Misa ya Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu Katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican Misa ya Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu Katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican 

Papa:Yesu anawapa wafuasi wake uhakika wa Roho Mtakatifu

Katika Misa ya Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu tarehe 3 Oktoba, Papa amesema, Roho Mtakatifu atakuwa wa kwanza kulinda na kutunza daima uhai na kumbukumbu ya sasa ya Mwalimu katika moyo wa mitume. Ni yeye ambaye anafanya utajiri na uzuri wa Injili iwe kisima cha furaha na mapya kwa dhati

Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia, Yohana 14,26). Kwa namna hiyo rahisi, Yesu anatoa uhakika kwa wafuasi wale wa kuwasindikiza katika maisha shughuli za kimisionari ambazo watakuwa wamekabidhiwa: Roho Mtakatifu atakuwa wa kwanza kulinda na kutunza daima uhai na kumbukumbu ya sasa ya Mwalimu katika moyo wa mitume. Ni yeye ambaye anafanya utajiri na uzuri wa Injili iwe kisima cha furaha na mapya ya dhati.

Moto na shauku ya kiinjili

 Ni mwazo wa mahubiri ya Baba Mtakatituf Francisko wakati wa kuadhimisha Misa ya Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana, tarehe 3 Oktoba 2018, katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu anaendelea katika mahubiri yake kisema: “Mwanzo wa kipindi hiki cha neema kwa ajili ya Kanisa, kinachoendana sawa na  Neno la Mungu, tuombe bila kuchoka Mfariji  atusaidie kufanya kumbukumbu na kutoa uhai wa maneno ya Bwana, yaliyokuwa yakiwachoma moyo  (rej Lk 24,32). Moto na upendo wa kiinjili ambao unatoa shauku na upendo wa ajili ya Yesu. Kumbukumbu ambayo inaweza kuamsha na kupyaisha ndani mwetu uwezo wa kuota ndoto na kutumainia. Kwa maana tunatambua kuwa, vijana wetu watakuwa na uwezo wa kina na maono kutokana na kipimo ambacho sisi watu wazima na wazee, tutakuwa na uwezo wa kuota ndoto na kuwaambukiza, na kushirikishana ndoto na matumaini ambayo tunayo ndani mwetu (Gl, 31).

Watu wazima washirikishane na vijana ndoto za matumaini

Roho Mtakatifu atupatie neema ya kuwa Mababa wa Sinodi walio na upako wa ndoto na matumaini, ili tuweze, kwa mara nyingine, kuutoa upako huo kwa vijana kama zawadi ya kinabii na maono; atupatie neema ya kuwa na kumbukumbu inayofanya kazi, hai na changamfu, ambayo inazaa katika kizazi, na wala haikandamizi unabii kwa njaa na matukio ua vikwazo vyetu, makosa na dhambi, lakini yenye uwezo wa kutafuta jisni ya kuwasha moto na kung’amua njia za Roho Mtakatifu.

Kwa mara ya kwanza maaskofu wawili wa china kuudhuria Sinodi

Ni katika mwenendo huo wa upole katika kusikiliza sauti ya Roho  ambayo imetufanya kuja kutoka pande zote za dunia. Leo hii kwa mara ya kwanza hapa tunao hata ndugu zetu maaskofu kutoka China. Tuwakaribishe kwa furaha: Katika Baraza zima la maaskofu na Kharifa wa mtume Petro, bado  inaonekana  neema kwa uwepo wao.

Kuungana kwa matumaini katika mkutano 

Baba Mtakatifu ameendelea kusema, “kuungana  katika matumaini, tunaaza mkutano mpya wa Kanisa wenye  wa kupanua upeo, katika moyo na kubadili mifumo ya ujenzi ambayo leo hii inatulemaza, inatutenganisha na kutuweka mbali na vijana, kwa kuwaacha wakiwa wanajiuliza maswali na yatima katika jumuiya ya imani ambayo inawasaidia, katika mwelekeo wa maana na maisha ( rej Esort. ap. Evangelii gaudium, 49).

Matumaini yatutafakarisha, yatatusukuma na kuvunja mitindo ya desturi: “tumezoea kufanya hivi”, na kututaka kuamka kutazama moja kwa moja uso wa vijana na hali ambazo wanaishi. Matumaini yenyewe, yatualika kufanya kazi kwa ajili ya kupindua mambo ya kitambo, ubaguzi na vurugu, ambazo zinawakabili vijana.

Vijana ni tunda la maamuzi

Vijana ambao ni tunda la maamuzi mengi yaliyochukuliwa wakati uliopita, wanatualika kubeba mzigo pamoja nao, wakati uliopo na kwa shughuli kubwa ili kupambana dhidi ya kila aina inayozuia maisha yao kuendelea kuwa na hadhi. Wanatuomba kuwa nao katika ubunifu, ambao ni mwenendo wa kiakili, na shauku iliyo jaa matumaini na ambayo haiwaachi katika mikono ya wafanya biashara wa kifo  na ambao wanawasonga maisha yao na kuwa na kivuli cha maono yao.

