Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anauliza swali, je Kanisa lingekuaje bila kuwa na watawa wa ndani? Papa Francisko anauliza swali, je Kanisa lingekuaje bila kuwa na watawa wa ndani?  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu amekumbuka Siku ya Pro Orantibus!

Watu hawa wasikose msaada,hata wa vitu kwa upande wa Kanisa zima. Ni wito wa Papa Francisko alioutoa mara baada ya katekesi yake tarehe 21 Novemba katika uwanja wa Mtakatifu Petro akikumbuka siku ya 65 ya Pro Orantibus,yaani Siku ya watawa wa ndani. Maisha ya Kanisa na dunia yangekuwaje bila kuwa na walinzi wa kutangaza asubuhi wakati bado kuna giza?

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo ni kumbuku ya Siku kuu ya B. Maria kutolewa Hekaluni na tunaadhimisha Siku ya pro Orantibus yaani Watawa wa ndani, ikitolewa kuwakumbuka jumuiya zote watawa wa ndani. Ni watawa wengi! Ni fursa na mwafaka kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi ya watu wengi ambao katika monasteri mbalimbali wanajikita kwa dhati kwa Mungu katika sala, ukimya na katika kujificha. Watu hawa wasikose ukaribu na msaada hata wa vitu kwa upande wa Kanisa zima. Huo ni wito wa Baba Mtakatatifu Francisko alioutoa mara baada ya tafakari ya katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote mjini Vatican akikumbusha juu ya Mama Kanisa kuadhimisho Siku Kuu ya Bikira Maria kutolewa Hekaluni, siku inayokwenda sambamba na kuwakumbuka watawa wote wa ndani.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu katika siku ya Pro Orantibus

Baba Mtakatifu  Francisko, ametuma ujumbe wake katika Mkutano uliondaliwa na Mashirika ya Kitawa (CIVCSVA)  katika fursa ya Siku Kuu  ya pro Orantibus, yaani (Watawa wa ndani) ambayo inawakumbuka jumuiya zote za watawa wanaoishi ndani na kuomba. Mkutano huo umefanyika tarehe 21 Novemba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano. Baba Mtakatifu anasema katika liturujia ya Siku kuu ya Bikira Maria kutolewa Hekaluni, inaadhimishwa leo hii mwaka wa 65 wa Siku ya Pro  Orantibus. 

Siku hii kwa mwaka huu inaadhimishwa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano na katika Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Yohane Laterano, ambapo inajikita katika kuwakilisha Katiba mbili zinazotazama moja kwa moja maisha ya watawa wa ndani, Katiba ya kitume ya “Vultum Dei Quaerere” yaani “Kuutafuta Uso wa Mungu”na “Cor Orans” yaani  Hati Elekezi ya Utekelezaji wake.

Katika fursa hiyo, Baba Mtakatifu amesema ninayo furaha kuwasalimia washiriki wote wa siku hiyo. Na kwa wote anawasalimia watawa wa kike na kiume wanaomfuata Kristo katika maisha ya utawa wa ndani kwa kutafuta uso wa Mungu na kushirikiana katika  utume wa Kanisa kutokana na kwamba ndiyo moyo wa sala.

Asante kwa ajili ya kujibu wito na kuudhuria mkutano huo na maadhimisho  na wakati huo huo Rais wa Baraza la Watawa na mashiririka ya kitume na Katibu wake, pamoka na  Sekretarieti  ya Pro Manialibus , ambayo kwa uangalifu mkubwa wanaandaa siku hiyo na kuihusika na watawa kwa namna pekee wa Kituo cha Mafungo na kuwasaidia Monasteri zenye kuwa na matatizo.

Ingekuwaje Kanisa bila kuwa na walinzi ambao wanatangaza siku mpya wakati bado ni usiku?

Baba Mtakatifu anaendelea katika ujumbe wake kuwa: Nichukue fursa ya siku hii kwa mara nyingine kutoa pongeza kwa niaba ya  Kanisa kwa ajili ya mtindo wa maisha yenu. Je maisha ya Kanisa yangekuwaje bila kuwa na watawa wa ndani? Ingekuwaje maisha ya watu wadhaifu wa Kanisa ambao wanapata msaada kwenu ili waweze kuendelea katika safari yao? Maisha ya Kanisa na ya dunia yangekuwaje bila kuwa na taa zinazoonesha mwambao kwa yule aliyepotea katika bahari kuu, bila kuwa na moto unaongaza usiku wa giza ambalo tunalipitia, bila kuwa na walinzi ambao wanatangaza siku mpya wakati bado ni usiku?

Baba Mtakatifu anatoa shukrani zake

Asante dada na kaka wa ndani kwa sababu ninyi ni kila kitu kwa ajili ya dunia: msaada wa wadhaifu, taa, mshumaa na walinzi (taz Cost. ap. Vultum Dei quaerere, I, 6). Asante kwa sababu mnatutajirisha na matunda mengi ya utakatifu, ya huruma na neema (taz ibid., I, 5). Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa: “Pamoja na Kanisa, hata mimi ninasali ili Bwana aweza kutimiza ndani ya mioyo yenu kazi yake na kuwageuza kwa dhati kuwa wake hadi mwisho wa maisha ya ndani; na jumuiya zenu au za kindugu ziwe kweli shule ya maombi  na sala. Ulimwengu na Kanisa unahitaji msaada wenu (…) Na huo ndiyo uwe unabiii wenu”(ibid., I, 36).

Changamoto na mafunzo ya kudumu ni msingi

Katika fursa hiyo, Baba Mtakatifu anawaalika kuwa makini juu ya changamoto za mafunzo ambao kama jinsi wanavyo tambua yahusu mchakato wa mwendelezo wa hisia za Kristo kwa  Baba ( taz Mtakatifu Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Maisha ya watawa, 65). Kwa maana hiyo ili kudumu katika mafunzo kwa maisha yote, inahitaji hata kukubali uwajibikaji kwamba mafunzo ni mchakato unaokwenda taratibu na ambao ni muhimu bila kuwa na haraka. Katika mantiki hiyo, Baba Mtakatifu anakumbusha hata umuhimu wa mang’amuzi na kusindikizwa kiroho na wito wa makandidate, bila kuwa na zile  hurka ya kuaka kuwa na  idadi kubwa na ya kutosha, bali kuwa na  mafunzo kwa ajili ya walimu na dada ambao wanaitwa kujikita katika huduma ya uongozi.

Ili maisha ya sala yaweza  kuwa na maana kwa ajili ya Kanisa na ulimwengu wa leo ni lazima kutazama juu ya mafunzo yanayostahili, dharura ya wakati uliopo, yaani mafunzo fungamani, yenye lengo na kuendandana kwa dhati na hali halisi. Mafunzo ya namna hiyo yatarutubisha na kulinda maisha yenu ya uaminifu katika ubunifu wa karama mliyopokea iwe kwa kila mtawa na kwa ajili ya jumuiya nzima. Akihitimisha, Baba Mtakatifu amesema siku hii iliyo wawezesha nao kukaa kindugu, iwaangazie mwana na maisha ya jumuiya: Bikira Maria mfano wa sala ya ndani awafundishe kutafuta daima sura ya Mungu na kubaki waaminifu katika utume wao wa kuwa na moyo wa sala wa Kanisa.

 

21 November 2018, 15:00