Sala kwa ajili ya wakristo wanaoteseka  iliyoandaliwa mjini Venezia na Chama cha Kanisa hitaji Sala kwa ajili ya wakristo wanaoteseka iliyoandaliwa mjini Venezia na Chama cha Kanisa hitaji 

Papa Francesco:Haki ni msingi wa mwisho wa binadamu!

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Patriaki wa Venezia, kwa ajili ya tukio liitwalo 'Venezia in Rosso', yaani mji wa Venezia na rangi nyekundu, ambapo Papa anawashukuru walioanzisha na kuandaa tukio hilo la kuwakumbuka watu wote wanaoteseka kwa ajili ya kutetea imani yao na zaidi wakristo duniani kote. Tukio hilo linafanyika jioni tarehe 20 Novemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa Patriaki wa Venezia akiwatakia matashi mema na ili fursa ya tukio la Venezia in Rosso liwafanye wawe makini juu ya janga la wakristo wanaoteswa kwa ajili ya kutetea imani yao. Ni katika Ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican.

Kukumbuka milioni moja ya wakristo wanaotesaka kwa sababu ya imani yao

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya tukio liitwalo (Venezia in Rosso) yaani mji wa Venezia kuwashwa taa za rangi nyekundu, ni tukio lililoandaliwa na Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji, linalojikita katika shughuli ya utume wa  kuwakumbuka watu wote wanaoteseka duniani kwa namna ya pekee wakristo,  wakitetea imani yao, kwa ushirikiano na Upatriaki wa Venezia  ambapo jioni tarehe 20 Novemba 2018, katika mji wa Venezia watawakumbuka wakristo milioni moja leo hii wanaotesa duniani kote na kwa namna ya pekee ya Asia Bibi ambaye ni mama hasiye na hatia, ambaye tarehe 31 Oktoba Mahakam Kuu ya Pakistan iliweza kutoa suluhisho la yeye kutokuwa na hatia baada ya kufungwa gerezani kwa mika mingi. Kutokana na fursa ya kumbukumbu hii, katika mji wa maji huko Venezia na maeneo mengine, wataungana kwa kuwasha taa za rangi nyekundu, ishara ya kuwaombea mashahidi wa kutetea imani yao.

Baba Mtakatifu amewatumia salam vijana

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu, aliotuma kwa Patriaki wa Venezia, Askofu Mkuu Francisko Moraglia, ujumbe uliotiwa saini na katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, Baba Mtakatifu anatoa salam za upendo kwa vijana ambao watashiriki hija ya kijimbo na ambapo baadaye kuwashwa taa za rangi nyekundu Kanisa kuu la Mama Maria Afya ya wagonjwa, njia ya mfereji mkuu, daraja la Rialto na maeneo mengine mengi yenye ishara maalum ya mji wa Venezia uliozungukwa na maji.

Tukio la kuhamasisha maoni ya umma juu ya janga la mateso ya wakristo

Kadhalika katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anahamasisha maoni ya umma kuhusu janga la wakristo wengi wanaoteseka kwa sababu ya kutetea imani yao kwa maana anathibitisha kwamba, kuna baadhi ya nchi ambazo wanaruhusu dini moja tu, na mahali pengine, inaonesha jinsi ganiya  kuwatesa kwa nguvu zote au kudharau kwa mantiki ya utamaduni, mbele ya wafuasi wa Yesu. Na ndiyo maana kuna haja msingi ya kuanzisha matukio yanayofanana hayo ya Venezia na sehemu nyingine kama zinavyo andaliwa na Baraza la Kipapa la Kanisa hitaji kwa lengo la utambuzi zaidi.

Hata hivyo ikumbukuwe Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji limewahi kuandaa tukio la kuwasha hata kumbusho muhimu la Koloseo mjini  Roma, ili kuweza kutoa umakini katika dunia, juu ya ukiukwaji wa uhuru wa dini. Baba Mtakatifu anandika: “Haki ndiyo msingi wa mwisho wa binadamu, kwa maana hiyo lazima haki hzizo ziweze kutambuliwa kwa maana zinaangaza hadhi kuu zaidi ya ubinadamu. Anahitimisha Baba Mtakatifu Francisko, ujumbe huo wa tukio la kuwakumbuka milioni ya wakristo duniani wanaoteseka kwa ajili ya kutete imani yao.

20 November 2018, 15:17