Vatican News
Balozi wa Bosnia na Erzegovina awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican. Balozi wa Bosnia na Erzegovina awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican.  (Vatican Media)

Papa Franciko apokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Josip Gelo

Balozi Josip Gelo alizaliwa tarehe 19 Machi 1966 ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Kunako mwaka 1993 alitunukiwa shahada ya uzamivu katika masuala ya kitaalimungu kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Kitaalimungu cha Zagabria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa, tarehe 16 Novemba 2018 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Josip Gelo, Balozi wa Bosnia na Erzegovina. Balozi Josip Gelo alizaliwa tarehe 19 Machi 1966 ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Kunako mwaka 1993 alitunukiwa shahada ya uzamivu katika masuala ya kitaalimungu kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Kitaalimungu cha Zagabria. Katika maisha yake, amewahi kuwa mwalimu wa shule za msingi, mwanajeshi na mshauri wa masuala shughuli za ulinzi na usalama wa ndani kati ya mwaka 2003 - 2005.

Lakini kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 2004 alikuwa ni Mkurugenzi wa habari na diaspora, manispaa ya Lvno, Bosnia na Erzegovina. Kati ya mwaka 2004- 2005 akateuliwa kuwa Rais wa Manispaa ya Livno, Bosnia na Erzegovina. Kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2016 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Wafranciskani huko Livno, Bosnia na Erzegovina. Kati ya mwaka 2016 - 2018 aliteuliwa kuwa Balozi wa Bosnia na Erzegovina nchini Italia, Malta, San Marino na mwakilishi wa kudumu wa nchi yake kwenye Makao makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO.

 

 

16 November 2018, 14:37