Tafuta

Vatican News
Papa Francisko na Kiongozi Mkuu Mar Gewargis III Catholicos-Patriaki wa Kanisa la Assira Mashariki wakati wa saini ya pamoja Papa Francisko na Kiongozi Mkuu Mar Gewargis III Catholicos-Patriaki wa Kanisa la Assira Mashariki wakati wa saini ya pamoja  (Vatican Media)

Papa amekutana na Patriaki wa Kanisa na Assira

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kiongozi mkuu, Mar Gewargis III, Catholicos-Patriaki wa Kanisa la Assira ambapo wametia saini ya Waraka wa Pamoja na kusali kwa ajili ya watu wanaoteseka hasa Iraq na Siria. Katika hotuba yake anashukuru Mungu zawadi ya Tume ya mazungumzo ya kitaalimungu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na Kiongozi Mkuu Mar Gewargis III, Patriaki Catholicos wa Kanisa la Assira ya Mashariki, tarehe 9 Novemba 2018 mjini Vatican. Baada ya Mkutano wao wa faragha, Baba Mtakatifu  Francisko na Catholicos Patriaki Mar Gewargis III wamesali kwa pamoja katika Kanisa la Redemptoris Mater kwenye Jumba la Kitume. Na mwisho wametia saini katika Waraka wa Pamoja. Ifutayo ni hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoitoa mbele ya Patriarki, Mar Gewargis III  wakati wa Mkutano wao na Waraka wa Pamoja na kabla ya kwenda kusali pamoja.

Kuwakumbuka watu wa nchi za Mashariki wanaoteseka na vurugu

Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo (Ef 6,23). Kwa kutumia maneno ya Mtume Paulo, ninawasalimu ninyi na kwa njia yenu, wajumbe wa Sinodi ya Maaskofu, Makleri na waamini wote wa Kanisa la Assira ya Mashariki. Imepita miaka miwili tangu kukutana kwa mara ya kwanza, lakini kwa  wakati huo, nimepata furaha ya kukutana nawe kwa wa upya,  tarehe 7 Julai huko Bari  wakati wa fursa ya Siku ya kutafakari na kusali  kwa ajili ya amani ya nchi za Mashariki ambapo pia ushiriki kuomba. Tunashirikishana kwa dhati mateso makubwa ambayo yanatokana na janga la hali halis ambayo ndugu kaka na dada wa Mashariki wanaishi, waathirika wa nguvu na mara nyingi kulazimika kuacha ardhi yao mahali walikuwa wakiishi daima.

Wanapitia njia kama msalaba kama ile ya  Kristo

Baba Mtakatifu anaendelea: Hawa wanapitia njia ya msalaba kama ile ya Yesu japokuwa wanatoka katika jumuiya tofauti  na kati yao  kujenga mahusiano ya kindugu na  kugeuka  kwa kwetu mashuhuda wa umoja. Na ili kuweza kusitisha uchungu mkubwa, tutaweza kusali pamoja na kuomba Bwana zawadi ya amani katika nchi za mashariki na zaidi kwa ajili ya Iraq na Siria.

Baba Mtakatifu anashukuru Mungu zawadi ya Tume ya mazungumzo ya kitaalimungu

Baba Mtakatifu katika hotuba yake: “Kwa namna ya pekee ya kutoa  shukrani kwa Mungu ni kwa ajili ya   Tume tuliyo nayo kwa pamoja kwa ajili ya mazungumzo ya kitaalimungu kati ya Kanisa katoliki na Kanisa la Assira ya mashariki. Kwa dhati, mwaka mmoja uliopita Baba Mtakatifu anaongeza, nilipata furaha ya kuwapokea Wajumbe wake, katika fursa ya kutia saini Waraka wa Pamoja juu ya “maisha ya Sakramenti”. Katika Tume hiyo, ambayo ni tunda la mazungumzo, inaonesha kuwa utofauti wa matendo na maadili, daima siyo kizingiti cha umoja na kwamba baadhi ya tofauti  zinazoj ieleza za  kitaalimungu, zinaweza kufikiriwa kwamba, zinakamilishana badala ya kuleta migogoro”. Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu anasema: “Ninasali ili kazi ambayo inapelekwa mbele, na ambayo katika siku hizi inaingia katika hatua ya tatu ya mafunzo juu ya Kanisa, itusaidie kuendelea na mchakato kwa mara nyingine tena kwenye hatua nyingine ya njia kulekea upeo unaosubiriwa na ambao tunaweza kuadhimisha Sadaka ya Bwana katika altare moja.

Safari hiyo unayosukuma kwenda mbele inahitaji mlinzi

Baba Mtakatifu akielezea mchakato wa safari anasema: Safari hiyo inatusukuma kwenda mbele, lakini inahitaji mlinzi daima aliye hai katika kumbukumbu, kwa ajili ya kuacha tupumue kupitia mashahidi wa wakati uliopita. Kwa dhati mwaka huu Kanisa la Assira ya Mashariki kama pia, Kanisa wa Wakaldayo, wanaadhimisha Mwaka wa 700 tangu kifo cha Abdisho bar Berika, Mkuu wa  Nisibi, mmoja wa waandishi maarufu wa utamaduni wa Siro ya Mashariki. “Kazi zake kwa namna ya pekee katika nyanja ya haki za sheria, hadi sasa ni maandishi msingi katika Kanisa lenu”.

Ninayo furaha kwa ushiriki wako, kama pia hata wajumbe wawakilishi katika Mkutano wa Kimataifa uliondaliwa kwa ajili ya fursa hii na Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki. Na ili mafunzo hayo katika taalimungu kubwa iweze kusaidia kutambua vema utajiri wa tamaduni za Sira na kuupokea kama zawadi kwa ajili ya Kanisa zima. Akihitimisha Papa anasema: Ndugu mpendwa, kwa upendo ninatoa shukrani kubwa kwa ajili ya ziara yenu na kwa ajili ya zawadi ya kusali pamoja leo hii, kwa ajili ya mmoja na mwingine. Kwa  kutumia sala ya Bwana  naili iwe ya kwetu: “ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja (…) na  ili ulimwengu upate kusadiki” (Yh 17, 21).

 

09 November 2018, 14:48