Tafuta

Vatican News
Papa Francisko na Mama Maria wa Aparecida Papa Francisko na Mama Maria wa Aparecida 

Papa Francisko awasalimia watu wote nchini Brazil

Katika Fursa ya kuadhimisha Sikukuu ya Mama Maria wa Aparecida, tarehe 12 Oktoba ya kila mwaka, ambaye ni Msimamizi wa nchi ya Brazil, Papa Francisko ametuma ujumbe wake wa matashi mema kwa watu wote wa Brazil kwa njia ya video

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika Sinodi inayoendelea mjini vatican , kuhusu vijana, imani na mang’amuzi ya miito, tarehe 11 Oktoba 2018, Askofu Vilsom Basso, wa Jimbo la  Imperatriz (Brasil) alitengeneza video ya Papa akiwa na kijana msikilizaji kutoka nchini Brazil katika fursa ya Sikukuu ya Maria wa Aparecida ambaye ni Msimamizi wa nchi ya Brazil, siku ambayo inaadhimishwa kila tarehe 12 Oktoba ya kila mwaka.

Papa akiwa na sanamu ndogo mkononi ya Maria wa Aparecida

Papa akiwa na sanamu ndogo mkononi ya Maria wa Aparecida  amezungumza kwa lugha ya kispanyola kwamba: “ Kwa watu wa Brazil, salam zangu za pendo ziwafikie ninyi nyote katika Sikukuu ya Mama Yetu wa Aparecida. Kila mmoja wenu anawaweza kukutana naye katika moyo, kama vile wavuvi, walivyokutana naye kwenye mto. Tafuteni maji ndani ya mioyo yenu na mtapata, kwa sababu yeye ni Mama. Na yeye anaweza kutusindikiza". "Mnikumbuke katika sala zenu".

12 October 2018, 11:52