Tafuta

Vatican News
Maji ni msingi wa Maisha. Ni aibu watu kufa kwa sababu ya ukosefu wa maji safi ya kunywa Maji ni msingi wa Maisha. Ni aibu watu kufa kwa sababu ya ukosefu wa maji safi ya kunywa 

Baba Mtakatifu anasema ni aibu watu kufa sababu ya maji machafu

Kwa bahati mbaya, katika nchi nyingi ambazo watu wake hawawezi kupata maji safi ya kunywa, havikosi viwanda vinavyotengeneza silaha na risasi zinazoendelea kuzorotesha hali hiyo. Kiu inahitaji utashi, msimamo na juhudi kwa taasisi zote, mashirika, wataalam, teknolojia na bila kukosekana fedha,hayo ni kwa mujibu wa Papa Francisko

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 8 Novemba saa tatu asubuhi majira ya Ulaya, umefanyika Mkutano wa kimataifa ulioongozwa na mada: “uendeshaji wa wema wa pamoja:”hupatikanaji maji ya kunywa kwa wote”. Ni Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ufaransa, Italia, Monako na Marekani uliopo Vatican. Kati ya watoa mada ni Kardinali PeterTurkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, Monsinyo  Bruno-Marie Duffé  Katibu wa Baraza hilo  na  Askofu Silvano Maria Tomasi, mjumbe wa Baraza hilo kwa upande wa uhamasishaji.  Kufuatia na fursa hiyo ya mkutano wa kimataifa, Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake akiwapongeza kuhusu uandaaji wa Mkutano huo kwa uendeshaji wa wema wa pamoja: hupatikanaji wa maji ya kunywa kwa wote.

Maji ni msingi wa Maisha

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake, anabainisha kuwa: maji ni msingi wa maisha. Lakini katika maeneo mengi duniani, kaka na dada zetu hawawezi kupata maisha yenye hadhi hasa kutokana na ukosefu wa maji safi. Katika takwimu inayoonesha janga la kiu,  hasa katika hali ya watu ambao wanaugua na mara nyingi wanakufa kwa sababu ya maji machafu, ndiyo inabaki  kuwa aibu kwa ajili ya binadamu wa karne ya XXI. Kwa bahati mbaya, katika nchi nyingi ambazo watu wake hawawezi kupata kwa kawaida maji safi, ndiyo mahali ambapo hapakosekani viwanda vya kutengeneza silaha na risasi zinazoendelea kuzorotesha hali hiyo! Ufisadi na faida binafsi za uchumi ambazo zinabagua na kuua ndizo zinaongezea mara nyingi dhidi ya juhudi ambazo kwa namna ya mshikamano ndiyo zingeweza kusaidia ule uwezekano wa kupata maji. Pamoja na hayo pia  Papa Francisko anaongeza kusema: Takwimu zinazoonesha  kiu, zinahitaji utashi, msimamo na juhudi kwa taasisi zote, mashirika, wataalam, teknolojia,na fedha ambazo haziwezi kukosekana.

Akikumbusha Waraka wa Laudato Si

Baba Mtakatifu anakumbusha jinsi gani, katika suala hili amekwisha pendekeza maoni yake, katika Waraka wa Laudato Si’ na hivi karibuni katika fursa ya Siku ya Kuombea huduma ya viumbe. Kwa maana hiyo ni matshi ya Baba Mtakatifu  Francisko kwamba wale wote watakaoshiriki katika Mkutano huo wanaweza kushirikishana katika mantiki zao za kitaaluma na kisiasa juu ya dharura, utashi na msimamo ambao ni wa lazima! Anaongeza: “Vatican na Kanisa, wanajikita katika jitihada za kukuza hupatikanaji wa maji safi ya kunywa kwa wote. Juhudi hizo inajionesha katika kuanzisha mambo  mengi yakiwema majengo na mafunzo ili kusaidia watu wenye hatari, na mahali ambapo hupatikanaji wa maji unakuwa ni shida na kati ya hao ametaja kuwa ni wahamiaji, na hivyo anatoa wito wa pamoja kuhusu maadili na misingi ambayo inatokana na Injili  na ile inayohusu elimu safi ya binadamu.

Elimu ya binadamu inayofaa

Baba Mtakatifu amesema: “Elimu ya watu inayofaa kwa dhati ni muhimu kwa ajili ya mtindo wa maishi ya kuishi na mshakamano kwa ajili ya ekolojia ya kweli ( taz Laudato Si’ 118;122) zaidi katika utambuzi wa kupata maji kama haki ambayo inatokana na hadhi ya binadamu, kwa maana hiyo,  mantiki ya maji inafanana kama ile ya  kila aina yoyote ya bidhaa. Misingi na thamani ya kiinjiili  ni lazima viende sambamba  katika juhudi za dhati kwa kila mmoja, ili kuweza kufukia ule wema wa pamoja katika familia ya binadamu (Evangelii gaudium, 179-183). Kwa mtazamo mwingine, imani na kila binadamu mwenye kiu, wanahisi kuwa sura sawa ya Mungu, kama tunavyosoma katika Injili ya Matayo: “Nilikuwa na kiu, hamkuninywesha” ( mt 25, 42). Kadhalika anasema katika mkutano huo kwa bahati nzuri unawaunganisha watu wa imani na tamaduni tofauti;ni sehemu mbili ya tasaufi na  kwa maana hiyo utamaduni wa maji hauwezi kudharauliwa kutokana na kwamba ni kiini cha kiungo jamii, cha kuishi na mpangilio kijumuiya.

Maji ni muhimu sana, manyenyekevu, ya thamani na safi (Mtakatifu Francis wa Asisi)

Akihitimisha ujumbe wake, Baba Mtakatifu anawaalika kutafakari juu ya ishara ya maisha katika misingi ya utadumani wa kidini; vilevile anawasihi watafakari juu ya rasilimali hiyo ambayo Mtakatifu Fracis wa Asisi alisemani “multo utile et humile et preziosa et casta”) Yaani ni “muhimu sana, manyenyekevu ya thamani na safi”. Ameombea Baraka ya Munu Muumba  kwa kila mmoja na katika familia zao, juu ya shughuli zote zilizoanzishwa katika kuborehsa uendeshaji wa maji na kuwatakia kazi njema bila kusahua wasali pia kwa ajili yake.

08 November 2018, 14:51