Tafuta

2018.10.28 Misa Takatifu ya kushukuru kwa hitimisho la Sinodi ya Maaskofu 2018.10.28 Misa Takatifu ya kushukuru kwa hitimisho la Sinodi ya Maaskofu 

Papa:kusikiliza,ukaribu na kushuhudia ni hatua za imani ya kikristo!

Katika mahubiri ya Misa Takatifu ya Kufunga Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, mahubiri ya Papa yamejikita katika hatua tatu za safari ya imani ya kwamba ni kusikiliza, kuwa na ukaribu na kushuhudia

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Tukio tulilosikia ni simulizi la mwisho wa shughuli ya kitume ya Yesu ambapo Mwinjili Marko anaonesha kuwa  muda kitambo Yesu ataingia katika mji wa Yerusalemu kwa ajili ya kifo na ufufuko. Bartimayo alikuwa wa mwisho kumfuata Yesu katika njia, akiwa ni mwombaji pembezoni mwa njia  ya Yeriko, na takuwa mtu anatakayefuata na wengine kuelekea Yerusalemu. Hata sisi tumetembea pamoja, na tumefanya Sinodi na sasa Injili hii inatoa ushauri, wa  hatua tatu msingi kwa ajili ya kutembea katika imani”. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko, Jumapili 28 Oktoba 2018, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wakati wa kufunga Sinodi ya XV ya maaskofu ambayo iliongozwa na mada ya Vijana, imani mang’amuzi ya miito”. Katika mahubiri hayo, anafafanua zaidi juu ya hatua tatu kuu za kutembea katika imani ya kweli.

Yesu anasikiliza kilio cha Bartimayo na ndiyo hatua ya kwanza

Papa Francisko akiendelea na mahubri yake amesema: hawali ya Yote Bartimayo, maana  ya neno ni “ mwana wa Timayo”. Na Somo lenyewe, linafafanua: mwana wa Timayo, Bartimayo ( Mk10,46. Lakini wakati Injili inasema hayo , inajitokeza sehemu nyingine inayojionesha kuwa; Baba hayupo. Bartimayo amelala pembeni mwa barabara, nje ya nyumba bila baba: hakupendwa, bali ameachwa peke yake, Ni kipofu na hakuna anayemsikiliza. Yesu anasikiliza kilio chake. Anapokutana naye, anamwacha azungumze. Haikuwa ni shida kutambua kwa haraka, nini angeomba Bartimayo. Inaonesha wazi ni kipofu na anataka kuona. Lakini Yesu hana haraka, kwa maana anampatia muda wa kumsikiliza. Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, tazama hiyo ndiyo hatua ya kwanza kwa ajili ya kusaidia hatua ya imani yaani kusikiliza .Ni mtu wa sikio; kusikiliza, kabla ya kuzungumza!

Kinyume chake che waliokuwa  na Yesu wanamkemea Bartimayo ili anyamaze. Kwa upande wa mitume, mwenye kuhitaji alikuwa ni msumbuafu katika safari yao, kwa maana hategemewi katika mpango. Wao walikuwa wanapendelea muda wao na ule wa Mwalimu, na maneno yao katika kusikiliza wengine. Papa anaongeza kusema,  hawa walikuwa wanamfuata Yesu lakini katika akili yao kuna mipango yao. Ni hatari ambayo lazima kujiangalia na , Baba Mtakatifu amethibitisha. Na ndiyo maana kinyume chake, Yesu katika kilio cha sauti ya kuomba msaada siyo usumbufu ,unaoaweka vikwazo katika safari, bali ni suala la maisha.

Ni jinsi gani ilimvyo muhimu kwa upande wetu kusikiliza maisha! Watoto wa Baba aliye mbinguni, anawasikiliza wana wake. Si meneno yasiyo na maana, bali ni mahitaji ya jirani. Kusikiliza kwa upendo, uvumilivu kama Mungu anavyofanya kwetu sisi kwa njia ya sala zetu ambazo mara nyingi zinarudiwa na   Mungu hachoki kamwe, bali anafurahia daima tunapomtafuta. Tumwombehata sisi neema ya kuwa na moyo wa mpole wa kusikiliza.

