Tafuta

Inawezekana duniani kufikia mwisho wa njaa na kufikia usalama wa vyakula kwa kila mtu Inawezekana duniani kufikia mwisho wa njaa na kufikia usalama wa vyakula kwa kila mtu 

Vatican:kushinda kipeo cha njaa kwa njia ya haki na kushirikisha

Askofu Mkuu Richard Paul Gallagher, Katibu wa mahusiano na ushirikiano na nchi za nje Vatican, katika Mkutano juu ya mada ya kupunguza njaa, uliofanyika tarehe 28 Septemba katika Chuo Kikuu cha Fordham mjini New York Marekani, ameonesha jitihada za Kanisa ili kuhakikisha haki ya chakula

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Uwajibikaji wa pamoja, mshikamano wa pamoja ndiyo maneno ya ufunguo uliolekezwa na Papa Francisko kwa ajili ya kuondaoa kipeo cha njaa duniani. Ni maneno ya Askofu Mkuu Paulo Richard Gallagher, Katibu wa wamahusiano na ushirikiano na nchi za nje Vatican, katika Mkutano juu ya mada ya kupunguza njaa, uliofanyika tarehe 28 Septemba katika Chuo Kikuu cha Fordham mjini New York Marekani.

Mwisho wa njaa na kufikia usalama wa vyakula, ndiyo lengo muhimu la umoja wa Mataifa ili kufikia  ajenda ya mwaka 2030, ya maendele endelevu.  Kuhusiana na suala hilo, kumekuwapo na mjadala uloandaliwa mjini New Yor Marekani na Siasa za Uchumi Kimataifa na maendeleo (Iped), pamoja na Chama cha Centesimus Annus Pro Pontifice Vatican. Mada ya mkutano huo ilikuwa ni “mwisho wa njaa: wito wa Papa Francisko kwa ajili ya matarajio mema”.

Ni maelekezo ambayo yamewekwa hivi karibuni na Kanisa ili kuhakikisha haki ya chakula kwa ajili ya wote, na ambayo ni safari iliyo mbali kabisa kufikia lengo, kwa mujibu wa hotuba ya Askofu Mkuu Richard Gallaghe, na kwamba licha ya kuwa na maandeleo makubwa ya kiteknolojia lakini bado ipo kazi kubwa ya kufanya.

Jitihada za Kanisa ili kuhakikisha haki ya chakula

Kuanzia katika mwaliko wa Kiinjili: “Nilikuwa na njaa mkanipatia chakula”, Kanisa daima limekuwa likitetea haki ya chakula, Askofu Mkuu Gallagher amebainisha na kuonegeza kusisitiza  kama vile Papa Mstaafu Benedikto XVI alivyosema katika ujumbe wake wa Siku ya Vyakula duniani mwaka 2007, iwe katika upande binafsi na hata ile ya kijumuiya ambayo inajumuisha watu wote na makundi ya kibinadamu.

Baada ya mika10, katika hotuba ya Papa Francisko kwenye  ofisi za FAO katika tukio kama hilo, alisisitiza juu ya kipeo cha njaa, kinavyoikumba leo hii watu milioni 821, na ambacho kinatokana na madaliko ya tabianchi, vyanzo vya maji salama, usimamizi  wa fedha kuhusu wahamiaji, biashara na utamaduni wa ubaguzi. Katika changamoto ya mwisho, Askofu Gallagher amebainisha kuwa inajumuisha hata  nyingine mbili za hatari zinazotazama moja kwa moja njaa na utapiamlo, kwa maana ya kusema ipo hali ya kutumia hovyo chakula, wakati wengine wanakufa kwa njaa.

Kutumia hovyo vyakula

Mbele ya ongezeko la ukosefu wa vyakula, Papa Francisko wakati anatoa hotuba yake katika Jumuiya ya kimataifa, alisema, ni lazima matunda ya ardhi yawekwe kwa pamoja na hupatikanaji kwa wote. Kwa mtu itakuwa inatosha kupunguza idadi ya kinywa ili kulisha na kutatua tatizo; lakini ni suluhisho linaweza kuwa la  uongo, kama unafikiria kwa ngazi ya kiwango cha mifumo kutumia zaidi na matumizi ya chakula ambayo hupoteza rasilimali nyingi. N alibainisha kwamba, kupunguza ni rahisi, lakini kushirikishana badala yake inahitaji uongofu, na hii ndiyo changamoto na wajibu unaotakiwa alisisitiza.

Papa Francisko na misingi ya kibanadamu

Pia papa alikuwa amenena, “ppendo unamaanisha kuchangia ili kila nchi ikaongeza uzalishaji na kufikia chakula cha kutosha. Upendo hutafsiriwa juu ya mwelekeo mpya wa maendeleo na matumizi,na kupitisha sera ambazo hatoai tofauti ya hali ya watu walio chini au utegemezi wao wa nje. Kuwapenda maana yake si kuendelea kugawanya familia ya wanadamu kati ya wale ambao wanavyo vya kutosha na wale ambao hawana vya kukidhi mahitaji”. “Njia ya Papa Francisko aliyokuwa anataka  kupunguza njaa haitokani  na hisia rahisi au uelewa usio wazi”, Askofu Mkuu Gallagher anasema: “Badala yake ni suala la haki, si ombi la dharura, au wito wa dharura kwasababu inaonesha ufumbuzi bora, katika hali ya kimataifa inayoongozwa na uwajibikaji wa pamoja, mshikamano na umoja”.

02 October 2018, 12:49