Tafuta

Vatican News
Katekesi ya Papa Francisko 21 Novemba 2018 Katekesi ya Papa Francisko 21 Novemba 2018  (Vatican Media)

Papa:kazi ya sheria ni kumfanya mtu afungue moyo kwa Mungu!

Katika Katekesi ya Jumatano 21 Novemba 2018, Baba Mtakatifu ametafakari kuhusu Amri ya mwisho ya Mungu, ustamani mke hasiye wako na chochote alicho nacho jirani yako. Amri zote ni kutaka kukomboa roho ya mtu na tamaa zake mbaya. Na mtu hawezi kujikomboa pekee yake, bali lazima kufungua uhusiano na Mungu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ndugu wapendwa kaka na dada habari za asubuhi! Mikutano yetu juu ya Amri za Mungu leo hii inatufikisha katika amri ya mwisho. Tumeisikiliza katika somo. Hayo lakini siyo maneno pekee ya mwisho katika maandisho hayo, bali kuna zaidi, kwa maana ni utimilifu wa safari kwa njia ya Amri kumi kwa kugusa moyo katika kile ambacho tulikabidhiwa. Kwa hakika katika mtazamo, si kwamba inaongeza kitu kipya zaidi ya mantiki hiyo yaa “ustamani mke hasiye wako na cho chote alicho nacho jirani yako. Na kwa njia hiyo ni amri inayohusu uzinifu na kuiba; lakini maneno hayo je yanatumika wapi?  Je ni mhutasari? Ni jambo ambalo ni la ziada?

Ndiyo utangulizi tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kuanza katekesi yake, katika mwendelezo wa ufafanuzi wa Amri za Mungu kwa waamini na mahujaji wote waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano tarehe 21 Novemba 2018 ambapo amefikia hatua ya mwisho ya amri ya kumi ya Mungu.

Dhambi inatokana na nini?

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi huo anasema:inabidi kutambua kuwa amri zote zina kazi ya kuelekeza mpaka wa mwisho na  vizingiti zaidi ambavyo binadamu anajiharibu binafsi na jirani, na  kukosa kuonja uhusiano na Mungu. Iwapo unakwenda kinyume zaidi, ni kujiharibu binafsi na kuaharibu hata mahusiano na Mungu na wengine. Kutokana na hiyo amri kwa maana hiyo zinaonesha hili, kwa njia ya neno hili la mwisho linathibitishwa kwamba, ukiukwaji wa amri hizo unatokana na  mzizi mmoja wa ndani yaani tamaa mabaya. Dhambi zote zinatokana na tamaa mbaya, Baba Mtakatifu anakazina na kuongeza: “ndipo hapo yanaanza kuzungukia moyo na kuingia katika wimbi hilo na kuishia katika ukiukwaji, lakini siyo ukiukwaji rasmi  na wa kisheria, kwa maana ni ukiukwaji ambao hujeruhi binafsi na wengine.

Katika Injili Bwana Yesu analeza wazi kuwa, maana ni ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. (Mk 7,21-23). Kutokana na hili, ni utambuzi wa kwamba mchakato wote wa Amri kumi za Mungu hauwezi kuwa na maana iwapo haufikii kugusa ngazi hiyo ya moyo wa binadamu. Baba Mtakatifu Francisko anauliza, Je mambo yote hayo mabaya yanatoka wapi? Katika Amri kumi za Mungu zinaonesha wazi na kwa kina juu ya mantiki ya hitimisho lake  yaani katika amri ya kumi ya mwisho. Mchakato wa safari yake ni katika moyo, hasa  kama moyo hauna uhuru, hakuna chochote kinachofaa kitu. Hiyo ndiyo changamoto ya kuweza kutafuta uhuru dhidi ya mabaya yote hayo. Amri za Mungu zinaweza kupunguzwa thamani katika  uso wa maisha ambayo yanabaki vilevile tu kama ya utumwa  na siyo kuwa wana huru wa Mungu. Na mara nyingi Baba Mtakatifu anaongeza kusema, kujifunika na kitambaa kwa kufika mabaya ni kubaki bila kupata suluhisho.

