu hali halisi ya chama kinachoundwa na makundi mawili, ya  Revival na Amen. Hiki ni  chama kinachojikita katika kutunza  ule ukale na umaarufu wa Taasisi ya kijamiii ya Torino na chenye lengo  la elimu na ambacho kimewezesha kuendeleza uzoefu wa tasaufi ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola, amebainisha Papa. Kwa msaada wa Msimamizi wao padre Piero Granzino, wanajitahidi kushuhudia Injili kwa njia ya muziki na nyimbo ili kuweza  kufikia moyo wa watu  wengi hata walio mbali na Kanisa au imani!

Baba Mtakatifu amesema: Utume wao unajikita katika karama na ushuhuda wa Padre Arione ambaye kwa kufuata mwongozo wa Mtaguso II wa Vatican kwa ajili ya Kanisa katika mazungumzo, na dunia ya leo, kwa  mwaka 1968, alionesha mantiki ya mtindo wa kukaribisha. Aalijikita katika mtindo wa kichungaji aliotumia muziki na nyimbo kama lugha yenye uwezo wa kuonesha kwa namna ya ulimwengu, uzuri na nguvu ya upendo kikristo. Alikuwa anakwenda katika kona za barabara, hata mahali ambapo Kanisa lilikuwa bado  halijafika ili aweze kukutana na watoto na vijana, mahali popote walipokuwa na kupanga nao.

Lengo ni kuinjilisha kwa njia ya nyimbo

Na kwa wote bila kuacha nyuma hata mmoja walimpenda na kupendekeza safari ya imani na kindugu. Lengo lake lilikuwa ni uinjilishaji kwa njia ya nyimbo, na kupendekeza imani ambayo inatangaza na kuimba upendo wa Mungu kwa kuanzisha urafiki na kushirikishana kindugu.

Baba Mtakatifu anawatia moyo waendeleze mbele karama ya ukarimu wa Mjesuit huyo na kupyaisha katika mitindo hiyo,  lakini kwa kuhifadhi karama ya kinabii ambayo bado ni muhimu na kuhitajika leo hii katika dunia. Na ili kufanya hivyo ni lazima kutunza  maisha binafsi ya ndani,na ili wasiache waibiwe na migongano ya  kidunia,  lakini waweze kuikuza kwa njia ya sala, kitubio na Ekaristi. Kwa kufanya hivyo, sauti zao na nyimbo zao zinaweza kuwa si tu zenye kuvutia na muziki, bali zinazotajirishwa na ushuhuda wao wa maisha ya kikristo kwa kukuza undani  mwao ile tabia ya kusikiliza utashi wa muungano na Mungu. Na kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu amesema, watakuwa daima wenye shauku inayong’aa katika Injili.

Utume wao unachimba mizizi kutoka katika utamaduni wa Maandiko Matakatifu

Baba Mtakatifu akiendelea amasema: Utume wao unachimba mizizi katika utamaduni wa Maandiko Matakatifu kwa namna ya pekee katika Zaburi ambayo inawaalika waadhimishe Bwana kwa kinubi , waimbe na zeze na kusifu kwa nyuzi za  kidanda na filimbi (taz Zb 33; 150) Ili kuimba vizuri inahitaji kuwajibika na kuwa na matashi mema, lakini ni nguvu yenye kupendeza, kwa sababu inaamsha mioyo na kuwa makini katika kusikiliza sauti ya Roho, hasa wakati wanapojibidisha katika maadhimisho ya Liturujia mbalimbali, kwa kuruhusu waamini waweze kuwana wakati mzuri wa kina na muungano na Mungu, hivyo basi wanasaidia kuelezea hili kwa furaha, imani, kutubu na upendo… Wimbo ni lugha ambayo inapelekea muungano na mioyo; Anawashukuru Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee kwa sababu ya kushinda kila aina ya mipaka wanaeneze ujumbe wa amani na kindugu.

Kwaya inaleta uzoefu wa furaha na uzuri wa umoja

Katika kwaya yao, wanafanya uzoefu wa furaha na kuleta uzuri wa umoja. Kwa maana hiyo anawashauri wawe na umoja hata katika maisha yao ya kila siku , iwe kati yao na hata kwa wengine. Na zaidi wazingatie kwamba kwa ajili ya uzuri wa nyimbo zao, watatambuliwa kama mitume na mashuhuda wa Kristo , wakipendana wao kwa wao kama Yeye alivyotupenda. Kwa maana hiyo wao wanashauriwa  kuwa na moyo na roho moja. Kwa ajili ya wengine wakikumbuka mwanzilishu wao katika kukuza masikini na waliobaguliwa, wanaweza kupenda kupokea watu katika jumuiya na familia, kuwasikiliza, kuimba kwa pamoja Injili ya wadogo. Huo ndiyo mtindo wa kuwa Kanisa la Kimisionari, lenye uwezo wa kuambukiza na kuvutia wale ambao wanasubiri, labda bila kujua namna ya kukutana na Yesu. Kadhalika anahitimisha akiwaomba, watafakari mara nyingi Neno la Padre Arione: Tembea kwa ajili ya kutafuta wengine na simama kwa ajili ya kujitafuta binafsi. Tabasamu ya nyuso zao, uzuri wa sauti zao na umoja wa nyimbo zao zinajieleza na kujiweka moja kwa moja katika sala na kuwawezesha kutoa mlio mzuri kwa wale ambao  wanasikiliza kwa furaha ya kweli ya maisha na matumanini ya wakati endelevu. Baba Mtakatifu anawatakia mema na kwa niaba ya Kanisa anawapongeza kwa ajili ya utume wao wanaoufanya katika Kanisa na katika jamii!

10 November 2018, 14:00