Tafuta

Vatican News
Katika Sala ya Malaika wa Bwana, Papa anasema kipindi cha Sinodi kimekuwa cha faraja na matumaini Katika Sala ya Malaika wa Bwana, Papa anasema kipindi cha Sinodi kimekuwa cha faraja na matumaini  (ANSA)

Papa katika sala ya Malaika wa Bwana:matunda ya Sinodi yametiwa chachu tayari!

Kipindi cha faraja na matumaini, ndiyo mbiu ya tafakari ya Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini waliounganika mjini Vatican. Papa Francisko ameeleza kwa ufupi hisia za siku 26 za Sinodi ya maaskofu, ambayo imehitimishwa kwa Misa Takatifu tarehe 28 Oktoba

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika tafakari ya Papa Francisko, kusikiliza, kufanya mang’amuzi na  matunda ya kwanza ya Sinodi  ndiyo yamekuwa msisitizo wake kwa mahujaji wote na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 28 Oktoba 2018. Papa Francisko akianza na tafakari amasema: “Asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tumeadhimisha Misa ya kufunga Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana. Somo la kwanza kutoka, Nabii Yeremia (31, 7-9) kwa namna ya  pekee likwenda sambamba na kipindi hiki, kwani neno hilo ni matumaini ambayo Mungu anawapatia watu wake”.

Ni neno la faraja kwa sababu Mungu ni baba wa watu wake, anawapenda na kuwatunza kama wanae (Yer 31,9); anawafungulia upeo mbele yao wa wakati ujao na njia yenye uwezo wa kupitia hata, “kipofu na kiwete, mwanamke mjamzito na anayetaka kujifungua (Yer 31,8), ikiwa na maana ya watu wanye shida. Hiyo ni kwa sababu matumaini ya mungu si ya udanganyifu, kwa mfano anasthibitisha Papa, “ kama ilivyo katika matangazo mengine kwenye luninga,  mahali ambapo wote wanaonekana ni wazuri  na wenye afya,  kumbe  hiyo  ni ahadi kwa watu wa kweli wenye kasoro, nguvu na udhaifu,  kama tulivyo sisi wote. Matumaini ya Mungu ni ahad iya watu kama sisi”, Papa maethibitisha.

Uzoefu wa mababa wa sinodi

Akiendelea kusisitiza juu ya  matumaini anabainisha kuwa: “Neno hili linajieleza vizuri, katika uzoefu ambao tumeuishi katika wiki hizi za Sinodi, na kwamba “ imekuwa ni kipindi cha faraja na matumaini, hasa kilikuwa ni kama kipindi cha kusikiliza”. “Kusikiliza kwa dhati inahitaji muda, umakini na ufunguzi wa akili na moyo. Hata hivyo ahadi hii ilibadilika kila siku kwa faraja kutokana na kwamba, anabainisha, “katikati yetu  kulikuwa na uwepo wa kupendeza na kichochea cha vijana, wakiwa na historia zao na michango yao”. “Kwa njia ya ushuhuda wa Wababa wa Sinodi, katika ukweli halisi wa vizazi vipya umeingia katika Sinodi, kwa namna ya kusema, kutoka kila bara na kutoka katika  hali mbalimbali za kibinadamu na kijamii”. Kwa mtazamo wa msingi wa kusikiliza, Papa anabinisha kuwa, “ tulijaribu kusoma kwa dhati ukweli na kuelewa ishara za nyakati zetu. Na mang’amauzi kijumuiya yamefanywa kwa mwanga wa  Neno la Mungu na la Roho Mtakatifu”.

Zawadi ya sinodi ya maaskofu

Hiyo ni mojawapo ya zawadi nzuri sana ambazo Bwana hufanya kwa Kanisa Katoliki, yaani, kukusanya sauti na nyuso kutoka katika hali halisi na  tofauti, hivyo kuweza kujaribu kufanya tafsiri zinazozingatia utajiri na ugumu wa matukio lakini daima kwa mwanga wa Injili. Papa amesema na kwamba, “katika siku hizi, tulijadili kwa pamoja jinsi gani  ya kutembea pamoja kupitia changamoto nyingi, kama  vile ulimwengu wa digital, matukio ya hali ya uhamiaji, hisia za mwili na ngono, majanga ya  vita, unyanyasaji na nguvu”.

Kutokana na hiyo, “Matunda ya kazi hii tayari yameanza “kuwa na chachu” Papa amethibitisha , kama juisi ya zabibu iliwekwa kwenye  mapipa mara baada ya baada ya mavuno. Sinodi ya Vijana ilikuwa ni mavuno mazuri na ahadi ya divai nzuri. Lakini ameongeza, “ningependa kusema kwamba matunda ya kwanza ya Sinodi hii inapaswa kubaki kwa dhati  katika mfano wa njia ile ambayo wamejaribu kufuata, tangu awamu ya kwanza ya maandalizi”. Ni mtindo wa Sinodi ambao hauna lengo kuu kama kuandaa hati, licha ya kwamba ni wenye thamani na  muhimu. Zaidi ya hati,ni muhimu kueneza namna ya kufanya kazi pamoja na vijana na wazee, kwa kusikiliza na katika kufanya mang’amuzi, ili kufikia uchaguzi wa kichungaji ambao unajibu hali halisi”. Papa amehimiza.

Kwa kufanya hivyo, “ tuombe kwa maombezi  ya Bikira Maria.  Yeye ambaye ni Mama wa Kanisa tumkabidhi shukranii kwa Mungu kwa ajili ya zawadi ya sinodi hiyo. Na yeye atusaidie katika kupeleke mbele kile ambacho tumepata uzoefu, bila hofu, katika maisha ya kawaida ya kijumuiya.  Roho Mtakatifu aweze kukuza  matunda ya kazi yetu kwa njia ya ubunifu wa mawazo yake ya hekima  na ili tuweze kutembea pamoja na vijana katika dunia nzima!

28 October 2018, 15:29