Jubilei ya  lasalliano Jubilei ya lasalliano 

Papa Francisko kuridhia mwaka wa Jubilei wa Lasalliano

Katika Mwaka wa 300 tangu kifo cha Mtakatifu Giovanni Battista la Salle, Papa Francisko ameridhia ufunguzi wa Jubilei ya Lasalliano itakayo anza tarehe 17 Novemba 2017 na kumalizika tarehe 31 Desemba 2019 katika Madhabahu ya Roma, kwa maana Mtakatifu huyo ni msimamizi wa walimu katoliki

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kufuatia tukio la mwaka wa 300 tangu kifo cha Mtakatifu Yohane Battista la Salle,(1719-2019) Mwanzilishi wa ndugu wa Shule ya Wakristo, Papa Fancisko amekubali ufunguzi wa Jubilei ya  La Lasalliano. Mwaka wa jubilei unaanza tarehe 17 Novemba 2017 na utamalizika tarehe 31 Desemba 2019 katika Madhabahu ya Roma, kwa maana Mtakatifu huyo ni msimamizi wa walimu katoliki.

Asiye jua mtakatifu Giovanni Battista wa la Salle,

Kwa yule ambaye hajuhi mtakati huo, inawazekana ikawa fursa ya kugundua karama na shughuli zake. Kabla ya kifo chake, alitamka maneno haya: “ ninakuabudu kwa mapenzi yote ya Mungu ambayo yapo katika mtamzamo wangu. Na maneno haya  yanayokusanya shughuli za mtakatifu huyo, kwa maana ni sura muhimu katika historia ya mafundisho  na ambaye alikuwa ni mwahamasihaji wa elimu kwa watu wote duniani. Alitangazwa mtakatifu kunako mwaka 1900 na Papa Leone XIII, na kutangazwa Msimamizi wa walimu katoliki kunako mwaka 1950 na Papa Pio XII.

Mtambueni Yesu chini ya mavazi mabovu ya watoto wanaokuja shuleni kwenu

“Mtambueni Yesu chini ya mavazi yaliochanika ya watoto maskini ambao wanakuja shuleni kwenu”. Je  Imani yenu ina nguvu kiasi cha kutingisha moyo wa wanafunzi wenu na ili waweze kuvuta hewa ya kikristo. Ni muujiza mkubwa ambao unaweza kufafanua na ndiyo moja ya swali ambalo Mungu anawauliza kwa sababu hiyo ndiyo lengo la huduma yenu. Pia Mtakatifu Giovanni anasema, “ iwapo taasisi yetu ni kazi ya binadamu, inawezekana ukaanguka; lakini kama ni kazi ya Mungu, hakuna nguvu yoyote itaweza kuharibu”.

Mtindo wa kufundisha watoto

Katika njia ya kufundisha watoto, yeye aliamua kuondoa lugha ya kilatini   na kuanzisha lugha ya kifaransa. Wakati huo huo aliangaikia  kuunda walimu wengine hasa ilipofika mwaka 1680 alianzisha, Jumuiya ya ndugu wa Shule ya wakristo. Akiwa na ndugu hao walianza kufungua mashule mengine na baada ya miaka 8 waliitwa kufundisha mjini Paris na kwa mwaka mmoja tu wanafunzi wao waliongezeka zaidi ya maelfu.

Pamoja  na hayo changamoto hazikukosa, kwa maana walifikia hata ya kuchoma shule zao, na ndipo  Mtakatifu Giovan Battista La sale alilazimika na jumuiya yake kuhamia katika mji kadogo wa Saint- Yon ( huko Rouen ) ambapo alifia  huko tarehe 7 Aprili 1719.

06 November 2018, 15:55