Vatican News
Papa Francisko amekutana na wanshirika wa Upendo ( Rosminian) Mjini Vatican Papa Francisko amekutana na wanshirika wa Upendo ( Rosminian) Mjini Vatican  (Vatican Media)

Papa kwa Warosmini:Utakatifu ni njia ya kubadili Kanisa!

Kila Mkristo anaalikwa kuwa mtakatifu na kupitia njia za kiroho katika upendo, ukimya wa ndani na uhifadhi wa kimya ya nje. Ni mfano wa Mwenyeheri Rosmini ambapo Papa Francisko amekumbusha wakati alipokutana na wanashirika wa Upendo wa familia ya Rosmini

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Kuwa makini katika kushikilia Kanisa na bila kikomo kwa ajili ya mafundisho ya Vatican, kama alivyokuwa akishauri na kuishi Mwenyeheri Antonio Rosimin”, ndiyo wito wa Papa Francisko aliowashauri kuuendeleza, asuhuhi ya tareje Mosi Oktoba 2018, alipokutana na wanashirika wa Upendo, Shirika lililoanzishwa na Mwenyeheri Antonio Rosimi kunako mwaka 1800. Ni Padre aliyekuwa  na mwanafalsa aliyezaliwa nchini Italia ya Kaskazini.  Amesisitiza hayo katika hotuba yake  kwa kuongozwa na mada ya upendo unaoungana na ambao unafanya kuwa mtakatifu kwa pamoja.

Utakatifu ni njia ya kubadili Kanisa

Shirika la Warosmini wako kwenye mkutano mkuu hadi tarehe 23 Oktoba, wakiongozwa na mada: “muwe wakamilifu,… muwe na huruma”. Katika kufafanua hilo, Papa anasema, ni wito wa mafundisho ya mwanzilishi ambaye alijikita katika hatua ya kwanza ya habari njema ya kila mkristo ambaye anaalikwa kuwa mtakatifu na kuipokea  njia hiyo pamoja katika upendo”.

Utakatifu na zoezi la fadhila havihifadhiwi kwa walio wachache tu, hata kwa kipindi maalum cha maisha tu,  Baba Mtakatifu amesema.  Bali ni kwa ajili ya wote wanaweza kuuishi kila siku kwa uaminifu wa wito kikristo. Ndiyo  watawa ikiwa ni  kwa namna ya pekee,  kuishi uaminifu  wao kwa maana ya  kujiweka wakfu kama mtawa. Kwa maana hiyo, Mwenyeheri Rosmini alikuwa akisali hivi: “Ee Mungu tutumie mashujaa wako”. Na hiyo ilikuwa wazi kwake kile ambacho alikuwa akisisitiza kutoka katika Motu Proprio Majorem hac dilectionem (yaani katika kanuni yake kuu ) kuhusu ushujaa wa maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine na kuutunza hadi kifo ( n.5). Utakatifu ni njia ya kweli ya mabadiliko ya Kanisa ambayo kweli Rosmini alitoa  katika kubadili dunia kwa kipimo ambacho inajibadili yenyewe.

Upendo msimamo wa kina na utakatifu katika utofauti

Upendo ni fadhila juu ya yote; Papa anathibitisha kuwa, Mtakatifu Paulo alikuwa akithibitisha pia kurudiwa hata  Mwenyeheri Rosmini wakati wa kuanzisha shirika la upendo. Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha kwamba, Padre huyo wa Trentino alikuwa akisindikizwa na nguvu na msimamo wa kina na uwezo wake wa kuwa kimya. Kwa maana hiyo amewataka wanashirika waige mfano wake na uweze kuwasaidia kuendelea katika kutoa matunda ya ukimya wa ndani na ushujaa wa kimya ya nje. Na hiyo ndiyo njia inayotoa matunda ya wema na utakatifu, njia ambayo wamepitia watakatifu na ambapo Kanisa linaelekeza waamini wake. Ni muhimu pia kuhifadhi utakatifu wa utofauti ambao mwanzilishi wao aliuchota kutoka kwa Mtakatifu Ignatius wa Loyola na kwamba bila kuwa nayo siyo rahisi kutenda kwa dhati upendo katika ulimwengu.

Muwe watu walio na mikono inayopokea.

Tasaufi ya upendo, akili na mali; ndiyo mambo muhimu ambayo Mwenyeheri Rosmini alikuwa wakiwashauri familia yake, hivyo hata Papa Francisko kwa kuanzia katika ushauri huo, leo hii amesema, ndio matendo ya upendo kwa mujibu wa Roho Mtakatifu anaelekeza kupenda. Matendo yao katika elimu na siyo mafundisho rahisi tu bali matendo ya upendo wa kiakili ambayo yanaanzia kwake Yesu Kristo, Neno lililofanyika mwili: na ukamilifu wa uwepo wao kitume.

Mahali walipo katika utume

Uwepo wao wa kitume, unachanua katika nchi ya Tanzania, Kenya na katika nchi za Marekani na Ulaya. Anawashukuru kwa ujasiri wa kuwa watu walio na mikono daima wazi kuelekea kwa wanaoteseka ili kupeleka msaada wa imani na upendo. Anawakumbusha kwa namna ya pekee, watawa kike na kiume Warosimi wanaofanya utume wao katika nchi ya Venezuela na ambao wanaalikwa kuwa mashuhuda wa ukaribu wa kiroho na chombo kwa watu ambao wanakabiliana na majaribu magumu.

01 October 2018, 15:22