Vatican News
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana  (AFP or licensors)

Papa:Ukuu wa uhuru wa Mungu kwetu sisi ni changamoto!

Jumapili 30 Septemba wakati wa tafakari yake katika sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko ametoa ushauri wa kujifunza kutoka kwake Yesu Kristo. Kristo anatualika kutofikiria kwa mujibu wa kanuni ya rafiki/adui,sisi/ wao, aliye ndani / aliye nje, bali kwenda zaidi ya upeo huo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu akianza tafakari lake wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili tarehe 30 Septemba 2018, kwa waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican, anaonesha, “jinsi gani ukuu wa uhuru wa Mungu anao utoa kwetu  sisi, unakuwa ni changamoto na Papa kushauri namna ya kubadilisha tabia zetu na mahusiano yetu”.

Injili ya siku inaonesha jinsi gani wafuasi wa waliona mtu aliyekuwa siyo mfuasi wa Yesu, lakini akitoa mapepo. Lakini jibu la Yesu, Papa anakumbusha, linakwenda katika mwelekeo tofauti: “ Yohane alimwambia Yesu, Mwalimu tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu”.

Kuwa makini kwa ajili ya wema ulio msafi

Papa Francisko ametoa ushauri kuwa, “ni lazima kujifunza kutoka kwa Yesu na kuwa makini kwa ajili ya wema, uzuri na ukweli ambao unatimizwa, ambao si kwa jina na mtu anayeutimiza. Ni Yesu tu peke yake ambaye kwa ukamilifu, ulio huru na wazi kwa Roho wa Mungu, ambaye kwa kila tendo halina kizuizi na mtu yoyote au  mpaka na ukuta”.

Kujitosheleza ni mzizi wa upropaganda

Pamoja na kuelewa tabia za kibinadamu za wafuasi wake, zilizojieleza katika tukio la Injili, Papa Francisko anaonya “kuhusu hofu ya mashindano ya wakristo ambayo yamekuwapo karibu kila nyakati na ambayo hata leo hii yapo katika mchakato  wa maisha yetu sisi”. Na hiyo hasa inatokana na neno “kwa sababu siyo mwenzetu”.  Papa Francisko anafafanua, hii ni kuangukia namna ya kujiona katikkujitosheleza, na ikiwa ni mzizi wa propaganda. Kanisa lililobarikiwa, halikui kwa njia ya upropaganda, bali kwa njia ya ushuhuda kwa wengine kwa njia ya Roho Mtakatifu”.

Inahitaji kufanya tafakari la dhamiri

" Kubaki umefungiwa ndani ya banda kwa kile ambacho tunajua au kinatuhusu, kinatoa msukumo wa kuhukumu wengine. Badala yake, Papa Francisko anaendelea na kufafanua:lazima kufanya tafakari la dhamiri binafsi na kufutilia mbali zaidi bila kuwa  ahadi ya kile ambacho kinaweza kuleta kashfa kwa watu, zaidi  walio wadhaifu katika imani.

Amehitimisha akiomba Bikira Maria mfano wa upole wa kukaribisha mshangao wa Mungu na ili atufundishe kupenda jumuiya zetu bila kuwa na wivu au kujifungia binafsi, ili tuweze kuwa wazi katika upeo mpana wa matendo ya Roho Mtakatifu!

01 October 2018, 09:08