Tafuta

Vatican News
Papa: Mgonjwa akipendwa kivuli cha Ethanasia hupotea Papa: Mgonjwa akipendwa kivuli cha Ethanasia hupotea  (ANSA)

Papa:uhusiano na mgonjwa unahitaji heshima, uhuru wake na uelewa

Imani ya mgojwa ya kuweza kupona na umakini wa mgonjwa kama ndugu anayeteseka, ndiyo dhana ambazo Papa Francisko amegusia katika hotuba yake kwa washiriki 70 wa Semina ya IV juu ya Maadili katika uendeshaji wa afya, aliowapokea asuhubi ya tarehe Mosi Oktoba 2018 mjini Vatican

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Iwapo mtu anahisi kupendwa, kivuli hasi cha eutanasia, hupotea au hakipo hata kidogo”. Ni maneno aliyo thibitisha Papa Francisko kwa washiriki karibia 70 wa Semina ya IV juu ya Maadili katika uendeshaji wa Afya, aliokutana nao mjini Vatican tarehe Mosi Oktoba 2018. Katika hotuba yake, kwa lugha ya kihispania, Baba Mtakatifu amemsalimia Askofu Msaidizi, Alberto Bochatey, wa Plata, raisi wa Tume ya Afya ya Baraza la Maaskofu wa Argentina na Mkurugenzi Mkuu wa shughuli hiyo Cristian Mazza, Rais wa Chama cha Afya na taasisi nyingine zinazowakilishwa, kwa fursa ambayo wametoa katika Semina hiyo, iliyoandaliwa chini ya mwongozo wa Baraza la Kipapa la Maisha, semina iliyo anza tarehe 1-5 Oktoba 2018 mjini Vatican

Katika mgonjwa ni sura inayoteseka

Hotuba ya Papa Francisko kwa washiriki wa semina hiyo, umezungukia zaidi ya yote  katika maneno matatu: miujiza, kutunza na imani.  Baba Mtakatifu amesema, “katika ulimwengu wa afya kwa ujumla na kwa namna ya pekee katika Bara la Amerika Kusini  inaishi kipindi cha kipeo cha uchumi na matatizo ambayo yanahusiana na upatikanaji wa matibabu na madawa na matatizo ambayo yanaweza kusababisha kuangukia katika hali ya kukata tamaa”. Lakini kama ni kweli kwamba kuwa uhusiano wa ghara ya ustawi unasabishawa na ugawanyaji wa rasilimali, Papa anawaalika watafuta kila njia ya kumfanya mgonjwa awe  ndugu.

Na hiyo ni katika utambuzi ya kwamba hata kama huwezi kutoa matatizo yote, lakini inawezekana kupeleka mabadiliko ya kiakili na kidhamiri. Na kwa namna hiyo suluhisho liwezekana kuwa la kueendeleza kwa njia kukubaliana kati ya umma na binafsi, sheria na maadili, haki ya kijamii na ujasiriamali mambo ambayo siyo mawazo yasiyo sahihi kabisa bali ni mtu halisi, ni uso ambao mara nyingi huteseka. Kwa maana hiyo amasisitiza: “muwe na ujasiri na ukarimu”, katika matumizi ya zana za kiuchumi na kiteknolojia na kisayansi, kwa sababu anaongeza Papa, “wale wanaopata faida na hasa masikini, watafurahia juhudi zanu na mipango yenu”.

Kwa kuwasinidikiza, kivuli cha euthanasia kinatoweka

Kwa kusisitiza zaidi Papa amesema, pia inachukua umakini kwa kuwa na huduma ya wagonjwa ambayo haijumuishi tu katika matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu na aishii tu katika kurejeshwa kwa afya. Lakini hiyo inaonekana hata katika huduma za mbadala. Na kwa maana hiyo, “kwa sasa tunakaribia kuwa na tabia ya kuhalalisha euthanasia, lakini tunajua kwamba inapotokea kusindikizwa kwa mshikamano wa kibinadamu na ushirikishwaji, mgonjwa sugu au mgonjwa aliye karibu  kumaliza muda wake anahisi kweli ushirikishwaji huo.

Kwa maana hiyo, “hata katika hali hizi ngumu, kama mtu anahisi kupendwa, kuheshimiwa, kukubaliwa, kivuli hasi cha euthanasia hutoweka au karibu haipo, kwa sababu thamani kuwepo kwake  inapimwa kutokana na uwezo wake wa kutoa na kupokea upendo, na si kutokana na uzalishaji wake! Wahudumu wa afya, kwa hiyo, wanapaswa kushiriki katika kupyaisha  ujuzi wao wa  wa kuendelea ili kukabiliana na wito wao kama “wahudumu wa afya na katika suala hili la  “Mkataba Mpya wa Wakala wa Afya”  ambacho ni chombo muhimu ameelekeza Papa Francisko.

Imani kwa mgonjwa ili apone

Kadhalika imani ya mgonjwa ndani yake mwenyewe na katika uwezekano wa wa kupona unahitajika. Hapa kuna sehemu kubwa ya mafanikio ya tiba. Lakini pia ni muhimu kwamba wahudumu wanaweza kutekeleza kazi zao katika mazingira ya utulivu. Pamoja na hayo Papa  anaonya juu ya hatari kwamba, kwa sababu ya utata wa mfumo wa afya, “masharti ya mkataba” uwe ndio ambayo unanzishwa  kati uhusiano wa mhudumu  wa afya na mgonjwa, kinyume na hiyo uaminifu huvunjika.

Na badala yake, Papa anaomba kuwepo na  jitihada za kudumisha dhamana hii ya ubinadamu wa kina katika utimilifu wake, kwa maana  uhusiano na mgonjwa unahitaji heshima ya uhuru wake na tahadhari, uelewa na mazungumzo kuwa kielelezo cha ahadi inayofanywa kama huduma.  Anawatia moyo kwamba kila mtu awe na busara, upendo na kuwa karibu na mtu mgonjwa ili kutimiza wajibu wake na ubinadamu wake mkubwa.

 

01 October 2018, 14:40