Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini Morocco, Mwezi Machi 2019 Papa Francisko anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini Morocco, Mwezi Machi 2019  (©milosk50 - stock.adobe.com)

Papa Francisko kutembelea Morocco, Machi 2019

Mfalme Mohammed VI pamoja na Maaskofu Katoliki nchini Morocco, wamemwalika Baba Mtakatifu Francisko kutembelea nchi yao kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019. Katika hija hii ya kitume, Baba Mtakatifu anatarajiwa kutembelea mji wa Rabat na Casablanca.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko uliotolewa kwake na Mfalme Mohammed VI pamoja na Maaskofu Katoliki nchini Morocco, kutembelea nchi yao kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019. Katika hija hii ya kitume, Baba Mtakatifu anatarajiwa kutembelea mji wa Rabat na Casablanca. Ratiba elekezi ya hija hii ya kitume, inatarajiwa kutolewa hivi karibuni kwa mujibu wa Dr. Greg Burke, Msemaji mkuu wa Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anataka kuendeleza majadiliano ya kidini na waamini wa dini mbali mbali duniani, ili kujenga na kudumisha umoja, upendo, haki na mshikamano wa dhati na kwamba, tofauti mbali mbali zisiwe ni chanzo cha vurugu na mitafaruku ya kijamii na kidini.

Papa: Morocco
13 November 2018, 15:50