Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Novemba 2018 Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Novemba 2018 

Katekesi ya Papa:Mlango wa shetani upo katika mifuko!

Wakati wa tafakari ya katekesi ya Papa Francisko, katika mwendelezo wa Amri za Mungu, tarehe 7 Novemba, amefafanua Amri ya, “Usiibe”. Katika kuifafanua vema, amejikita kutazama mafundisho jamii ya Kanisa na Katekisimu ya Kanisa Katoliki (n. 2402 -2403), mahali ambapo wanazungumzia juu ya upeo wa mali zote katika dunia hii

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wapendwa kaka na dada, habari za asubuhi! “kwa kuendelea kuendelea Amri za Mungu, leo tumefika Neno la Saba “Usiibe”. Katika kusikiliza amri hii tunafikia mada ya wizi, suala linalohusu mali ya wengine. Hakuna utamaduni ambao wizi na unyanyasaji wa mali ni halali. Kwa dhati, katika unyeti wa binadamu huathirika sana na ulinzi wa milki. Lakini ni vyema kujifungulia katika uelewa mpana wa Neno hili, kwa kuzingatia suala la mada ya umiliki wa mali kwa njia ya  mwanga wa  hekima ya kikristo. 

Katika Mafundisho jamii ya Kanisa wanazungumiza juu ya upeo mali zote mahali zitakapokuwa. Tunasema kwa upeo wa vitu vyote na hebu tusikilize Katekisimu ya Kanisa  katoliki inasemaje:  “Mwanzoni Mungu aliimanisha dunia na rasilimali zake kwa usimammizi wa jumla wa manadamu kuzitunza, kuzitawala kwa kazi na kufurahia matunda yake (n. 2402), hadi hapo ni katekesimu ya Kanisa Katoliki. Lakini bado sehemu nyingine inaendelea ya  katekisimu kuelezea kuwa: “ Lengo la mali kwa ajili ya wote hubaki la kwanza na hata kama kuendeleza mali ya wote kwahitaji heshima kwa ajili ya haki ya mtu kumiliki mali na kuitumia”(n. 2403. Baraka hata hivyo hazikujipanga mfululizo katika dunia,  kwa maana kuna tofauti, hali tofauti, tamaduni tofauti, hivyo unaweza kushi kwa kumsaidia kutoa kwa mmoja na mwingine.

Dunia ni tajiri kwa rasilimali

Ni mwanzo wa tafakari ya Katekesi ya baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 7 Novemba 2018 kwa mahujaji na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua anasema: Dunia ni utajiri kwa rasilimali ili kuhakikisha wote  kuwa na mali  zote msingi. Pamoja na hayo wengi wanaishi katika umasikini na kutia kashfa na rasilimali, zinanatumiwa bila vigezo, na zinaharibika. Licha ya hayo,  dunia ni moja tu! ubinadamu ni moja tu Baba Mtakatifu amesisitiza! Baba Mtakatifu Francisko amesema, “Leo hii utajiri wa dunia uko mikononi mwa wali wachache, wakati huo walio wengi zaidi ni  masikini au tuseme, taabu na  mateso ni kwa walio wengi”. Iwapo katika ardhi hii, kuna njaa, si kwamba inasababishwa na ukosefu wa chakula! Na  cha zaidi Baba Mtakatifu anafafanua,  kwa sababu ya mahitaji ya masoko, inafikia hata hatua kwa wakati mwingine kuharibiwa na kutupa. Kile kinachosekana ni kuhusu mpangilio wa muda mrefu kwa wajasiriliamali ambao wangeweza kuhakikisha uzalishaji wa kutosha na kuweka mbinu za mshikamano katika kuhakikisha usambazaji wenye haki.

Binadamu katika matumizi yake ya mali na mantiki ya amri ya usiibe 

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kutazama katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasema tena: “binadamu katika matumizi yake ya vitu, anapaswa kutambua kuwa mali anazozimiliki kihalali hazipo kwa ajili yake tu bali pia kwa ajili ya wengine, kwa maana ni mwenye jukumu la kuzifanya zizalishe na kushiriki faida zake na wengine, kwanza ya wote familia yake” (n. 2404) kutokana na hilo, Baba Mtakatifu anaongeza ili “utajiri uweze kuwa mwema ni lazima uwe na ukuu kijamii”. Mara baada ya kufafanua zaidi, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba katika mantiki hiyo ya umiliki ndipo inajitokeza maana chanya na kubwa ya amri ya “ Usiibe.

