Tafuta

Mwenyeheri  Giuseppe Toniolo ni baba wa familia,aliyekuwa mstari wa mbele katika masuala ya Kanisa na kijamii Mwenyeheri Giuseppe Toniolo ni baba wa familia,aliyekuwa mstari wa mbele katika masuala ya Kanisa na kijamii 

Papa:kuna ya haja ya wakatoliki kuiga mfano wa Toniolo!

Katika Barua ya Baba Mtakatifu kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Milano, iliyotiwa saini ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vartican , katika fursa ya mkutano juu ya Mwenye heri Giuseppe Toniolo, akiadhimishi miaka 100 tangu kifo chake,anawatakia wakristo waitalia waige mfano wa mwalimu wa mafundisho ya kijamii na kushinda vishawishi vya utofauti

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemtumia barua Askofu Mkuu Delpini wa Jimbo Kuu la Milano katika fursa ya kukumbuka ya miaka 100 tangu kifo cha Mwenye heri Giuseppe Toniolo. Katika barua yake iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Baba Mtakatifu anaonesha furaha kubwa katika fursa ya maadhimisho ya Miaka 100 ya kifo cha Giuseppe Toniolo, siku iliyoandaliwa katika Makao ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano. Ni mkutano ambao umeandaliwa kwa ajili ya heshima ya sura ya Baba wa familia na wakuigwa mwalimu wa uchumi  na mfano wa utakatifu wa walei kwa maana hiyo anawatakia wakristo waitalia wajifunze kutoka kwa mwalimu huyo wa mafundisho jamii na kishinda vishawishi vya utofauti wakati huo wakijikita kutafuta njia za michakato ya umoja unaoelekeza mapendekezo ya dhati katika jamii. Kuanzisha kwa tukio hilo ni mwafaka ili kuweka mwanga, si tu kwa wale wanaostahili wa kihisotria, lakini pia watu wa sasa kama mwenye Heri Tonioliìo, kwa kuvutiwa na ushuhuda wake na mawazo mapya ya kuigwa katika wajibu wa kijamii na kisiasa, ambapo kwa wakatoliki hawawezi kuacha, na iwapo wanataka kuwa waaminifu wa Injili. Kwa hakika profesa asili wa Venezia japokuwa mzaliwa wa Pisa anabaki daima kuwa mwalimu na kwa maana nyingine ni manabii. Katika mambo mengi aliyoyafanya ya kuweze kuwa ya wakati wetu.

Kati ya 1845-1918 ilikuwa kipindi cha mabadiliko

Miaka aliyoishi kati ya 1845-1918, ilikuwa ni kipindi cha mabadiliko makubwa sana, kwa namna ya pekee  katika mchakato wa viwanda, alitoa sura mpya ya jamii na matokeo hayo yalikuwa yanalenga, kama Papa Leone XIII alivyokuwa ameandika katika waraka wake wa Rerum Novarum  kuwa “kuna ulazima wa kila mmoja kuinglia kati  na kusadia bila kusita na kwa kutafuta fursa kwa wafanyakazi ambao sehemu kubwa wanajikuta katika hali mbaya na isiyo stahili ubinadamu. Ongezeko la ukiritimba wa uzalishaji na biashara, na kwamba kuna idadi ndogo sana ya watu matajiri ambao wanafanya mchazo usiokuwa na maana katika kutoa huduma (Waraka, Rerum Novarum 2). Wakati huo katika barua hiyo Papa Leone aliwaalika waamini wachukue majukumu ya masuala ya kijamii, akiwashauri wajikite kwa dhati katika kutafuta jibu katika mwanga wa kujipyaisha, jibu kubwa ambalo linatoa upumuaji, lenye uwezo wa kwenda katika mzizi wa matatizo.  Kulikuwa na hatari ya kwamba katika dunia ya wafanyakazi wangeweza kujiingiza katika hali mbaya na kuwa mateka wa itikadi ambazo zingekuwa  ngumu na kuleta matatizo makubwa na vigumu kuweza kupata suluhisho.

