Tafuta

Vatican News
Mkutano wa vijana na Mababa wa Sinodi mjini Vatican, tarehe 6 Oktoba 2018 Mkutano wa vijana na Mababa wa Sinodi mjini Vatican, tarehe 6 Oktoba 2018  (Vatican Media )

Papa katika sikukuu ya vijana:Sikilizeni wazee na kukaribisha!

Umakini wa maisha, udhati, kusikiliza wazee, kumkaribisha mwingine, na daima kuwa katika mwendo; ndiyo ushauri wa Papa Francisko aliowapatia maelfu ya vijana waliokuwapo Jumamosi jioni 6 Oktoba, katika Ukumbi wa Mwenyeheri PauloVI mjini Vatican kwa kushiriki hatua muhimu ya Sinodi ambayo inawahusu wao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Saa 11 Jioni Baba Mtakatifu aliingia katika Ukumbi wa mwenyeheri Paulo wa VI na kutembea akiwasalimia kwa mikono na kubadilishana vikofia wakimpatia na cha kwake. Baadaye alikaa katika jukwaa pembeni akiwa na makardinali na maaskofu. Katika Jukwaa alikaribishwa na salam ya baadhi wawakilishi wa vijana, karibu elfu saba. Vijana waliozungumza ni kutoka Ufilippini, Marekani, Benin, Cuba, India, Hong Kong, Brazil na Ujerumani. Mada ya Mkutao huo wa siku hiyo ilikuwa ni: " Sisi kwa ajili. Wamoja, mshikamano wa ubunifu".

Jinsi gani ya kufanya ili kuwa na furaha? 

Katika shuhuda zilizokuwa zikifuatia, moja baada ya nyingine, imejitokeza swali; je ni jinsi gani ya kuweza kuwa na furaha? ni jinsi gani ya kujaza utupu ambao mara nyingi unahisi ndani hasa usipopata maana ya maisha binafsi au hakuna uwezekano wa kukamilisha ndoto kutokana na ukoasefu wa ajira na fursa? Ni maswali ambayo kutoka ndani ya kina vijana wengi wamemkabidhi Papa Francisko na Mababa wa sinodi ambao wapo mjini Vatican hadi tarehe 28 Oktoba watatafakari juu ya uhusiano wa Kanisa na hali halisi ya vijana.

Si tu  kwanini, lakini ni kutojua ni jinsi gani ya kutatua matatizo. Maswali tisa yaliyotolewa moja kwa moja na kukabidhiwa Papa Francisko: ni barabara ipi ya kuchukua ili kujitafuta binafsi na kugundua thamani ya maisha; jinsi gani ya kuishi kwa dhati wito katika shughuli za kisiasa katikati ya masuala ya ufisadi au mbele ya mapendekezo ya kazi wakati mwingine kinyume na thamani binafsi.  Jinsi gani ya kutobaki na tofauti mbele ya ukosefu wa usawa wa kijamii au kushinda kasumba zinazotazama mgeni kama adui. Ni mantiki zipi za kuweza kuzingatia katika uwepo wa matumizi ya mitandao ya kijamii na tovuti.

Swali jingine kutoka kwa kijana wa nchi ya  Pakistan,lilikuwa ni Kanisa linafanya nini kwa ajili vijana wakristo wanaoishi katika nchi mahali ambapo ukristo umebaguliwa na jinsi gani ya kufanya mabadiliko ya sura hasi na ya uchungu ambayo unaonekana na vijana wengi wa Kanisa wanapokutana na sura tofauti

Hotuba ya Papa bila kusoma: Baba Mtakatifu hakusoma hotuba iliyokuwa imeandaliwa na kuleza mara moja kuwa hana maana ya kijibu maswali hayo, bali kupendlea kwamba itakuwa kazi ya Mababa wa Sinodi, lakini ameongeza,kwamba atawapa maelekezo. Kwa kuanzia katika historia yake binafsi amewaomba wasikilize kwa makini."

