Tafuta

Vatican News
Papa wakati wa salam baada ya katekesi, amewakumbusha kusali kwa ajili yake, ili apate kuimarisha waamini imani Papa wakati wa salam baada ya katekesi, amewakumbusha kusali kwa ajili yake, ili apate kuimarisha waamini imani  (Vatican Media)

Siku kuu ya kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Mt. Yohane wa Laterano

Wakati wa kutoa salam zake Baba Mtakatifu mara baada ya katekesi yake, amewakumbusha mahujaji na waamini juu ya Siku kuu ya kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano Ijuma tarehe 9 Novemba. Ameomba waamini kumwombea katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya katekesi yake, Baba Mtakatifu amewasalimia mahujaji katika lugha mbalimbali na kati yao pia  washiriki wa Mkutano wa kwanza kimataifa wa Chama cha  wanaume unaofanyika mjini Roma kwa siku hizi. Amekumbusha kuwa siku ya Jumapili ijayo itakuwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 100 ya huru nchini Poland, amewatakia matashi mema watu wote wa Poland, ili waweze kuishi zawadi ya uhuru katika amani na matarajio ya kujenga nchi yao katika wakati endelevu unaojikita katika kurithi daima tasaufi ya walio watangulia na upendo kindugu.

Siku kuu ya kutabarukiwa kwa Kanisa kuu la Mt. Yohane wa Laterano la Roma

Baba Mtakatifu amekumbuka juu ya siku ya Ijumaa 9 Novemba 2018, kuwa ni sikukuu ya Ukulu wa Kanisa Kuu la Latenano , Kanisa Kuu la Askofu wa Roma, kwa maana hiyo, ameowaomba wasali ili Papa aweze kuwaimarisha ndugu katika imani. Na katika Lugha ya kingereza, pia Papa Francisko amesalimia mahujaji kutoka Denimark, Japan, Ufilippini na Marekani na wote amewatakia matashi mema na Mungu awabariki

        

07 November 2018, 15:44