Hitimisho la Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana mjini Vatican Hitimisho la Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana mjini Vatican 

Papa:Ni kipindi cha kulinda Kanisa dhidi ya Mshtaki Mkuu kwa sala na toba

Wahusika wa kwanza wa hati ya mwisho ya Sinodi ni sisi. Ndiyo moja ya kiini cha hotuba ya Papa Francisko, bila kuandika wakati wa kufunga kazi ya Mkutano Mkuu wa XV wa Sinodi ya Maaskofu iliyoongozwa na mada ya “Vijana, imani na Mang’amuzi ya miito” Papa katika mazungumzo yake, amesisitiza kwamba hata sisi kama wana tu wadhambi, lakini Kanisa lisichafuliwe

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni wakati wa kulinda Kanisa dhidi ya mshtaki  Mkuu kwa njia ya sala na kitubio. Sisi kama watoto wote tu wachafu, lakini Kanisa lisichafuliwe. Ni sisitizo kuu la Papa Francisko, usiku wa tarehe 27 Oktoba 2018 wakati wa kutoa hotuba yake  bila kuandika katika kufunga kazi ya Sinodi ya Maaskofu, iliyokuwa inahusu vijana. Sinodi ilianzia tarehe 3 Oktoba ambayo inafungwa rasmi na Misa Takatifu 28 Oktoba, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu akisistiza, anaomba kuacha mioyo yetu ifanya kazi katika Hati ya mwisho, na anasema:“ Watu wa kwanza wahusika wa Hati hiyo ni sisi”.

Sisi ndiyo wahusika wa kwanza wa Hati ya mwisho

Akiendelea na hotuba yake kwanza, Papa anasisitiza kuwa, Sinodi siyo Bunge. “Ni nafasi ya ulinzi kwa njia ya Roho Mtakatifu kutekeleza hilo” na kwa njia hiyo amefafanua kuwa, ​​“taarifa inayotolewa ni ya kawaida na siyo “vitu maalum”. Kadhalika akiendelea na hotuba yake, Papa amekumbusha kwamba, “Matokeo ya Sinodi siyo hati”, kwa maana anasema, “Sisi tumejazwa na nyaraka” na hivyo anaongeza:  “Sijui kama waraka huu utafanya kitu nje”,  japokuwa anao uhakika kuwa, “ninajua kwamba ni lazima hufanyike ndani mwetu, na lazima kufanya kazi ndani mwetu”.

“Sasa Roho anatupatia hati hii ya kufanya kazi moyoni mwetu. Sisi ni wapokeaji na wahusika wa waraka huu. Sio watu nje. Na ili hati iweze kufanya kazi, ifanyike sala na hati, kuisoma, kuomba mwanga na mengine zaidi ... lakini hasa hati hii cha msingi ni kwa ajili yetu”. Anaongeza kueleza, “ Ndio, itasaidia wengine wengi, lakini wahusika wa kwanza ni sisi: kuna Roho ambaye amefanya yote haya na anarudi kwetu. Tafadhali msisahau”. Ameomba Papa Francisko!

Kanisa lisichafuliwe ni wakati wa kumtetea na kumlinda Mama 

Zaidi ya hayo Papa ameweka msisitizo juu ya utakatifu wa Kanisa, ambalo linapaswa kutetewa na kulindwa kwamba: “Mama yetu ni mtakatifu”, lakini watoto, yaani  “sisi sote ni wenye dhambi”,  “kwa sababu ya dhambi zetu, daima Mshtaki Mkuu” hutumia fursa ya kuzunguka dunia akiwatafuta wale atakao washitaki. Na kwa muda huu yuko anatushitaki kwa nguvu”, anaongeza, “na mashtaka haya ni mateso”.  Amesema hayo  kwa kubainisha juu ya “mateso ya Wakristo katika sehemu mbalimbali duniani. Lakini pia inakuwa ni aina nyingine ya mateso ambayo ni “mashtaka yanayoendelea kulichafua Kanisa”. Amesema Papa.

Pamoja na hayo amesema, “ Kanisa halipaswi kuchafuliwa”, “watoto ndiyo, yaani sisi sote ni wachafu; lakini mama siyo hivyo”.  Na ndiyo maana huu  ni wakati wa kumtetea Mama. Na mama analindwa dhidi ya Mshtaki Mkuu kwa sala na toba”, anaongeza ufafanuzi: “ndiyo sababu niliomba katika mwezi huu unaoisha siku chache zijazo, kusali Rosari, ili kuomba kwa Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, kuomba  kwa Mama Yetu daima ili aweze kufunika  Mama yetu Kanisa daima …Tuendelee kufanya hivyo. Kwa maana ni wakati mgumu, kwa sababu mshtaki kupitia kwetu atataka kushambulia Mama, na Mama huyo hasiguswe. Na hili ndilo nilitaka kusema kwa moyo wote mwishoni mwa Sinodi! Papa amesisitiza!

Mwanzoni mwa hotuba yake bila kusoma, Papa alipendelea  kuwashukuru wote waliofanya na kufanikisha kazi ya Sinodi hiyo ambayo inakaribia kumalizika. Kwa namna ya pekee, hasa shukrani kwao, vijana, ambao amesema, “walileta muziki wao hapa katika ukumbi huo: Neno “Muziki” ikiwa na maana ya utani maana neno la kidiplomasia ni kelele kidogo! Amefafanua Papa! Na hatimaye kwa kumalizia, Papa  Francesco anakumbusha  kuwa sasa, Roho Mtakatifu “anatupatia hati hii sisi sote, hata kwa ajili yangu, ili kutafakari kile anachotaka kutuambia”.

 Mwisho waliimba wimbo wa Shukrani ( Te deum) kwa lugha ya kilatino na kutawanyika kutoka ukumbini tayari kwa kupata mlo wa usiku na kulala, ambapo Papa Francisko aliwatakia mlo mwema na usiku mwema.

28 October 2018, 09:59