Msafara wa Picha Takatifu kuelekea katika uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Msafara wa Picha Takatifu kuelekea katika uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 

Papa:tupeleke Injili pamoja na vijana na ndiyo njia!

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amekumbusha juu ya Siku ya Kimisionari duniani. Mwaka huu inaongozwa na mada kuwa: “pamoja na vijana, tupeleke Injili kwa watu wote” na kwa pamoja na vijana ndiyo njia!

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

“Wapendwa kaka na dada, jana huko Malaga Uhispania walimtangaza mwenyeheri Padre Mjesuit, Tiburzio Arnáiz Muñoz, Mwanzilishi wa Shirika wa Wamisionaria wa Mafundisho vijijini. Tumshukuru Bwana kwa ajili ya ushuhuda wa mtumishi wake wa Mapatano na ambaye hakuchoka kutangaza Injili, hasa kati ya wanyenyekevu na walio sahauliwa. Kwa mfano wake, utusukume kuwa wahudumu wa huruma na wamisionari jasiri katika kila sehemu; na maombezi yake yatusaidie katika safari yetu. Kwa ajili ya Mwenyeheri BeatoTiburzio tumpigie makofi!

Siku ya Kimisionari duniani

Hayo ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote na waamini katika kiwanja chaa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili 21 Oktoba 2018. Akiendelea amesema:“Leo ni maadhimisho ya Siku ya Kimisionari duniani. Kwa kuongozwa na mada, “pamoja na vijana, tupeleke Injili kwa wote”. Pamoja na vijana ndiyo njia! Baba Mtakatifu ameongeza: "na ni ukweli kwamba, neema ya Mungu ambayo tunaifanya ya uzoefu katika siku hizi kwenye Sinodi ambayo inawawahusu wao katika kuwasikiliza na kuwahusisha, tunagundua shuhuda nyingi za vijana ambao katika Yesu wameweza kupata maana ya furaha ya maisha”

Mara nyingi wamekutana naye kwa neema ya vijana wengine, ambao wamekwisha tayari kushiriki katika usindikizwaji wa kaka na dada ambao ni Kanisa. Tusali ili kizazi kipya kisikose kutangaziwa imani na kuitwa kushirikiana katika utume wa Kanisa. Aidha Papa anafikiria wakristo wengi wanaume na wanawake, walei, watawa, mapadre, maaskofu ambao wametoa maisha yao na wanaendelea hadi leo hii kuwa mbali na nchi zao, wakitanzagza Injili. Kwa wote Baba Mtakatifu ameomba kuwaonesha upendo, shukrani na sala, kwa kusali kwa pamoja kwa ajili yao, sala ya salam Maria.

 

 

 

22 October 2018, 12:54