Papa amekutana na Wanafunzi wa Shule Katoliki ya Uandishi nchini Ujerumani Papa amekutana na Wanafunzi wa Shule Katoliki ya Uandishi nchini Ujerumani 

Papa Francisko:Ninyi hamfanyi kazi, bali mnatimiza zoezi na wajibu!

"Tuweze kuwasaidia watu wafungue macho yao na masikio, na zaidi juu ya mioyo yao yote ili waweze kuwa walinzi wa kila mmoja na kutambua kuwa ni wana na wa Baba mmoja”. Ndiyo maombi ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake alipokutana na wanafunzi wa Shule Katoliki ya Uandishi wa habari kutoka Ujerumani

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 9 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wanafunzi wa Shule Katoliki ya Uandishi wa Habari kutoka Ujerumani ambapo amewakaribisha wote kwa furaha. Katika hotuba yake Baba Mtakatifu anasema, “wote mnatoka katika Taasisi inayo hamasisha kizazi kipya kuhusu matangazo. Anamshukuru Mkurugenzi wa chuo hicho, Bwana Bernhard Remmers na Ndugu Mdogo Mkapuchini,  Helmut Rakowski O.F.M.Kap. kwa hotuba na salamu zenu!

Uandishi  wa habari ya Kanisa Katoliki nchini Ujerumani

Akiendelea na hotiba yake amesema: Miaka hamsini iliyopita, baada ya Mtaguso wa II wa Vatican, ilianzishwa Shule ya Uandishi wa habari ya Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, kwa lengo la kuwapa majukumu watu wanaofanya kazi katika vyombo vya habari. Tangu wakati huo huo, chuo hicho kinatoa waandishi wenye kuwa na taaluma na wanaofanya kazi, kama wakristo katika jamii.

Baba Mtakatifu amewapongeza kwa moyo wote, wahusika na wanafunzi waliomalizi katika Taasisi hiyo, marafiki na wote wanaosaidia kufanikisha shughuli hiyo. Ameongeza kusema: Ujurumani, inaweza kujivunia kwa kutambua kuwa wapo waliohitimu na kupata diploma kutoka katika Tasisi hiyo (IFP) na kati yao ni waandishi, ambao wanafanya kazi katika vyombo vya habari kijamii, hata vya Kanisa.

Ninyi hamfanyi kazi, bali mnatimiza zoezi na wajibu

Kwa kufafanua zaidi Baba Mtakatifu Francisko anasema: ni uandishi gani wa kikristo unawatofautisha matendo yao chanya kuelekeza kwa mtu na kwa ajili ya maadili yao ya kitaalamu: “Ninyi hamfanyi kazi, bali mnatimiza zoezi na wajibu”. Ni jinsi ani  gani ilivyo rahisi kuacha maadili hayo na  na kuwambukizwa maoni ya umma ya pamoja, ya kughushi, na kusambaza na kuchochea! Katika mazoezi, hayo kama waandishi wakati mwingine  hawakabiliani  zaidi na ubaya, bali wanaruhusu mambo yaende jinsi yalivyo au kama baadhi wameamua kwenda mbele (Gaudete et Exsultate 137).

Baba Mtakatifu anawasihi kwa namna hiyo, “Tuombe kwa sauti moja, tuombe na uhuru utokao kwake  Roho Mtakatifu, kwamba atusaidie kuamini katika ukweli wa Kristo ambaye hutufanya tuwe huru. Tukiwa tunakwenda zaidi vizingiti vya huzuni na kujiachia, tuweze kuwasaidia watu wafungue macho yao na masikio, nazidi hasa  juu ya mioyo yao yote ili waweze kuwa walinzi wa kila mmoja na kutambua kuwa ni wana na wa Baba mmoja.

Asante kwa sababu mnazungumza mambo mazuri, labda yasingeishia ukurasa wa kwanza

Akihitimisha kwa vijana wanafunzi hao anawashukuru kwa kusema: Asante kwa sababu kama waandishi wa habari mnawaangalia watu na mnatoa wito dhidi ya ukosefu wa haki na kuonesha kile ambacho ni chenye haki. Asante kwa sababu mnazungumza juu ya mambo mazuri ambayo labda yasingeweza kuwekwa katika ukurasa wa kwanza, lakini ambayo huwaweka watu katika kitovu. Asante kwa sababu ya mtindo wa kikristo unaoongoza kazi ya Kanisa.  Ninawatakie matashi mema mwendelee kufanya uandishi wa habari wa watu na kwa ajili ya watu. Tafadhali msisahu kusali kwa ajili yangu”.

09 November 2018, 15:21