Mwenye heri Toniolo aliandaa Kongamano kwa ajili ya kumsaidia Papa katika hali ngumu katika masuala ya Roma

Mwenye heri Toniolo alijikuta katika utume huo wa kijamii  kwenye maisha yake, kwa wakatoliki wa Italia, aliandaa kazi ya Kongamano hasa kwa ajili ya kumsaidia Papa katika hali ngumu ya masuala ya Roma na kupelekea ufunguzi wenye upeo kwa mtamzamo wa mwanga, juu ya michakato ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Utafiti wake wa mafunzo, mwenye uwezo wa kupenda ukweli hadi kwenda kunyume na mambo ya sasa, iliweza kumsaidia kutambua fundo la masuala ya kijamii, kuyaelewa katika uchumi tofauti na maadili yaliyoendelezwa katika wimbi la sheria ya faida, katika utupu au udhaifu wa mihimili ya kati na mashauri muhimu kwa ajili ya manufaa ya walio dhaifu zaidi katika jamii

Ndani ya moyo wake alikuwa na  ufahamu kwamba, kukutana kati ya imani na utamaduni inawezekana kuondoa jamii ya kisasa kujijali

Toniolo alikuwa mstari wa mbele bila kuchoka katika shughuli za kijamii , hata katika matendo na ya ishala ya ulimwengu uliopyaishwa. Ndani ya moyo wake alikuwa na mradi wake wenye  ufahamu kwamba, kukutana kati ya imani na utamaduni inawezekana kuondoa jamii ya kisasa katika kujali sana vitu vya kimwili na vinavyosimama tu juu ya upande mmoja na ili watu kuwa na uhuru na uhuru bila mipaka na vikwazo, kwa upande mwingine kundokana  na uongo wa sheria ya kuimarisha vikwazo na udhalimu. Toniolo kwa mawazo yake yalikuwa katika jamii ya kidemokrasia ambayo lengo lake la mwisho lilikuwa ni wema na ustawi wa jamii wa kuunganisha kwa nguvu zote za kijamii kwa ajili ya faida ya maskini zaidi. Na ili demokrasia iweze kuwa hivyo, japokuwa na  uwazi kwa kila mtu na kwa ushirikiano wa kila mtu, katika macho ya Mwenye Heri Giuseppe Toniolo hasingeweza kukamilisha, hilo bila kuchota kiini cha maisha katika thamani ya Injili, anasema Baba Mtakatifu Francisko

Hitimisho:Maono ya mwenye heri Toniolo ni kuona dunia ya amani

Maono haya, kutokana na nyanja ya kiuchumi na kijamii, yalikuwa ni makuu katika kanuni juu ya sayansi na utamaduni. Kwa sababu hiyo yeye alianzisha Chama cha Jamii katoliki Italia kwa ajili ya masomo ya kisayansi, tofauti na Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu. Maono hayo yalitoa mwamko mkuu katika maendeleo na kuwa na tabia daima ya kimataifa hasa wakati wa masalia ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Toniolo alionesha jinsi gani ya kuweza kuondoa matatizo na jinsi gani ya kuhakikisha amani kwa siku zijazo. Yeye aliomba Vaticankuwa mwahamasishaji wa Taasisi ambayo iwe kama maabara ya sheria ya haki za kimataifa ambayoo ianzishwe vizuri na pana ya kushirikisha. Nani asiyeona leo, matukio ya vita vya kikanda ambavyo mara nyingi husababisha hofu ya kuenea duniani, ni kiasi gani kuna haja hii ni ya haraka, ili kuunganisha haki za mataifa na mahitaji ya familia ya wanadamu wote? Baba Mtakatifu anahitimisha na swali: Je, si kushirikiana na Toniolo kwamba matarajio ya amani imara na ya kweli lazima yajengwe kwa kuunganisha heshima ya haki za binadamu na kushinda ubinafsi, kwa kupitia tena mahusiano ambayo mwanadamu huongeza, kwa misingi ya thamani takatifu ya maisha na thamani ya familia?  Ninawatakia mema katika mafaikio ya siku hiyo ya mafunzo na mafanikio.

Ni nani  huyu Toniolo?

Toniolo alikuwa Mtume wa Rerum Novarum , kiongozi wa Wakatoliki kijamii wa Italia na kwa namna ya pekee ni mmoja wa ushuhuda wa kijamii katika nyakati zile. Alifariki tarehe 7 Oktoba 1918. Tarehe 14 Juni 1971 Mtakatifu Pauli Vi aliliridhisa ushujaa wa fadhila za utakatifu na kuwa mtumishi wa Mungu. Alizaliwa huko Treviso kunako tarehe 7 Machi 1854 na kutangazwa Mwenyeheri kunako tarehe 29 Aprili 2012 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Roma katika Misa iliyoadhimishwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.

24 November 2018, 14:20