Tafuta

Kardinali Pietro Parolin anamwakilisha Papa Francisko katika kilele cha Jubilei ya Miaka 130 ya Uinjilishaji nchini Mali, 2018 Kardinali Pietro Parolin anamwakilisha Papa Francisko katika kilele cha Jubilei ya Miaka 130 ya Uinjilishaji nchini Mali, 2018 

Jubilei ya Miaka 130 ya Uinjilishaji Mali! Haki na Amani!

Karne ya kumi na tisa ilipambwa na juhudi za pekee katika mchakato wa uinjilishaji Barani Afrika, ulioziwezesha jumuiya za Kikristo kukua kwa haraka, ingawa tayari kuna Jumuiya ya Bamako tayari inaadhimisha Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, kazi na utume uliofanywa kwa ari na moyo mkuu kutoka kwa Wamisionari wa Roho Mtakatifu kuanzia mwaka 1888.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameandamana na Padre Arvèdo Godima, Mmisionari wa Afrika pamoja na Padre Florent Konè, Gombera wa Seminari kuu “St. Augustin” huko Samaya, amemwakilisha Baba Mtakatifu Francisko katika kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 130  ya Uinjilishaji nchini Mali, maadhimisho ambayo yamefanyika kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Kita, kuanzia tarehe 17-18 Novemba 2018.

Baba Mtakatifu Francisko katika barua ya utambulisho kwa Kardinali Parolin anakaza kusema, karne ya kumi na tisa ilipambwa na juhudi za pekee katika mchakato wa uinjilishaji Barani Afrika, ulioziwezesha jumuiya za Kikristo kukua kwa haraka, ingawa tayari kuna Jumuiya ya Bamako tayari inaadhimisha Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, kazi na utume uliofanywa kwa ari na moyo mkuu kutoka kwa Wamisionari wa Roho Mtakatifu kuanzia mwaka 1888 kwa kuanza kujenga Parokia ya kwanza Kite na huo ukawa ni mwanzo wa kuenea kwa imani ya Kikristo nchini Mali.

Viongozi wa Kanisa nchini Mali wanasema, maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 130 ya Uinjilishaji nchini humo yalianza kwa habari mbaya ya vita na mipasuko ya kijamii, lakini kwa sasa anasema Baba Mtakatifu Francisko kwamba, Kardinali Parolin anaweza kumwakilisha ili kuwatangazia tena furaha ya Injili ya Kristo, fursa ya kukuza na kudumisha imani na urafiki na mafungamano ya kijamii nchini Mali. Baba Mtakatifu anapenda kuwahakikishia upendo wake wa dhati na uwepo wake kwa njia ya sala.

Katika barua yake, Baba Mtakatifu anamkumbuka na kumwombea pia Makardinali Charles Martial Lavigerie, aliyejitaabisha kulea na kuifunda mihimili ya uinjilishaji, miaka 150 iliyopita. Vijana na waamini wote wanapaswa kuendelea kuwa waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake na kwamba, Bikira Maria, Mama wa Kanisa aendelee kusaidia mchakato wa haki, amani na upatanisho, ili amani ya kudumu iweze kutawala tena Mali kwa kufumbatwa katika toba na wongofu wa ndani. Waamini wawe ni vyombo na mashuhuda wa imani inayomwilishwa katika matendo; waendelee kukuza na kudumisha Ibada kwa Bikira Maria; ili kutangaza na kushuhudia Injili ya upendo kwa watu wote. Baba Mtakatifu anakaza kusema, roho ya ufukara na mapendo ndio utukufu na ushuhuda wa Kanisa la Kristo!

Kardinali Parolin: Mali

 

 

17 November 2018, 14:50