Kwa niaba sisi wote wazima; tusameheni, iwapo mara nyingi hatukuweza kuwasikiliza

Baba Mtakatifu akiwageukia vijana amesema: “Ninataka kuwambia vijana, kwa niaba ya wote wazima; tusameheni, iwapo mara nyingi hatukuweza kuwasikiliza; iwapo badala ya kufungua mioyo tumeziba masikio. Kama Kanisa la Yesu,tunatamani kujikita katika usikivu wenu kwa upendo na kwa uhakika wa mambo mawili: ya kwamba maisha yenu ni tunu kwa Mungu, sababu Mungu ni kijana na anapenda vijana; na kwamba maisha yenu ni tunu kwa ajili yetu na zaidi ni lazima ili kwenda mbele

Hatua ya pili ni kusindikiza katika safari

Baada ya kusikiliza, hatua ya pili ni ile ya kusindikiza safari ya imani: ili kuweza kuwa karibu. Papa Francisko anasema: tunamtazama Yesu ambaye haweki mwakilishi yoyote katika “ umati ambao ulikuwa unamfauta, bali anakutana  yeye binafsi na Bartimayo. Alimwambia unataka nikufanyie nini? .Unataka nini. Yesu anajifananisha na Bartimayo, yeye hakuanzia na matarajio yake; siyo mimi nifanye, na si mimi nizungumze  badala yako; si kwa mujibu wa mawazo yaliyo kwisha wekwa na kila mtu, bali kwa ajili yako, katika hali yako. Hivyo ndivyo  anafanya Mungu, anakuhusisha binafsi kwa upendo na kwa namna ya  kipekee, kwa kila mtu. Kwa  namna yake ya kutendo Papa Francisko anathbitisha, ndiyo ujumbe  wake ulio tayari, na ndiyo imani inachanua katika maisha.

Imani ni maisha, ni kuishi kwa upendo wa Mungu ambaye alitubadili kwa namna ya kuishi kwetu

Iwapo imani inajikita zaidi katika mazoea tu ya mafundisho, ipo hatari ya kuzungumza kwa kichwa tu, bila kuguswa moyo. Iwapo inajikita katika mambo ya kufanya tu, ipo hatari ya kugeuka na siyo ya  kimaadili na kupunguzwa katika kijamii. Imani badala yake ni maisha: ni kuishi kwa upendo wa Mungu ambayo alitubadili namna ya kuishi kwetu. Hatuwezi kuwa mafundishaji  au wanaharakati; tunaitwa kupeleka mbele kazi ya Mungu kwa jinsi ya Mungu, katika ukaribu, yaani kuwa karibu naye, katika muungano  kati yetu, karibu na ndugu zetu. Na tazama, Ukaribu, ndiyo siri ya kuonesha moyo wa imani, siyo mtindo mbadala. Kujifanya karibu, ni kupeleka habari mpya ya Mungu katika maisha ya ndugu, ndiyo dawa dhidi ya kishawishi cha orodha ambayo tayari imewekwa. Papa Francisko ameongeza kusema kuwa; “ tutazama kama sisi ni wakristo wenye uwezo wa kuwa na  ukaribu, tunao ondokana na mahesabu yetu ili kukutambua wale wasio kuwa wa kwetu, na ambao kwa shuaku kubwa Mungu anawatafuta.

Kishawishi katika maandiko: kunawa mikono kama pilato

Kuna kishawishi ambacho kinajitokeza mara nyingi katika Maandiko cha kunawa mikono. Papa anabainisha kuwa ndicho kile cha umati katika Injili ya siku; ni kile alichokifanya Kaino kwa  Abeli, ni kile alichofanya Pilato kwa  Yesu, kunawa mikono.  Lakini sisi tunataka kumuiga Yesu kwa jinsi ya kuchafua mikono yetu. Yeye katika njia ( Yh 14,6) , kwa ajili ya Bartimayo alisimama njiani;Yeye ni mwanga wa dunia( Yh 9,5) aliinama juu ya kipofu. Tutambue kuwa Bwana alichafua mikono yake kwa ajili ya kila mmoja wetu na kwa kutazama msalaba, pale tukumbuke kuwa Mungu alitukaribia katika dhambi na mauti. Alijifanya kuwa karibu yangu na yote hayo  yalianzia hapo.  Kwa ajili ya pendo wake tunapo karibia jirani, tunabeba maisha mapya na siyo walimu wa wote, si wataalam wa mambo matakatifu, lakini ni mashuhuda wa upendo unaookoa.

