Papa Francisko amekutana na Chama cha "Giorgio La Pira" mjini Vatican na kuwahamasisha waige mfano wa maisha ya Mtumishi wa Mungu anayebeba jina la Chama chao Papa Francisko amekutana na Chama cha "Giorgio La Pira" mjini Vatican na kuwahamasisha waige mfano wa maisha ya Mtumishi wa Mungu anayebeba jina la Chama chao 

Papa:upo ulazima wa kuwa na walei waaminifu katika kipindi kigumu!

Katika kipindi kigumu cha kisiasa nchini Italia na kimataifa kuna ulazima wa kuwa na walei waamini kama ule wa Mtumishi wa Mungu, Girogio La Pira. Kwa maana hiyo, leo hii tunatakiwa kuwa manabii wa matumaini,manabii wa utakatifu ambao hawana hofu ya kuchafua mikono, kufanya kazi na kuendelea mbele. Leo hii kuna haja ya kuwa mbayubayu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu wapendwa, ninayo furaha ya kukutana nanyi wakati mkiudhuria mkutano wa kitaifa wa vyama mbalimbali vinavyo husika na  Mtumishi wa Mungu Giorgio La Pira. Ninawasalimia kila mmoja na kushukuru Mwenyekiti wa Chama cha Giorgio La Pira kwa maneno yake. Ninawatakia matashi mema wa mkutano wenu wa tafafakari na mafunzo ili uweze kuwafanya mkue katika jumuiya, kanda zote za Italia mahali mlipo, kwa shughuli kwa ajili ya maendeleo fungamani ya watu. Ni mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 23 Novemba 2018, wakati alipokutana mjini Vatican na wanachama cha “Giorgio La Pira”, Chama ambacho kinamuenzi Mtumishi wa Mungu Giorgio La Pira.

Katika kipindi kigumu cha kisiasa Italia na kimataifa kuna ulazima wa walei waamini

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake, anasema kuwa, katika kipindi kigumu cha maisha ya kisiasa na kimataifa, kuna ulazima wa kuwa na walei waaminifu na watu wa hali ya juu kibinadamu na wakristo kwa ajili ya huduma kwa manufaa ya ya wote, kadhalika ni muhimu kugundua kwa upya sura ya Girogio La pira,ambaye ni  mfano wa kuigwa kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya ulimwengu wa sasa. Alikuwa shahidi wa shauku ya Injili na nabii wa nyakati zile na za kisasa; mtazamo wake mara zote uliongozwa na mtazamo wa Kikristo, wakati matendo yake mara kwa mara yalitanguliza zaidi ya muda wake.

Shughuli za mafundisho na jitihada za katiba ya Italia

Katika shyìughuli zake zilikuwa mbali mbali na hasa katika kufundisha Chuo Kikuu huko Firenze, lakini pia hata Siena na Pisa,wakati huo huo pembeni mwake aliweza kutoa  maisha yake katika matendo mbalimbali  ya upendo kwa mfano na kuudhuduria misa ya Maskini katika Parokia ya Mtakatifu Procolo. Kunako mwaka 1938 aliweza kuishi katika Koventi ya Mtakatifu Marco mahali ambapo alinzisha mafunzo ya Mababa wa Kanisa, aliandika na kuwa mwariri wa magazeti msingi, wakati huo hakukukoa kuzungumzia masuala ya udikteta wa wakati huo, hadi mapolis kutaka kumkamatana, na ndipo akakimbilia mjini Vatican. Akiwa mjini Vaticana katika  nyumba ya Katibu Mkuu msaidizi wa Vatican wa wakati ule Montini aliweza kumpongeza sana juu ya wajibu wake na jitihada zake za dhati katika jamii. Kunako mwaka 1946 alichaguliwa katika kamati ya serikali na kutoa mchango mkubwa katika Katiba ya Jamhuri ya Italia. Lakini utume ulijionesa wenye manufaa kwa wote na kutambuliwa kuwa wa hali ya juu alipochaguliwa kuwa Meya wa mji wa Firenze katika miaka ya hamsini. La Pira alijikita wajibu wake wa kisiasa ulio kuwa wazi kwa mahitaji ya wakatoliki,kijamii na daima akiwa anawatazama walio wa mwisho, sehemu kubwa ya watu wadhaifu.

