Tafuta

Papa Francisko amekutana na wakilishi wa wayahudi mjini Vatican Papa Francisko amekutana na wakilishi wa wayahudi mjini Vatican 

Papa Francisko: bila kumbukumbu hakuna wakati endelevu!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi Mkutano wa Kiyahudi kutoka Caucaso tarehe 5 Novemba mjini Vatican. Hawa ni wayahudi wanaoishi katika mlima wa Caucaso, wanaoitwa kwa jina Juhuro, katika eneo la Daghestan na kanda za kaskazini ya nchi ya Azerbaigian

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mara ya kwanza Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi  Mkutano wa Kiyahudi kutoka Caucaso tarehe 5 Novemba mjini Vatican. Hawa ni wahayahudi wanaoishi katika mlima wa Caucaso , kwa jina jingine wanaitwa Juhuro. Ni kikundi cha wayahudi wa Caucaso katika eneo la Daghestan na kanda za kaskazini ya nchi ya Azerbaigian.

Katika hotuba yake  Papa FRancisko amesimulia juu ya mkutano wake wa hivi karibuni nchini Lithuania tarehe 23 Septemba wakati wa kufanya maadhimisho ya  miaka 75 ytangu mauaji ya kimbari ya wayahudi na mara baada ya kuharibu kambi huko Vilinius  kwa mauaji ya maelfu na maefu ya kiyahudi. Kutokana na hilo, Papa amekumbusha juu ya umuhimu wa  kufanya kumbukumbu.

Kufanya kumbukumbu

Kufanya kukmbuku ya mauaji ya kimbari Papa anasema ni lazima kwa sababu ya wakati uliopita uweze kubaki kumbukumbu hai. Bila kukumbumbu hai hakutakuwapo na wakati endelevu kwani tusipojifunza kutoka katika kurasa za historia ya giza zaidi tunaweza kujikuta tunarudia makosa yale na pia hadhi ya binadamu itabaki maandishi yaliyokufa.

Kutetea uhuru wa dini

Matukio mengine ambayo yamekuwa  katika mawazo ya Papa Francisko, ni kuhusu miaka 75 tangu kufungwa kwa mtaa wa kiyahudi wa  Roma na tarehe 9 Novemba  itakuwa ni kumbukumbu ya  miaka 80 ya usiku wa  ule wa kuharibu maeneo mengi ya ibada za kiyahudi ambapo Papa amesisitiza juu ya kusitisha kila aina ya mzizi  ya ukatili uliyo ndani ya moyo wa binadamu  na katika watu ambao kwa dhati hahawezi kamwe kukiukwa hadi yao , kwa maana ya uwepo wa muumbaji. Kutokana na hilo  Baba Mtakatifu amesisitizia juu ya kuwa na haki sawa hasa ya uhuru wa dini;  pia juu ya kupinga vikali ubaguzi dhidi ya wayahudi na  wakati huo huo kuonesha urafiki uliopo kati ya wayahudi na wakatoliki.

Urafiki kati ya wayahudi na wakatoliki

Papa anasema: "kuzungumza na wengine na kusali kwa ajili ya wote, ndizo nyenzo ili mikuki iwe miundu ya kupogolea (Is 2,4) , na ili uwepo upendo palipo na chuki na msamaha palipo na ugomvi, hakuna kuchoka katika maombi na kukimbilia njia za amani kwa sababu leo hii, siyo wakati wa kutafuta ufumbuzi kwa njia ya ukatili na kwa ghafla, badala yake ni wakati wa dharura ya kufanya mchakato wa wagonjwa  katika kuelekea njia ya mapatano".

05 November 2018, 14:27