Vatican News
Papa Francisko akiwahutubia Waseminari wa Jimbo  Kuu la  Agrigento anawataka wajikite katika utume wa kweli, hasa wa kusikiliza kilio cha watu Papa Francisko akiwahutubia Waseminari wa Jimbo Kuu la Agrigento anawataka wajikite katika utume wa kweli, hasa wa kusikiliza kilio cha watu  (Vatican Media)

Papa:Kanisa linawaita kusikiliza kilio cha binadamu!

Katika mkutano na waseminari wa Jimbo Kuu la Agrigento, Baba Mtakatifu Francisko, amezungumza nao kwa urahisi na kuwakabidhi hotuba yake aliyokuwa ameiandaa, wakati huo huo amefafanua baadhi ya ufunguo wa maneno msingi katika maisha yao ya baadaye katika ukuhani

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumamosi tarehe 24 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na waseminari kutoka Jimbo Kuu katoliki la Agrigento nchini Italia. Amezungumza nao bila kusoma hotuba yake aliyoiandika na kuwakabidhi. Hata hivyo wakati wa kuzungumza anawashukuru kumtembelea na kwa namna ya pekee anamshukuru Gombera. Kwa muda kitambo amependa kuwashauri baadhi ya takafari binafsi na kijumuiya ambayo ameyatoa katika Sinodi ya vijana. Katika hotuba aliyo wakabidhi jambo la kwanza anawashauri watazame sura ya mitume wa Emau.

Jambo la kwanza ni picha ya kibiblia ile ya safari

Hawali ya yote ni sura ya bibiblia ya Injili ya mitume wa Emau. Baba Mtakatifu amependelea kuwakabidhi picha hiyo kwa sababu iliwaongoza katika kazi ya mwisho ya Sinodi na ambayo inaweza kuendelea kuvutia katika safari yao. Kwa hakika ni neno la safari  ambalo ni ufunguo wa kwanza. Baba Mtakatifu anasema, Yesu aanakutana nasi katika safari na wakati huo huo yeye ni njia, yaani hali halisi ya kila mmoja ambaye analikwa kuishi na ni ndiyo mchakato wa kina , njia ya imani na matumaini ambayo inatambua kipindi cha mwanga na kile cha giza. Na hapo katika safari Bwana anakutana nasi, anatusikiliza na kuzungumza nasi, baba Mtakatifu anasisitiza.

Ufunguo wa pili ni kusikiliza

Baba Mtakatifu akiendelea n ana ufafanuzi anasema, hawali ya yote Bwana anatusikiliza. Na ndiyo ufunguo wa neno la pili. Bwana Mungu wetu ni Neno na wakati huo huo ni mkimya, akiwa anasikiliza, Yesu ni Neno aliyejifanya msikilvu anatokea katika hali yetu ya ubinadumu. Yeye alipojitokeza huku Emau  katikati ya mitume wakati wa safari yao akiwa nao aliwasikiliza na hata kuwasaidia kwa njia ya maswali ili waweze kutoa kile walicho nacho ndani mwao, matumaini yao na hata kukata tamaa kwao. Hali hiyo katika maisha ya seminarini, ina maana ya kwamba kuwa na  nafasi ya kwanza ambayo ni mazungumzo na Bwana anayejifanya kusikiliza mwingine: Yeye ananisikiliza na mimi ninasikiliza Yeye, hakuna kujidanganya na kujiwekea pazia. Kusikiliza kwa moyo katika sala ni kuelimisha kuwa watu wenye uwezo wa kusikiliza wengine na kuwa kama Mungu anavyotaka mapadre  wanaotoa huduma ya kusikiliza, Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema: kwa jinsi gani kuna haja hiyo! na inatuelimisha daima kuwa Kanisa la kusikiliza na  jumuiya ambayo inatambua kusikiliza. Baba Mtakatifu anasema. Ninyi sasa mnaishi kwa namna ya pekee mkiwasiliana na vijana, mnamkutana nao, mnawasikiliza na kuwaalika wajieleze… Lakini hiyo ndiyo shughuli ya maisha yote ya kichungaji, ni kama Yesu, kama Kanisa linawatuma katika dunia ili kusikiliza kilio cha binadamu ambaye mara nyingi ni kilio cha ukimya, wakati mwingine kunyamazishwa na kusongwa.