Uhamasishaji wa mipango ya amani kijamii na kimataifa

La Pira alijikita katika kuhamasisha mipango ya kuhamsisha amani kijamii na kimataifa, kwa kuandaa mkutano kimataifa kwa ajili ya amani na ustaarabu kikristo pia hai katika hatua za kupinga vita vya kinyuklia. Mfano wake msingi ni wa kuigwa kwa  wale anaojikita katika shughuli za umma Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza, na wote wanaalikwa kuwa makini katika hali halisi hasi ambazo Mtakatifu Yohane Paulo II alizitaja kuwa ni mifumo ya dhambi (taz  Sollicitudo rei socialis, 36, ya tarehe 30 desemba 1987 inayohusu matatizo ya taalimungu za kisasa). “Na hiyo inajikita katika mantiki kwa maana ya kuwa katika hotuba ya mwenyekiti wenu, mara mbili amesama neno:“kipindi cha kuchanua”. Leo hii inaihitaji kuchanua. Leo hii tunatakiwa kuwa manabii wa matumaini, manabii wa utakatifu ambao hauna hofu ya kuchafua mikono, kufanya kazi na kuendelea mbele. Leo hii kuna haja ya kuwa mbayubayu na hivyo ndiyo ninyi”, Baba Mtakatifu amebainisha.

Umuhimu wa kuhifadhi urithi wa La Pira

Baba Mtakatifu Francisko anasitiza juu ya umhimu wa kuhifadhi urithi wa La Pira katika uzoefu wao mbalimbali wa vyma vyao na ambao unajikita kama talanta ambazo Bwanaanaomba kwa kila mmoja ziweze kuongezeka. Anawahimiza zaidi kuthamanisha zile fadhila za kibinadamu na kikriso ambazo ni sehemu ya urithi wa mawazo ya kitasaufi ya Mtumishi wa Mungu Giorgio La Pira. Na kwa namna hiyo, wao wanaweza kujikita katika maeneo yao na miji wanayoishi kuwa wahudumu wa amani na mafunzo ya haki, ushuhuda, mshikamano na upendo. Kuwa kama chachu ya thamani za kiinjili katika jamii,hasa kwa mantiki ya utamaduni, wa kisiasa;  na wanaweza kupyaisha kwa shauku kubwa kujituma kwa ajili ya wengine na kuwapa furaha na matumaini!

Chama cha Giorgio La Pira ba shughuli zake

Kuhusu chama hiki cha Giogio La Pira lilikubaliwa kuwa chama cha Kimaadili, kwa utambuzi wa Hati ya Serikali kunako tarehe 28 Machi 1996 na kutangazwa katika Gazeti rasmi tarehe 12 Aprili 1996.  Katika  maandiishi  yake ya mirathi, La Pira alimteua kuwa mrithi wa ulimwengu wote Konventi ya Mtakatifu  Marko kwa  usimamizi wa Shirika la Wadomenikani, ambapo hadi sasa wanahudumu,wakati huo huo akawateua  èia hata wahudumu wake wa karibu Pino ARPIONI, Fioretta MAZZEI na Antinesca TILLI. Shughuli hiyo ya Waraka wake na urithi wa ulimwangu, ulianza tangu Januari 1978 mara tu baada ya miezi michache ya kifo cha Pira ,na  Chama hicho kilichokuwa na lengo la kuhamasisha ili kuzaliwa rasmi. Kusudi la Chama hicho na hadi sasa ni “kukuza mipango ya kiutamaduni na kijamii kwa jina la Profesa Giorgio La Pira ili kufanikisha kuendeleza mawazo na hatua  za matendo kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa, kuhifadhi na kutumia kwa madhumuni ya kisayansi na kiutamaduni Maktaba ya Profesa Giorgio La Pira”.

23 November 2018, 15:59