Papa anashukuru nchi ya Lebanon kwa makaribisho ya wakimbizi!
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Jumanne tarehe 20 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Chama cha Wamaronite kutoka nchini Lebanon ambapo amewashukuru sana Jumuiya ya Walebanon kwa sababu ya kuwa na uwezo wa kuwatunza na kuwa na msimamo kati ya wakristo na waislam na kwa ajili ya ukarimu wa kuwapokea zaidi ya milioni moja ya wakimbizi kutoka pande zote za nchi za Mashariki ambazo ziko katika moto wa vita.
Ametamka hayo katika hotuba yake bila maandishi, ambapo amezungumza na wajumbe hao katika ukumbi wa Clementina wakiwa ni Wanachama wa Wamaronite na viongozi wa nchi ya Lebanon,mara baada ya kuzungumza na na maaskofu 35 ambao ni wa Kanisa la Upatriaki wa Antiokia ya Wamaronite, wanaojikita katika utoaji wa huduma ya kichungaji katika Jumuiya ya Lebanon, lakini hata wakihudumia waamini wengine wengi kutoka diaspora mbalimbali.
Waamini na maskofu na ndiyo wanatoa utambuzi bora wa jumuiya
Mara baada ya salam kutoka kwa Kardinali Bechara Boutros Rai, patriaki wa Antiokia ya Kimaronite, Baba Mtakatifu Francisko amewalekea zaidi ya walei 50 wa Chama hicho kwa kusisitizia kwamba ni wazo zuri la kusindikizwa na maaskofu, kwa maana hiyo inawezekana kujua kwa undani zaidi jumuiy hiyo. Hata hivyo kama kawaida yake ya vichekesho hakukosa kwatania akiongeza kusema:“na hivi waamini wanaweza kuchambua maaskofu!” Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Nimeambiwa kwamba nitakutana na watu karibia arobaini kuwasalimia, lakini sasa nimeona ongezeko zaidi la watu kutoka Lebanon!” “Asante kwa ujio wenu na kwa wingi wenu!”
Asante kwa sababu ya msiamamo kati ya wakristo na waislam
Akiendelea na shukrani, amewashukuru jumuiya ya Walebanon kwa ajili ya kile wanachofanya nchini humo. “Kwa ajili ya kutunza na kuwa na msimamo, na kwamba msimamo huo wa kiubunifu ni wa nguvu kama mpanzi, kati ya Wakristo na Waislam na Wasuuni na Washiite; ni msimamo ambao ni wa kizalendo na kindugu” amesisitiza. Aidha “kwa ajili ya ukarimu na moyo wa mapokezi ya wakimbizi ambapo amethibithisha kuwa ni zaidi ya milioni moja. Asante sana!”. Na mwisho Baba Mtakatifu Francisko anamwomba Bwana ili awabariki wote, faimilia zao nchi zao , watoto wao na wakimbizi wao.