Ufunguo wa neno la tatu ni kung’amua

Baba Mtakatifu akiendelea anasema:Kutembea; kusikiliza na neno la tatu ni kung’amua. Katika seminari ni mahali na kipindi cha mang’amuzi. Na hiyo inahitaji kusindikizwa kama Yesu alivyofanya kwa mitume wake, katika mitume wote kwa namna ya pekee Mitume kumi na mbili. Aliwasindikiza kwa uvumilivu, na hekima, aliwaelimisha kufuata ukweli na ili kutoa pazia za kuficha uongo wa ndani ya mioyo. Kwa kuheshimu na kwa maamuzi kama urafiki mwema, hata kama tabibu mwema ambaye wakati mwingine, lazima atumie zana za kuumiza.  Matatizo mengi yanayojitokeza katika maisha ya padre, Baba Mtakatifu anabainisha, yanatokana na ukosefu wa mang’amuzi mema katika miaka ya seminari. Si kwa wote na siyo mara nyingi, lakini ni wengi, Baba Mtakatifu amesisitiza! Ni kawaida hiyo hata katika maisha ya ndoa, mambo mengine ambayo hayakuweza kukukabiliwa kwanza, yanaweza kugeuka kuwa matatizo baadaye. Yesu hakujifanya akiwa na Mitume wa Emau, hakuwaingilia na wala kuzungukia matatizo. Aliweza kuwaita wapumbavu na kwamba wana mioyo mizito, kwa sababu hawakuamini manabii (Lk 24,25) . Na baadaye aliwafungulia mioyo yao juu ya Maandiko matakatifu mara baada ya kukaa mezani na uwepo wake mpya kwa ishara ya mkate uliomegeka. Baba Mtakatifu anaongeza Fumbo la wito na mang’amizu ni kazi nzuri ya Roho Mtakatifu ambayo inahitaji ushirikiano wa kijana aliyeitwa na mtu mzima anayemzindikiza.

Neno la nne ni utume

Neno la nne linalotambulika la uchaguzi wa utume na Sinodi ya vijana ilitoa thamani kubwa ya ukuu wa muungano wa utume wa kwenda pomoja kukutana  na wengine. Mitume wawili wa Emau walirudi pamoja Yerusalemu na hasa waliungana na jumuiya ya kitume ambayo kwa nguvu ya Roho ikawa yote ya kimisionari. Vishawishi vinavyoweza kujitokeza, Baba Mtakatifu anasema, msisitizo huo ni muhimu  kwa sababu ya vishawishi ambayo vinaweza kuonekana hasa ya kujiona na ubinafsi  katika utume wa kimisionari. Hilo ni jambo lisilokuwa jema Baba Mtakatifu anakazia. Na hili suala ambalo hata kwa waseminari linaweza kujitokeza mapema, au katika kuandaa matukio, au maadhimisho mazuri na mambo mengine. Baba Mtakatifu anabainisha kuwa mara nyingi mtindo wao wa kuishi umekuwa ni wa kibinafsi zaidi ya kuwa na upamoja, undugu.

Kutokana na saula hilo Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kuwa, ukuhani na uchungaji wa kijimbo ulikuwa unawakilisha labda kung’aa binafsi, lakini uliokuwa una ukosefu kidogo ushuhuda wa muungano na upamoja. Shukrani kwa Mungu sasa unaendelea kukua hali ya upamoja na muungano hasa kutokana na ukosefu wa makleri, Japokuwa Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, muungano hautendeki kwa kulazimishwa ni lazima kuamini  na kuwa mkarimu wa Roho Mtakatifu. Anahitimisha Baba Mtakatifu akiwakumbusha kwa mara nyingine tena ushuari wake aliowapatia kuhusiana na picha ya kiinjili ya mitume wa Emau, safari; kusikiliza; kung’amua; na kwenda pamoja. Anamwoma Bikira Maria awasindikize, na anawabariki na kusali kwa ajili yao, lakini pia wasisahau kusali kwa ajili yake.

 

 

 

24 November 2018, 14:35