Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anawatuma vijana wawe ni vyombo na mashuhuda wa amani nchini Madagascar. Papa Francisko anawatuma vijana wawe ni vyombo na mashuhuda wa amani nchini Madagascar.  (Vatican Media)

Papa Francisko anawatuma vijana wa Madagascar kuwa wajumbe wa amani

Kuanzia tarehe 8 hadi 14 Oktoba huko Mahajanga, nchini Madagascar, familia ya Mungu inaadhimisha Siku ya Vijana Kitaifa inayoongozwa na kauli mbiu Usiongope Maria, maana umepata neema kutoka kwa Mungu”. Huu ni sehemu ya mchakato wa maisha na utume wa Kanisa kwa vijana ambao kwa wakati huu wanasindikwa na tafakari kuhusu Bikira Maria, Mama wa Mungu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumapili tarehe 14 Oktoba 2018 mara baada ya maadhimisho Ekaristi Takatifu ya kutangazwa kwa watakatifu wapya wa Kanisa, Papa Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video, kwa vijana wa madagascar waliounganika huko Mahanjanga kuanzia tarehe 8 hadi 14 Oktoba wakiadhimisha Siku ya viojana Kitaifa. Akianza ujumbe wake amesema:  “Ninayo furaha kubwa kuzungumza moja kwa moja na ninyi. Ninyi mpo ndani ya moyo wangu kama jinsi ilivyo kwa mababa wa Sinodi, kwa sababu umakini wetu ni kwa ajili yenu ninyi vijana. Ninyi mmekuja kutoka pande zote za kisiwa kizuri kwenye mkutano juu ya mada :“Usiogope Maria, maana umepata neema kutoka kwa Mungu”.

Usiogope Maria maana umepata neema kutoka kwa Mungu

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video anasema: “Neno hilo kwa Maria, kutoka kwa Malaika ni kwa ajili ya wote, kwa ajili yenu ninyi nyote. Mungu anawaelekeza ninyi. Kama Bwana alivyomtazama Maria na anakampatia zawadi ya neema yake, anawatazama hata ninyi kwa upendo, heshima na ukarimu. Yeye anajua hofu yenu na udhaifu wenu. Kwa njia yake kila kitu kinawezekana. Maria aliweka kila kitu katika Mikono yake: na hivyo fanyeni kama Yeye na kuipokea zawadi hiyo ya Mungu katika kufungua wazi mioyo yenu vema. Na neema ya Mungu na ni tunu ambayo siyo rahisi kuisahau, Baba Mtakatifu amebainisha.

Yesu anatoa maana ya maisha yenu yote

Akiendelea kufafanua zaidi katika ujumbe wake kwa njia ya video anasema: “Hiyo ni kwa sababu Bwana kamwe halazimishi: Yeye daima atwambia: Kama unataka… kama unataka… na hivyo Papa anaongeze kuwashauri vijana: “ chukueni muda kwa ajili ya kusikiliza mwaliko wake na kujibu kwa moyo wenu wote na kuwa ukarimu wenu!  Ni kwa jinsi gani ya kuwa na  furaha katika kujibu mwaliko wa Yesu!  Na hivyo kama ilivyo kwa mapadre wengi, na watawa wengi wanaweza kushuhudia.  Yesu anatoa maana ya maisha yenu yote”.

Msibaki wapweke bali Kanisa ni familia kubwa

Papa Francisko amewapa ushauri vijana wa Madagascar kuwa: “Msibaki pekee yenu”, Kanisa ni familia kubwa na ndani yake mtapata daima msaada na nguvu: katika maparokia yenu na katika makundi yenu, kwa njia ya sala, sakramenti, urafiki, kusindikizwa na mapadre na watu wengine wabatizwa”. Enendeni na kutangaza kwa wote kuwa, Bwana anawapenda, pia  pamoja naye kila hofu yoyote hutoweka: Timizeni ndoto zenu na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kujenga wakati wanu endelevu  na ule wa nchi yenu, kwa kutafuta daima wema wa mmoja na wengine”.

Wawe wajumbe wa amani

Papa Francisko akihitimisha katika kutoa ujumbe wake kwa njia ya video anasema: “Ninawatuma kama wajumbe wa amani na matumaini katika miji yenu, katika vijiji vyenu  mahali mnapoishi na kufanya kazi”. “Mungu awabariki na kubariki familia zenu!Ninawaombao na ninyi naomba msali kwa ajili yangu na kwa ajili ya maaskofu wenu wote”.

 

 

14 October 2018, 11:56