Umilikaji wa mali wamfanya anayezimiliki kuwa msimamizi wa mapaji ya Mungu.  Na kuongeza kusema Baba Mtakatifu: “Hakuna ambaye ni bwana kabisa wa mali kwa maana, yeye ni msimamizi wa mali”. Kumiliki ni kuwajibika. Unaweza kusema kuwa: “lakini mimi ni tajiri wa kila kitu”… ndiyo, Baba Mtakatifu anaongeza: “lakini huo ni uwajibikaji ulio nao, na kila mali itokanayo na mantiki ya Mungu, Mtoaji imeasalitiwa; imesalitiwa katika maana yake ya kina”.  Kile ninachomiliki kwa dhati ni kile ambacho ninatoa. Hiki ni kipimo cha kutathmini jinsi gani ninavyoweza kuwa na utajiri, ikiwa ninafanikiwa vizuri au vibaya; neno hili ni muhimu” amehimizia Papa: “kile ambacho ninacho mimi mwenyewe ni kile ninachoweza kutoa”. “Ikiwa ninaweza kutoa, mimi niko wazi, mimi ni tajiri, si tu kwa kile nilicho  nacho bali  pia kwa ukarimu: na ukarimu pia ni wajibu wa kutoa, kwa sababu kila mtu aweze kushiriki”.

Utumwa wa kile ulicho nacho

Baba Mtakatifu Francisko anasema: “Kwa hakika iwapo siwezi kutoa chochote, ni kwa sababu mimi ni mtumwa kwa kile nilicho nacho. Kitu hicho kina uwezo juu yangu na ndiyo maana mimi ni mtumwa”. Lakini umiliki wa mali ni fursa ya kuzizidisha kwa ubunifu na kutumia kwa ukarimu na hivyo kukua katika upendo na uhuru. Kristo mwenyewe, licha ya kuwa kwaasili alikuwa Mungu, lakini: “hakufikiri kuwa sawa na Mungu, lakini  kwa hiari yake alijitoa mwenyewe” (Fil 2,6-7)  na kututajirisha kwa umasikini wake (taz 2 Kor 8,9). Wakati ubinadamu unahangaika kupata zaidi, Mungu ujishusha na huokoa kwa kujifanya maskini: Mtu yule Msulibiwa amelipa kwa ajili ya wote kwafidia isiyohesabika kwa  upande wa Mungu Baba,mwingi wa huruma”  (Ef 2,4 na Yk 5,11).

Mlango wa shetani upo katika mifuko

Akihitimisha tafakari ya katekesi yake kuhusu amri ya saba “ Usiibe, Baba Mtakatifu anasema: Kile kinachofanya kuwa tajiri siyo mali bali ni upendo Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza kusema, “mara nyingi tumesikia yale ambayo watu wa Mungu uwaambiwa: “Shetani huingia katika mifuko yake”.  Kwanza fedha hufika, upendo wa fedha, njaa ya kumiliki; na baadaye ubatili: Baba Mtakatifu ametoa mfano: “Ah, mimi ni tajiri na ninajivunia hiyo”; na mwisho, kiburi na majivuno. Hii ndiyo njia yashetani anayoitumia kutenda ndani mwetu. Lakini mlango wa kuingilia upo katika mifuko. Kwa njia hiyo: “kaka na dada , kwa mara nyingine tena, Yesu Kristo anatufunulia maana kamili ya Maandiko.“Usiibe” maana yake ni upende na mali zako, fursa za mali zako ziwe ni kwa ajili ya  kupenda kama unavyoweza. Na kwa njia hiy basi maisha yako yanakuwa mazuri na milki inakuwa zawadi ya kweli. Kwa sababu maisha siyo wakati wa kumiliki walakini kupenda!

07 November 2018, 15:03