Tafuta

Vatican News
Wanahija kutoka nchini Albania wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko Wanahija kutoka nchini Albania wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko  (Vatican Media)

Papa:kuishi pamoja kati ya dini tofauti ni thamani na nguvu ya watu!

Alitetea kwa ujasiri thamani za kidini na kwa jina la kikristo hadi kufikia kupewa heshima ya jina la "mwanariadha wa Kristo”. Ni maelezo ya Papa kwa wajumbe karibia 200 kutoka nchini Albania, kufuatia na fursa ya maadhimisho ya miaka 550 tangu kifo cha shujaa wa Taifa Giorge Castriota Skanderbeg

Sr. Angela Rwezaula

Tarehe 19 Novemba jioni, katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko  amekutana na wajumbe karibia  200 kutoka nchini Albania, wakiwa katika hija yao kuanzia eneo la Aquile, kufuatia na fursa ya maadhimisho ya miaka 550 tangu kifo cha shujaa wa Taifa lao, Hayati Giorge Castriota Skanderbeg. Kati ya  wajumbe hao walikuwapo maaskofu, viongozi wa kisiasa, wa dini na watawa.

Wakati wa hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka wasifu  mkuu wa kiongozi ambaye kwa  karne ya XV aliweza kuunganisha Albania na kuilinda nchi dhidi ya mashambulizi ya Ottoman kutoka Uturuki. Kutokana hivyo amesema, Giorge Castriota Skanderbeg alitetea kwa ujasiri thamani za kidini na kwa jina la kikristo hadi kufikia kupewa heshima ya jina la “mwanariadha wa Kristo” na kujikita kwa dhati katika ishara zake za utambulisho wa utamaduni wa Albania. Utambulisho huo ulikuwa ni  jambo  kuu la ushirikiano na muungano wa Taifa, kwa kutafsiri kwa kiasi kikubwa ile  thamani ya imani na wajibu wake katika huru aliokuwa amejiwekea.

Fursa ya maendeleo na msimamo

Baba Mtakatifu Francisko ameendelea na hotuba yake katika nchi ya Aobania, hyuo ndiyp ulikuwa kwa dhati mwaka wa kitaifa wa Skanderberg” na tayari miaka 50 iliyopita, Papa Pauli VI alikutana na wawakilishi wa Albania kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 500 tangu kifo cha shujaa wa nchi hiyo ambapo katika fursa hiyo aliwataka kwamba madhimisho yasiishie katika sifa tu na mambo ya wakati uliopita, badala yake nchi ya Albania iwe ni fursa muafaka kwa ajili ya kupyaisha wajibu wa kila mmoja, wazalendo na kwa ajili ya maendeleo ya dhati na msimamo kwa namna ya kwamba kizazi endelevu cha vijana kisiweze kuwa na hali ya kuchagua  kuhama nchi na kudhoofisha nguvu ya nchi, na hivyo ni kuwajibika kwa dhati katika makuzi ya binadamu na raia.

Jumuiya ya arberesh

Baada ya kifo cha Skanderbeg  kunako mwaka 1468 na kufuatia mashambulizi ya waturuki, kwa dhati nchi ya Albania, alipendelea kuhama na idadi kubwa kupata makao nchini Italia hasa katika Mkoa wa Calabria na kisiwani Sicilia ambapo waliweza kuendelea utamaduni asili wa Kanisa la Albania wa Lungro ambao ni uwanda wa Albania na Grottaferrata. Hii ni jumuiya ya Arberesh ambao kwa utamaduni wao na lugha yao wameweza kuirithisha kizazi hadi kizazi na ambapo inatoa mtazamo wa picha halisi ya  hali ya nchi ya Albania ya wakati wa uongozi wa Skanderbeg na kuthibitisha kwamba ushujaa wa Albania, bado unabaki kuwa na thamani katika ngazi ya kuhifadhi kwa ufanisi wa mahusiano asili ya nchi yao.

Utambulisho wa kitasaufi na dini nyingi

Giorgio Skanderbeg, ambaye katika nembo yake inaonesha Tai mweusi na ndani ni rangi nyekundi ambayo ndiyo msingi wa bendera ya Albania;  kwa maana hiyo ndege huyo ndiye anayepeleka nchi ya Albania kuelekeza utambulisho wa kitasaufi ambao ulikuwa unaunganisha watu wa Albania, zaidi ya tofauti na tabia za dini zilizopo nchini humo. Kutokana na hiyo, Baba Mtakatifu Francisko, amekumbusha juu ya  ziara yake ya kitume aliyotembelea nchini Albania kunako mwaka 2014 ambapo aliweza kujionea hali halisi ya nchi  katika heshima na imani kati ya wakatoliki, waorthodox na waislam na kwamba ni thamani yenye msingi wa nchi ambayo inachota thamani ya hali ya  juu na maalum katika nyakati zetu hizi.

Hii yote inaonesha amani ya kuishi kati ya wazalendo wenye dini tofauti na  kwamba ndiyo njia ya dhati ya kujikita na ambayo inaweza kuzaa umoja, uhuru ulio ubora wa nguvu na ubunifu wa watu wote, kwa kuunda ule urahisi wa kuishi katika ushirikiano wa kweli na undugu. Ni kujikita katika mapenzi mema ya kufikiria tofauti kama fursa ya mazungumzo na kuheshimiana, kutambuana kwa kukuza zaidi maendeleo ya mchakato wa kitasaufi wa dhati na kugeuka kuwa mfano  ambao ni mwafaka unaotazama faida ya kujenga amani ya kudumu, inayojikita juu ya heshima ya hadhi na maisha ya binadamu.

Kumbukumbu ya mashahidi na Mama Teresa wa Kalcutta

Baba Mtakatifu katika hotuba yake, amewabariki kwa Baraka ya kitume wajumbe wote na watu wa Albania, akikumbuka Watakatifu Mashahidi ambao walitoa ushuhuda wao wa imani kwa gharama ya maisha yao na Mama Teresa wa Kalcuta.

 

 

 

 

20 November 2018, 10:40