Tafuta

Vatican News
Papa Francisko akiwa na Rais wa Paraguay Bwana Mario Abdo Benitez Papa Francisko akiwa na Rais wa Paraguay Bwana Mario Abdo Benitez  (ANSA)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Paraguay

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Paraguay, Bwana Benítez mjini Vatican tarehe 5 Novemba 2018, ambapo mara baada ya mkutano wao, amekutana na Kardinali Parolin Katibu wa Vatican akiongozana na Askouf Mkuu Paulo Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mahusiano na nchi za nje

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 5 Oktoba 2018, katika Ukumbi wa Kitume mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Paraguay, Mheshimiwa Bwana Mario Abdo Benítez, ambapo mara baada ya mkutano wao, amekutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican akiongozana na Askouf Mkuu Paulo Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mahusiano ushirikiano na nchi za nje.

Katika mazungumzo yao, wameeleza juu ya kufurahishwa na uhusiano mzuri ulipo kati ya Vatican na nchi ya Paraguay pia wamesisitiza juu ya umuhimu wa thamani za kikristo katika historia hasa hali halisi ya nchi yao. Katika mantiki hiyo, pia walionesha maana kubwa ya shughuli za kichungaji za Kanisa mahalia katika kusaidia jamii ya Paraguay. Vile vile wametazama  hali halisi ya nchi hiyo kwa namna ya pekee kutazama uhamasishaji wa kijamii na msaada kwa upande wa familia, mapambano dhidi ya uamsikini, ufisadi na biashara haramu. Katika mazungumzo pia wameweza kukabiliana hata masuala yanayoitazama amani katika dhana ya kimataifa na kikanda.

 

 

 

06 November 2018, 09:36