Hatua ya tatu ni kushuhudia

Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake amefafanua juu ya hatua ya tatu ya kushuhudia kwamba; tutazame mitume wanaomwita Bartimayo, awendi kwake anayeomba omba  na kutulizwa na senti, hata kumpatia ushauri; wanakwenda kwa jina la Yesu. Kwa dhati wanamweleza maneno  matatu tu na yote ya Yesu, jipe moyo! Inuka, Anakuita (Mk 10, 49) . Ni Yesu peke yake katika Injili anasema jipe moyo, kwa maana ni Yeye peke yake anayefufua moyo. Ni Yesu peke yake katika Injili anasema inuka, ili kuponesha Roho na mwili. Ni Yesu Peke yake anaita, akibadili maisha kwa yule anayemfuata, na kumsimamisha aliye ardhini, kwa kuleta mwanga wa Mungu katika giza nene la maisha.  Watoto wengi, vijana wengi kama Bartimayo wanatafuta mwanga katika maisha. Wanatafuta upendo wa kweli. Kama Bartimayo, licha ya kuwapo watu wengi, yey anamwomba Yesu, hivyo hata wao wanaomba maisha, japokuwa mara nyingi ni ahadi za uongo na ni wachache ambao wanajijali ki ukweli.

Siyo Mkristo ambaye anasubiri  ndugu aje kubisha hodi katika milango yetu; wanapaswa kwenda kwao, si kujipeleka  wao binasi, bali Yesu. Yesu anatutuma kama wale mitume, anatia moyo na anaamsha kwa jina lake. Anatutuma kwenda kuwambia kila mmoja; Bwana anaomba ujiajichie  ili upate kupendwa naye! Ni mara ngapi, badala ya kuupeleka ujumbe huu wa wokovu tumebaki nao katika maelekezo yetu, katika mihuri yetu ndani ya Kanisa! Mara ngapi, badala ya kusema maneno ya Bwana, tumetumia maneno mengine yenye kuwa na mawazo yetu na kwa faifa binafsi! Mara ngapi watu wanahisi uzito wa taasisi badala ya uwepo karibu wa Yesu rafiki! Na kwa maana hiyo tumegeuka kuwa  katika shirika lisilo la kiserikali na siyo kama jumuiya ya waliokombolewa ambao wanaishi furaha ya Bwana

Kusikiliza, kuwa karibu, kushuhudia

Safari ya imani katika Injili inahitimishwa kwa namna nzuri na ya kushangaza na Yesu anatamka: “Enenda zako, Imani yako imekuokoa” (Mk 10,52). Licha ya hayo Bartimayo  hakuwa amekiri imani, hakutenda kazi yoyote; yeye aliomba huruma. Kwa maana hiyo ktendo la kuhisi mwitaji wa wokovu ndiyo mwanzo wa mani. Ndiyo njia ya moja kwa moja kwa ajili ya kukutana na Yesu. Imani iliyo mwokoa Bartimayo haikuwa katika mawazo yake yaliyo  wazi juu ya Mungu, bali katika kumtafuta na  utashi wa kukutana naye. Imani ni suala la kukutana na siyo nadharia; ni katika kukutana na Yesu anayepita, katika kukutana na moyo unaodunda wa Kanisa. Kwa njia hiyo, si katika kuhubiri yetu, bali ni katika ushuhuda wa  maisha yetu na ndiyo utakuwa mwafaka!

Akihitimisha amesema: “Ninyi nyote mlioshiriki katika safari ya pomoja, ninasema asante kwa ushuhuda wenu. Tumefanya kazi katika muungano na kwa uwazi, kwa utashi wa kuhudumia Mungu na watu wake. Bwana awabariki katika hatua zenu ili muweze kusikiliza vijana, kuwa karibu, na kushuhudia na wao furaha ya maisha yenu. Yesu.

28 October 2018, 12:29