Lazima kuacha kujifunika na kuficha mabaya

Baba Mtakatifu anasema ni lazima kuacha kujifunika kitambaa na kujificha ubaya wa amri juu ya tamaa, kwa sababu, amri hiyo inatufanya tujione umaskini wtu na kutupeleka katika unyenyekevu mtakatifu. Kila mmoja anaweza kujiuliza: je ni tamaa gani mbaya  inayo nishambulia mara nyingi? Wivu, kijicho na masengenyo? Kwa mambo yote mabaya yanayokuja nyuma yangu. Kila mmoja anaweza kujitafakari na itakuwa ni vema kila mmoja kufanya hivyo ameshauri Baba Mtakatifu. Binadamu anahitaji unyenyekevu huo, ambao unamsadiaia aweze kujikomboa na ambapo anatoa kilio kwa Mungu aweze kukombolewa. Mtakatifu Paulo anaelezea vema hasa akijikita kufafanua juu ya amri kuhusu tamaa ( Rm 7,2-24).

Kusahihishwa kwa njia ya Roho Mtakatifu

Ni vigumu kufikiria kwamba unaweza kujisahihisha bila kuwa na zawadi ya Roho Mtakatifu. Ni kazi bure kufikiria kujitakasa mioyo yetu kwa juhudi na utashi wetu, na kwa maana hiyo haiwezekani. Ni lazima kujifungulia mahusiano na Mungu, katika ukweli na uhuru. Ni kwa njia hiyo tu juhudi zetu zinaweza kuleta matunda  kwa maana yupo Roho Mtakatifu anayetupeleka mbele.

Kazi ya Sheria ya kibiblia siyo ile ya kukataisha tamaa binadamu ambaye kwa utii wa maandisho unampeleka awe na  wokovu wa juu na zaidi usiowezekana. Majukumu ya Sheria ni kumpelea mtu katika ukweli wake, ikiwa ni pamoja na umasikini wake ambao unageuka kujifungulia katika ukweli binafsi wa huruma ya Mungu, ambayo inambadili na kumpyaisha. Mungu mmoja, anao uwezo wa kupyaisha mioyo yetu, kwa mkataba ya kwamba, nasi pia tunafungulia mioyo yetu na ndiyo moja ya sababu ; Yeye anafanya kila kitu lakini kabla ya yote, hata sisi lazima kumfungulia mioyo.

Sisi ni waombaji hivyo tuache tuongozwa mioyo yetu na  Roho Mtakatifu

Maneno ya mwisho ya Amri za Mungu yanafundisha wote kujitambua kuwa ni waombaji; yanasaidia kujiweka mbele ya mchanganyo wa moyo wetu ili kusitisha kuishi ubinafsi na kugeuka kuwa maskini wa roho, wa kweli,  kwa mfano wa Baba Mungu na kuacha ugeuke kuwa Mwana anayefundishwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni mwalimu anayetuongoza na kwa hiyo tuache tuongozwe na yeye. Sisi ni waombaji, na tuombe neema hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amehimiza!

Heri masikini wa Roha maana Ufalme wa mbingu ni wao (Mt 5,3) Ndiyo, wenye heri ni wale wasio jidanganya kujiokoa wenyewe kwa kuamini kuwa wanaweza kujioka na udhaifu bila msada wa Mungu ambaye peke yake anaweza kuponya. Ni kwa njia ya huruma ya Mungu anaye ponyesha moyo. Heri wale wanaojitambua tamaa zao mbaya na kwa moyo uliopondeka, kujinyenyekeza na hawakai mbele ya Mungu na wengine kama vile ni wenye haki, badala yake wanajiona kuwa wenye dhambi. Ni jambo jema  ambalo Petro alisema kwa Bwana: “ Nenda mbali nami Bwana kwa sababu mimi ni mdhambi. Baba Mtakatifu amehitimisha: ni sala nzuri hiyo ya kusema “ nenda mbali Bwana maana mimi ni mdhambi”. Hao ndiyo wanao tambua kuwa na upendo na wanatambua kuwa na huruma kwa wengine, kwa sababu wamefanya uzoefu juu ya maisha yao binafsi.

 

21 November 2018, 14:50