Vatican News
Vatican Pope Angelus Vatican Pope Angelus  (ANSA)

Papa Francisko:Mungu na jirani ni sura mbili katika medali moja!

Mungu ambaye ni upendo, alituumba kwa upendo na ili sisi tuweze kupenda wengine na kubaki tumeungana naye. Itakuwa ni uongo kujidai unampenda jirani bila kumpenda Mungu na unampenda Mungu bila kumpenda jirani! Ni tafakari ya Papa, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 4 Novemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kitovu cha Injili ya Dominika hii ( Mk 12,28b-34), kuna amri ya upendo: upendo wa Mungu na upendo wa jirani. Mwandishi alimuuliza Yesu: “ni amri ipi kuu kuliko zote?”. Yeye alijibu kw akikiri imani ya kila mwisraeli aliyokuwa anafungua na kufuga siku yake ambayo inaanza na maneno ya “Sikiliza Israeli! Bwana Mungu wetu ni Mmoja (Kumb 6,4). Kwa namna hiyo Israeli inahifadhi amri yake kwa uhakika wa msingi wake wa kuamini ya kwamba yupo Bwana mmoja na Bwana huyo ni wetu kwa maana anajihusisha nasi katika agano lisilotengenishwa, alitupenda, anatupenda  na daima atatupenda.  Na katika msingi huo  wa upendo wa Mungu unaotokana na sisi kwa kupewa amri mbili; mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa akili yako na kwa nguvu zako zote(…), mpende jirani yako, kama nafsi yake ( Mk12,30-34). Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Neno la Mungu, ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili, tarehe 4 Novemba 2018, kwa waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Mungu na jirani ni sura moja katika medali

Baba Myakatifu Francisko akiendelea kufafanua Injili ya Siku anasema: Kwa kuchagua maneno mawili yaliyosemwa na Mungu kwa watu wake na kuyaweka pamoja, Yesu alifundisha mara moja na daima kwamba upendo kwa ajili ya Mungu na upendo kwa ajili ya jirani, ni vitu viwili visivyotengena na zaidi vinasaidiana mmoja na mwingine. Japokuwa vimeweka kila mmoja katika nafsi yake, lakini vina sura mbili katika medali moja kwa maana vikiishi kwa pamoja ndiyo nguvu ya kweli ya waamini! Kupenda Mungu ni kuishi naye na kwa ajili ya kile ambacho ni chake, na kile ambacho Yeye mwenyewe anafanya. Mungu wetu anajitoa kwetu bila kubakiza, anasamehe bila mpaka, anayo mahusiano yanayohamasisha na kufanya ukue. Kwa njia hiyo kupenda Mungu ina maana ya kuwa na mtaji ambao ni msingi wa nguvu zake ili uwe mhudumu wake katika hutoaji wa huduma bila kujibakiza kwa jirani na kutafuta kusamehe bila mpaka, kwa kuhamasisha kujenga uhusiano wa umoja na kindugu, amethibitisha Baba Mtakatifu.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko, amefafanua ya kwamba: mwinjili Marko, hana wasiwasi wa kutaka kufafanua ni nani jirani, kwa sababu jiarani ni mtu ambaye mimi ninakutana naye katika safari, katika siku zangu za kila siku. Na kwamba hiyo haina maana ya kuchagua jirani, kwa maana huo si mtindo wa ukristo au kwa kufikiria kuwa jirani yangu ni yule ninaye mchagua hapana!  Hiyo si tabia ya ukristo bali ni ya upagani; Kinachotakiwa ni kuwa na macho ya kumwona na kuwa na moyo wa kumtakia mema. Ni kukuwajibisha  kumwona kwa mtanzamo wa Yesu, kujikita katika kusimsikiliza daima na kuwa karibu na mwenye kuhitaji.

Mahitaji ya jirani yahitaji majibu ya dhati

Mahitaji ya jirani yanahitaji kwa hakika majibu ya dhati Baba Mtakatifu anathibitisha na kuongeza : lakini kabla ya yote wanahitaji ushirikishwaji. Kwa sura ya jirani tunaweza kusema mwenye njaa, anahitaji, si sahani ya supu, bali hata tabasamu, asikilizwe na hata kumwombea, labda inawezekana kusali kwa pamoja. Injili ya sikua Baba Mtakatifu anabainisha, inawaalika wote kuelekeza mtazamo si tu katika dharura ya ndugu ya masikini zaidi, bali hawali ya yote kuwa makini kwa ajili ya mahitaji ya lazima ambayo ni ukaribu kidugu kwa maana ya maisha na huruma.

Huo ndiyo wajibu wa jumuiya kwa maana, inahitaji kuhepuka hatari za kuwa jumuiya inayoishi kwa kuanzisha mambo mengi, lakini bila kuwa na mahusiano; kuna hatari ya jumuiya kuwa kituo cha huduma lakini bila kuwa wasindikizaji kwa maana kamili na ukristo amethibitisha Baba Mtrakatifu. Tuombe Mungu ambaye ni upendo , alituumba kwa upendo na ili sisi tuweze kupenda wengine na kubaki tumeungana naye. Itakuwa ni uongo wa kujidaidi kupenda jirani bila kumpenda Mungu; na vileviel ni kujidanganya bure kwa kujidai unampenda Mungu bila kumpenda jirani. Ukuu wa aina mbili wa upendo, kwa ajili ya Mungu na jiranni katuka umoja wake unayo tabia ya mfausi wa Kristo. Bikira Maria atusaidie kupokea na kushuhudia katika maisha ya kila siku mwanga wa mafundisho hayo.

 

05 November 2018, 10:48