Vatican News
Vifo vya wakopti nchini Misri vinaendelea kwa sababu ya kukiri imani yao Vifo vya wakopti nchini Misri vinaendelea kwa sababu ya kukiri imani yao 

Papa awaombea waathirika wa Kanisa la kikoptiki nchini Misri

Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake kufuatia shambulio la kigaidi lilitokea hivi karibuni kwa mahujaji wa wakoptiki wakati wanarudi kusali

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 4 Novemba 2018, Baba Mtakatifu ameonesha masikitiko yake kufuatia shambulio la kigaidi lilitokea hivi karibuni kwa waamini wa Kanisa la  Kikoptiki nchini Misri. Anasali kwa ajili ya waathirika na mahujaji waliouwawa kwa sababu wao ni wakristo. Baba Mtakatifu anamwomba Maria Mtakatifu awatulize wanafamilia na Jumuiya nzima.  Watu wote wameungana pamoja kusali sala ya Salam Maria…

Kuhusiana na tukio hilo

Taarifa kuhusiana na tukio hilo kutoka tovuti ya Kanisa la Kikoptiki nchini Misri linaandika kuwa waathirika  ni kikundi cha mahaujaji waliokuwa wanatoka hija katika Kanisa la Mtatifu Samuel Muungamishi katika eneo la Minya huko Misri ya kati. Na kikundi cha wanajihadi wenye silaha, waliweka kizingiti katika barabara na kufuatia risasa. Watu kadhaa wamekufa japokuwa bado idadi inaendelea kuongezeka kutokana na majeruhi wengi. Kadhalia mahujaji hao walikuwa hawana askari wa kuwasindikiza katika mabasi yao. Jumuiya ya wakoptiki ni sehemu ndogo karibia asilimia 10-15 % ya milioni 600,000 ya watu wa misri na ndiyo jumuiya kubwa ya kikristo katika nchi za Mashariki.

Ikimbukwe hata Mwezi Mei 2017, ilitokea shambulizi kama hilo dhidi ya Bus moja la waamini wa kikoptiki walio kuwa wakielekea katika Monasteri kusali. Katika tukio hilo walikufa watu zaid ya 30. Wanajihadi waliwalazimisha kushuka na kuwapiga risasi moja kwa moja. Kufuatia na shambulizi hilo inathibitishwa kuwa waumini wa Kanisa la Coptiki bado wanaendelea kulengwa na Waislamu wenye msimamo mkali. 

05 November 2018, 10:05