Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 

Papa:Tuombe nuru ili tusifikiri kwa mantiki ya dunia, bali ya Mungu

Katika tafakari ya Papa Francisko Jumapili 21 Oktoba 2018 anasema: wakati mitume walikuwa wanazungumza juu ya “kiti cha utukufu” kile cha kukaa karibu na Kristo Mfalme, Yesu alikuwa anazungumza juu ya “kikombe” cha kunywea cha ubatizo, cha kupokea, kwa maana ya mateso na kifo chake

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sura za Injili ya siku kutoka Marko ( Mk 10,35-45) inaeleza kuwa, Yesu kwa mara nyingine tena na kwa uvumilivu mkubwa anatafuta namna ya kuwasahihisha mitume wake, ili wawez kubadili mantiki ya ya dunia hii, na kufikiria ile ya Mungu. Fursa hiyo inajitokeza kutokana na ndugu wawili Yakobo na Yohane, mitume wawili wa kwanza kabisa ambao Yesu alikutana nao na kuwaita wamfuate. Na tayari walikuwa wamekwisha tembea naye safari ndefu kwa maana hiyo, wao sasa ni sehemu moja kabisa ya kikundi cha mitume kumi na mbili. Wakati wako katika njia kuelekea Yerusalem, mahali ambapo, mitume kwa shauku kubwa walikuwa wanatarajia Yesu katika fursa ya sikuu ya Pasaka, atafanya upyaisho wa Ufalme wa Mungu na ndugu wawili walikwenda haraka na kumkaribia Mwalimu wao kwa maombi yao: “Turuhusu kukaa katika utukufu wako, mmoja kulia na mmoja kushoto kwako” (Mk, 10, 37)

Ni mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili 21 Oktoba kwa mahujaji na waamini wote kutoka pande za dunia, katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko, kwa kuongozwa na Injili ya Siku ya Mtakatifu Marko, anathibitisha kuwa, “Yesu anatambua vema kuwa Yakobo na Yohane, kweli wanashauku kubwa kwa ajili yake na kwa sababu ya Ufalme, lakini pia anatambua kuwa matarajio yao yamechafuliwa na roho ya dunia”. Kwa njia hiyo, anawajibu: “Ninyi hamtambui kile mnachoomba” (Mk 10,38). Wakati wao walikuwa wanazungumza juu ya “kiti cha utukufu” kile cha kukaa karibu na Kristo Mfalme, Yeye alikuwa anazungumza juu ya “kikombe” cha kunywea cha ubatizo, cha kupokea, kwa maana ya mateso na kifo chake.

Yakobo na Yohane wakiwa wanashangaa daima fursa waliyokuwa wanatarajia, wanaitikia kwa nguvu zao, ndiyo tunaweza! Lakini hata hivyo Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, hapa inaonesha jinsi gani, bado hawajatambua kweli kile wanacho sema. Yesu anawatawangazia kuwa, Kikombe chake wataweza kukinywea na ubatizo wake wanataupokea, kwa maana hata wao kama ilivyo mitume wengine, watashiriki msalaba wake, itakapowadia saa yao. Pamoja na hayo, Yesu lakini anaendelea kusema: kukaa kwangu kulia au kukaa kushoto, siyo jukumu lake kuwajalia; ni kwa wale walioandaliwa ( Mk 10,40). Hiyo ni kama kuwaambia, sasa ninyi nifuateni na kijifunza njia ya upendo wa kupoteza, lakini zawadi yenu ataifikiria Baba wa mbinguni. Njia ya upendo daima ni ile ya kupoteza kwa sababu kupenda maana yake ni kuacha ubinafsi pemebeni na kujitosheleza ili kuweza kuhudumia wengine.

Yesu alitambua mara moja kuwa mitume wengine kumi, walikuwa wamekasirikia Yakobo na Yohane na kujionesha wazi na kuwa na hisia za kidunia.  Kutokana na jambo hilo, linampatia fursa Yesu kuwapa somo, ambalo ni somo kwa ajili ya wakristo wote wa nyakati zote hata kwetu sisi, Baba Mtakatifu anabinisha. Na ndipo, “Yesu akawaita, akawaambia, mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. (Mk 10, 42-44).

Ndiyo kanuni ya kikristo.

Ujumbe wa Mwalimu uko wazi kwa sababu wakati wakuu wa Mataifa wanajenga viti vyao, kwa ajili ya utawala wao, Mungu anachagua kiti kibaya, yaani msalaba, mahali pa kutawala wakati unatoa maisha: “Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumikia, na kutoa nafsi yake kwa ajili ya fidia ya wengi”. Njia ya kutoa huduma ndiyo dawa mwafaka dhidi ya maradhi ya kutafuta daima nafsi za kuwa wa kwanza; ni dawa ya wale wanaopenda kukwea, kwa kutafuta nafasi za kwanza, na ambazo zinaaambukiza wengi katika mantiki ya kibinadamu, wala hizo pia haziwaachi hata wakristo, watu wa Mungu, hata katika uongozi kwenye ngazi ya Kanisa. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, kama mitume wa Kristo, tupokee Injili hiyo kama tahadhari ya kuweza kubadilika, na ili kushuhudia kwa ujasiri na ukarimu wa Kanisa ambalo linainama chini ya miguu ya walio wa mwisho kwa upendo na urahisi. Bikira Maria aliyekubali kwa unyenyekevu mapenzi ya Mungu, atusaidie kufuta Yesu katika njia ya huduma, njia ya mwalimu ambaye anatupeleka Mbinguni.

22 October 2018, 12:00