Tafuta

Watu wanaomboleza kuondokewa na ndugu zao kuokana na  ajali mbaya ya treni nchini India Watu wanaomboleza kuondokewa na ndugu zao kuokana na ajali mbaya ya treni nchini India 

Telegram ya Papa kwa ajili ya waathirika wa ajali ya Treni,India

Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko makubwa kutokana na ajali ya treni iliyotokea Ijumaa tarehe 19 Oktoba 2018 katika eneo la Amritsar, nchini India na kusababisha vifo karibia ya watu 60 na majeruhi wengi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwa jina la Baba Mtakatifu Francisko  ametuma salam za rambirambi kwa njia ya Telegram kupitia kwa viongozi wa Kanisa Kwa ajili ya raia na viongozi wa serikali mahalia kufuatia na wathirika wa ajali ya treni iliyotokea huko Amritsar, katika serikali ya Punjab nchini India.

Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko makubwa kutokana na  ajali ya treni iliyotokea Ijumaa tarehe 19 Oktoba 2018 katika eneo la Amritsar, nchini India na kusababisha vifo karibia ya watu 60 na majeruhi wengi. Katika ujumbe huo, uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, Papa anaonesha mshikamano wa dhati kwa wote ambao wamepatwa na mkasa huo na kuwahakikishia sala zake kwa wote walioaga dunia , wanaolia kwa ajili ya wapendwa wao. Anawapa baraka zake ili majeruhi waweze kupona, kuwa na nguvu na amani na marehemu wapumzike kwa amani.

Ajali ya treni ilitokea wakati watu mahali wakifanya sherehe ya dini na wahindi. Watu wengi walikuwa karibu na reli wakitazama michezo ya itifaki , wakati treni mbili zilikutana na kugongana  katika njia moja na kuwakanyaga watu. Viongozi wa India wamefungua kesi kwa uchunguzi wa janga hilo la Reli.

Katika ujumbe wa Maaskofu mahali, wamesema kushutushwa na  tukio hili na kwamba ndugu kaka na dada ambao wamekutana na mauti wakiwa vijana walikuwa wakisheherekea sikukuu ya dini. Mungu awajalie pumziko la milele. Kadhalika katika ujumbe wao wanahitimisha wakisema kwa mara nyingine tena, kuna ulazima wa kuboresha usalama wa reli na  barabara na uwepo wa kanni moja ya ulinzi wa kutosha wakati wa sherehe mbalimbali , kwa maana maisha ni tunu msingi na lazima kuilinda kwa kila hali.

22 October 2018, 15:35