Uwezo huo wa kuota ndoto kwa pamoja, ambao Bwana anatuzawadia leo hii kama Kanisa, Baba Mtakatifu anaendelea kuthibitisha, ni kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo alivyo sema katika Barua yake kwamba ili kuendeleza kati yetu tabia ya dhati lazima, “ Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine (Fil 2,4). Na wakati huo huo inataka kutazama juu zaidi,  kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake (Fil 2,3). Katika roho hiyo, tutafute kujikita katika usikivu kwa wengine ili kung’amua pamoja kile ambacho Bwana anaomba kwa Kanisa.

Upendo tuliotumwa kwa watu lazima upanue upeo

Na hii inahitaji sisi kuwa makini hasa katika suala la mantiki ya kujitegemea na kuwa kumbukumbu binafsi ambayo inaweza  kuishia hata  katika  kukifanya muhimu kile ambacho ni cha pili, badala ya kuwa muhimu kile kinacho hesabika. Upendo wa Injili na kwa watu tuliotumwa sisi unatutaka tuupanue kwa upeo  wetu, na si kupotea mbele ya ziara ya kutume, mahali ambapo anatuita kuwa na lengo kubwa kwa ajili ya manufaa ya wengi zaidi. Bila mtazamo huo, jitihada zetu zote zitakuwa bure. Baba Mtakatifu amesisitiza.

Kumsikiliza Mungu ili kusikiliza naye kilio cha watu

Zawadi ya kusikiliza kwa uaminifu, kuomba na haraka iwezekanavyo bila hukumu na masharti itatuwezesha kuingia katika muungano na hali tofauti ambazo watu wa Mungu wanaishi. Kumsikiliza Mungu, ili kusikiliza pamoja naye kilio cha watu; kusikiliza watu, inaweza kutufanya  kupumua kwa mapenzi ambayo Mungu anatuita (Hotuba yake mkesha wa sala ya Sinodi juu ya familia Oktoba 2014). Mtazamo huu unatulinda dhidi ya majaribu ya kuangukia katika nafasi za kimaadili au madaraka, pia kutokana na kivutio cha mawazo yasiyo ya kawaida na ambayo hayaendani na  hayajawahi kuwa ya ukweli kwa watu wetu (rej J.M. BERGOGLIO, Meditaciones para religiosos, 45-46).  Baba Mtakatifu amesema: “Ndugu, hebu tuweke wakati huu chini ya ulinzi wa mzazi  Bikira Maria.  Yeye ni mwanamke wa kusikiliza na kuwa na kumbukumbu, atuongoze nasi ili kutambua athari za Roho na ili kuwa na uangalifu (taz Lk 1,39), kati ya ndoto na matumaini, tuwasindikize na kuwasaidia vijana ili wasiache unabii.

Kwa Mababa wa Sinodi

Baba Mtakatifu akiwageukia mababa wa sinodi amesema: "wengi wetu tulikuwa vijana au tulikuwa tunaanza hatua za maisha ya dini, wakati wa kumalizika Mtaguso wa Vatican II. Vijana wa wakati ule walipewa ujumbe wa mwisho kutoka kwa Mababa wa Mtaguso. Kwa maana ya kile ambacho tumesikia kutoka kwa vijana kitakuwa ni chema kupitia kwa upya katika moyo na ili kukumbuka maneno ya mshairi: "Mtu atunze kile alichoahidi akiwa mtoto” (F.HÖLDERLIN). 

Mababa wa mtaguso walisema 

Baba Mtakatifu ameendelea kueleza juu ya ujumbe wa Papa Paulo VI: “Kanisa kwa miaka 4 imefanya kazi kwa ajili ya kupyaisha uso wake, na ili uweze kuendana na ishara za mwanzilishi wake, aliye mkuu na hai, Kristo kijana milele. Katika hitimisho kubwa la kurudia kutazama kwa upya maisha, linawaelekeza ninyi vijana, hasa katika Mtaguso uliowashwa mwanga ambao unaangazia wakati endelevu wa maisha yenu. Kanisa linatamani kuwa na jamii ambayo mnajikita kujenga heshima ya hadhi, uhuru na haki ya mtu;  na watu wenyewe ndiyo ninyi (…) na imani, (…)  na kwamba  ninyi mtaweza kuwa na msimamo wa imani katika maisha na kile ambacho kinatoa maana ya maisha na uhakika wa uwepo wa Mungu mwema na wa haki.

Kwa jina la huyo Mungu na la Mwanae Yesu, ambapo sisi tunawashauri kufungua mioyo yenu kwa mujibu wa ukuu wa dunia na kuwa na subira ya wito kwa ndugu, katika kijikita kwa  nguvu zenu na chachu ya ujana katika kutoa  huduma kwao. Pambaneni dhidi ya ubinafsi, kataeni kutoa uhuru katika mchakato wa hisia za vurugu na chuki, ambazo husababisha vita na msafara wa uchungu na mateso. Muwe wakarimu, wasafi, wenye heshima na wawazi. Jengeni kwa shauku kubwa ulimwengu ulio bora zaidi ya sasa (Rej ujumbe wa Papa Paulo VI wakati wa kumaliza Mtaguso Vatican II, 8 Desemba 1965).

03 October 2018, 10:47