Baba Mtakatifu Francisko, ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Varona kuanzia 22-25 Novemba 2018 Baba Mtakatifu Francisko, ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Varona kuanzia 22-25 Novemba 2018 

Katika mtazamo wa huruma,kila mtu anaweza kudhubutu uhuru!

Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa washiriki wa Toleo la Nane la Tamasha ya Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona Italia, kuanzia tarehe 22-25 Novemba 2018. Kitovu cha ujumbe wake ni mada ya uhuru ambapo anathibitisha kuwa, ni lazima uwe kwa watu wote na kwa ajili ya wema wa pamoja

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya Video kwa washiriki wa Tamasha la Nane la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona nchini Italia yaliyozinduliwa tarehe 22 -25 Novemba 2018, kwa kuongozwa na kauli mbiu “ hatari za uhuru”.  Akiendelea na ufafanuzi anasema: Hatari za uhuru ndizo zinazosaidia daima kujiweka katika safari ya wanaume na wanawake, jamii na ustaarabu. Ni zawadi kubwa ya Mungu kwa ajili ya kiumbe chake hata kama wakati mwingine, kiumbe hicho kinapotea njia na kusababisha vita, ukosefu wa haki, ukiukwaji wa haki msingi na ukosefu haki za binadamu.  Kwa maana hiyo, anawatakia washiriki wote, matashi mema ya Toleo la Nane la Tamasha ya  Mafundisho jamii ya Kanisa  na ili kwamba lazima kudhubutu kwa ajili ya wengine.

Ni lazima kujaribu na kujihatarisha kwa ajili ya wengine

Kama wakristo, waamini wa Injili na wenye utambuzi wa uwajibikaji tulio nao kwa ajili ya ndugu wote, tunaalikwa kuwa makini na kukesha kwa sababu ya hatari za uhuru, ili isipoteze maana yake yake ya juu zaidi na wajibu. Kudhubutu kwa ajili ya wengine, kwa dhati ni kujiweka katika majaribu. Na ndiyo wito wetu wa kwanza. Wote tunatakiwa kujikita kwa dhati kuthubutu ili kuweza kuondoa kila aina ya kile kinachozuia hupatikanaji wa tunu ya uhuru kwa wanaume na wanawake. Na wakati huo huo, ni kutafuta namna ya kuonja uhuru huo na kutunza nyumba yetu ya pamoja ambayo Mungu alituzawadia

Hali ya kwanza ni Utamaduni wa ubaguzi

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea katika ujumbe wake kwa njia ya video anaelezea hali tatu zinazozuia wanaume na wanwake kutozaa matunda ya uhuru wao na kutoweza kuthubutu: Hali ya kwanza ni ile hali ya kukosa kujikita katika kutafuta haki; hali ambayo inazidi kupenyeza mizizi yake katika dunia nzima hata katika miji yetu anabainisha! Katika utamaduni wa ubaguzi wa kijamii, watu wako hatari ya kuishia pembezoni na siyo katika uzoefu wa maisha yao na matunda mabaya ya uhuru wa mwingine, bali hata kunyimwa ule uwezekano wa kuweza kuwa na uhuru wao, familia zao, maisha yao mema, haki na hadhi yao.

Hali ya pili ni hatari za teknolojia

Utawala wa teknolojia usipoweza kusindikizwa  kwa namna ya maendeleo na yenye kufaa na uwajibikaji wa thamani na utambuzi, matokeo yake ni hasi katika uzoefu wa uhuru, kama alivyo kuwa amekumbusha tayari Papa Paulo VI, kuhusu binadamu, kwamba anapoteza maana ya mpaka na matokeo yake ni kutotazama changamoto za wakati, na zaidi tulizo nazo mbele yetu. Kwa maana hiyo kukomaza kwa mbinu za kiufundi, unaweza kuumiza watu,Baba Mtakatifu amesisitiza.

Hali ya binadamu kutumia hovyo

Hali ya tatu na mbaya inaonyeshwa katika  kupunguzwa kwa mtu katika hali ya matumizi. Katika kesi hii, uhuru huko hatarini na bado unabaki kuwa udanganyifu tu. Baba Mtakatifu anasisitiza . “Kama nilivyokwisha eleza katika Waraka wa kitume wa Laudato si, kwa mujibu wa mantiki hiyo kwamba, walio na uhuru ni wale wenye  uwezo wa kutumia, wakati  wenye  kuwa huru ni sehemu ndogo ambao wao wana nguvu za kiuchumi na fedha.  Huo siyo uhuru, anathibitisha Baba Mtakatifu badala yake ni utumwa na uzoefu wa kila siku ambao unajikita katika ukosefu wa imani, hofu na kujifungia binafsi.

Matashi mema ya kudhubutu

Akiendelea ametoa mfano kwamba: “na hata hivyo, kama itakumbukwa na ushuhuda wa watu walikombolewa dhidi ya amana na ukahaba, kamwe  pasiwep na mtu yoyote wa kukata tamaa ya kuwa na shauku ya kuthubutu kwa ajili ya uhuru kamili” Hata kama wengine wana hofu ya kwenda kinyume, lakini wapo wengi katika maisha yao ya kila siku wanaishi mtindo wa maisha mema, yenye msimamo, yaliyo wazi na wanakaribisha”.

Dunia inahitaji watu walio huru!

Uhuru huo siyo ndoto kamwe, bali unajenga katika maisha ya kile ambacho unashauku nacho, japokuwa wengi hawana ujasiri wa kufuata. Kwa hakika kuwa uhuru ni changamoto na changamoto ya kudumu, inavutia, inashinda, inatoa ujasiri, inafanya watu kuwa na ndoto, inajenga tumaini, inadhamiria mema na inaamini wakati ujao. Kwa maana hiyo ina nguvu ambayo ni nguvu kuliko utumwa wowote. Dunia inahitaji watu huru!

Msiwe na hofu ya kutenda yaliyo mema

Anahitimisha Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki wote ya kwamba akiwatakiwa matashi mema ya kuwa na uhuru na wasiwe na hofu ya kujitoa na kuchafua mikono yao kwa ajili ya kutumiza wema na kusaidia wale wenye kuhitaji. Anawakumbusha kwamba: uhuru wa binadamu unamfunua mwenyewe hadi mwisho hasa anapojigundua kuwa amezaliwa na kupendwa kwa uhuru wote na Baba muumba ambaye anajionesha uso wake kwa njia ya Mwanae katika sura ya huruma. Katika mtazamo wa huruma, kila mtu daima anaweza kutembea na kudhubutu ule uhuru!

23 November 2018, 12:26