Tengenezeni njia ninyi. Ninyi ni vijana  katika safari;katika safari, inayotazama upeo ,na siyo katika kioo. tazameni mbele katika safari, na sio kukaa katika sofa. Mara nyingi inanijia kusema hivi:kijana , mdogo, mvulana, msichana ambaye anakaa katika sofa, anaishia kwenda pensheni akiwa na umri wa miaka 24; ni mbaya sana, hiyo! Na ninyi mmesema vema kujitafuta binafsi. Kujitafuta binafsi sio kioo, kutazama jinsi  ulivyo. Kujitafuta binafsi ni kufanya , ni kwenda katika kutafuta wema, ukweli, na uzuri. Utapata mwenyewe.

Wajibu wa udhati na katika huduma: Papa Francisko pia amesema alivyo guswa na swali juu ya udhati na msimama ambao unajua jinsi gani ukosefu wa udhati uleta mabaya kwa vijana , kama Kanisa linalohubiri, na  baadaye linakwenda katika njia ya malimwengu. Ameongeza: "Lakini hata ninyi mnapaswa kuwa na usahii katika njia zenu".

Mvulana aliomba jinsi gani ya kujikita katika siasa bila kuacha thamani ya kikristo.Papa anajibu: Kuna tatizo la ukosefu wa usawa:ni kupoteza maana ya mamlaka, mi kupoteza kile ambacho Yesu alitueleza kuwa mamlaka ni huduma: mamlaka ya kweli  kuhudumia. La sivyo ni ubinafsi, na kumshusha mwingine, asiweze kukua, kumtawala na kumfanya mtuma,siyo watu walio komaa.Mamlaka ni kufanya watu wakue, na kuwafanya wawe wahudumu wa watu.

Kuweni na uhuru ambo ni ule wa Yesu: Kwa maana hiyo mwaliko wa nguvu kwa vijana ni ule wa kuishi bila kuamini itikadi au masoko:"Ninyi vijana, wavulana na wasichana anasema Papa, ninyi hamna bei. Ninyi siyo bidhaaya kuweka katika mnada . Tafadhali msiache kununuliwa, msiache kudanganywa, msiache kutumikihwa na ukoloni wa itikadili mbali mbali ambazo zinawaeka mawazo katika vichwa vyenu , na mwishoe mnaishia kuwa watumwa, madwa ya kulevya , walioshindwa maisha.

Si tu web: bali ni kukuza uhusiano wa dhati juu ya matumizi ya web, na hivyo  Papa Francisko anawaalika kuzingatia daima uwepo wa dhati wa maisha na uhusiano na wengine:"Ni kweli:kuunganishwa na digital kwa sasa, ni salama, ni haraka; lakini ikiwa umezoea kutumia hivyo, utaishi kama familia kwenye meza ya chakula cha mchana au chakula cha jioni, kila mtu akiwa na  simu, akizungumza na wengine, au kila mmoja pamoja na simu ya mkononi, bila kuwa na uhusiano halisi, na bila uwazi.

Ni kuishi umoja, peke yetu hatwendi mbele: Moja ya mada kuu ya sasa ni kuhusu makaribisho ambayo utafikiri mgeni anakuja kuchuka nafasi, kwa maana ya tabia inayojionesha kwa kumwona mgeni, utofauti na wahamiaji kama hatari, ubaya na adui.  "Leo hii kuna mtindo wa walio wengi ehee, na watu wengi hupendezwa sana, Papa amesema ambao hawataki kuwa na uhusiano na umaarufu wa watu. Wingi ni utumaduni wa watu, utamaduni wa kila mmoja wa watu wenu; unaojitokeza katika sanaa, hujieleza katika sikukuu! Kila mtu huadhimisha sikukuu kwa njia yake: huo ndiyo umaarufu. Lakini umaarufu ulio kinyume: ni ule wa kufungwa juu ya mtindo huu. Tumefungwa, tuko peke yetu. Na tunapokuwa tumefungwa, hatuwezi kwenda mbele. Papa amethibitisha.

 

Kusikiliza wazee na kutazama mbele: Papa Francisko akendelea kufafanua juu ya udhati wa maisha yao, anawaalika kuzungumza na wazee , babu na bibi. " Wao ni mzizi ya dhati ya maisha yao, ni mzizi ya kukua kwao, kuchanua na kutoa matunda. Na anahitimisha " Chukueni mzizi na kuipeleka mbele ili kutoa matudna , na ninyi mtakua hata matunda ya wengine.

08 October 2018, 10:00