Tafuta

Vatican News
 Baba Mtakatifu akisali katika masalia ya Mtakatifu Nicola wa Bari Baba Mtakatifu akisali katika masalia ya Mtakatifu Nicola wa Bari  (Vatican Media)

Barua ya Papa kwa ajili ya miaka 50 ya kutabaruku Kanisa!

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Askofu Mkuu Francesco Cacucci wa Jimbo Kuu Katoliki la Bari – Bitonto na Mwakilisho wa Kipapa wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicola kufuatia na maadhimisho ya miaka 50 tangu kutabarikiwa na kuwa Kanisa Kuu la Kipapa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Askofu Mkuu  Francesco Cacucci wa Jimbo Kuu Katoliki la Bari – Bitonto na Mwakilisho wa Kipapa wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicola kufuatia na maadhimisho ya miaka 50 tangu kutabarikiwa Kuwa Kanisa  Kuu la Kipapa la  Mtakatifu Nocola wa Bari.

Kanisa hilo lilipewa heshima kuwa Kanisa la Kipapa na Mtakatifu Paulo VI

Katika ujumbe wake anasema imepita miaka 50 tangu mtakangulizi wake Mtakatifu Paulo Vi alipoiteuwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicola wa Bari, kuwa Kanisa la Kipapa na kupewa Ofisi ya Mwakilishi wa Kipapa, Askofu Mkuu wa Bari. Umuhimu wa siku hiyo anasema, ni sababu ya furaha kwa ajili ya Jimbo Kuu, kwa ajil ya mji na mkoa wa Puglia, kwa ajili ya Shirika la Wahubiri ambao wanatunza hekalu Takatifu, kama pia ukatoliki mzima wa maneo hayo ya imani, sala , mikutano na mazungumzo kwa ajili ya kukuza mchakato wa kiekumene. Katika miaka hii, anaendelea kueleza, Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicola ambalo kwa namna ya pekee limeungana na Vatican, limetambua kuonesha kwa namna ya pekee wito ambao unajikita katika mchakato wa safari ya umoja wa wakristo. Yote hayo yamewezekana kuwa rahisi kutokana na uwazi wa ibada ya Mtakatifu, Askfo wa Myra na waamini wa Mashariki na Magharibi. Kutokana na hilo, mawazo ya Baba Mtakatifu yanawaendea wotae ambao kwa namna moja au nyingine wanashirikishana katika shughuli za kiliturujia, kichungaji, kiutamaduni, hasa zadi  kiekumene na  mahali ambao matunda yameweza kuonekana machoni pake, hivi karibuni alipotembelea mahali hapo katika fursa ya Mkutano wa maombi na tafakari kwa viongozi wote wa Makanisa, wakiwepo pia wa kutoka nchi za Mashariki.

Baba Mtakatifu anawatia moyo wote ambao wanashirikiana katika wajibu mbalimbali wa kichungaji katika historia ya Kanisa

Baba Mtakatifu anawatia moyo wote ambao wanashikiriana katika wajibu mbalimbali wa kichungaj katika historia hiyo na ambayo inaendelea katika Kanisa kuu huduma ya roho ya ushirikiano na kupyaisha shuhghuli za kitume, kwa kusaidia mahujaji na watu ambao wanafika hapo na kutazama kwa imani na kugundua umuhimu wa kiroho. Hiyo ni pamoja na kukuza kwa waamini ile mchakato ya safari ya kumtafuta Mungu ambayo inajikita kwa kina katika matendo ya toba na kutafuta mahali pazuri pa sala isiyoshibisha na tafakari. Baba Mtakatifu ameongeza kusema, maombi yana nguvu maalum za uinjilishaji na muhimu kwa ajili ya kuufikia ule ukamilifu wa muungano kati ya wakristo. Kadhalika, Baba Mtakatifu anawatakia mema katika kuadhimisha  siku hiyo ya kutimiza miaka hamsini  ili iweze kuwa sababu ya kupyaisha ule utashi wa pamoja katika kujifunza kwa pamoja historia za Kanisa Kuu la Kipapa, sura ya Mtakatifu Nicola na kama pia hata juu ya Taalimungu ya kiekuemene. Tafakari ya kisayanisa ikisindikizwa na mipango ya maonesho ya kiutamaduni, inaweza kuwa karibu na toba katika liturujia na sala kwa Mtakatifu, na ili kuweza kuchangia kidumisha mahusiano ya kiekumene kati ya jumuiya katoliki na kiorthodox.

Baraka ya Baba Mtakatifu

Katika hisia hizi, Baba Mtakatifu Francisko anawaombea kwa Mama  Bikira Maria na Mtakatifu Nicola, na kwa moyo wote, anawabariki kwa  Baraka ya kitume, Askofu Mkuu na Jumuiya nzima ya Jimbo, pia Kardinali Angelo Beciu anaye mwakilisha katika kuadhimisha Misa Takatifu  ya kumbukumbu, Mapadre Wadomenikani, wahamasishaji, watoa mada katika Mkutano na wote ambao wanashiriki maadhimisho hayo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

24 November 2018, 14:05