Tafuta

Kardinali Mario Aurelio Poli Askofu Mkuu wa Buenos Aires  na  maaskofu  wengine wa nchi ya Argentina wakiwa na Papa Francisko Kardinali Mario Aurelio Poli Askofu Mkuu wa Buenos Aires na maaskofu wengine wa nchi ya Argentina wakiwa na Papa Francisko 

Papa kwa Sinodi ya Buenos Aires:Jilinde na vizingiti vitatu dhidi ya umoja wa Kanisa!

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa ajili ya Sinodi ya Jimbo Kuu la Buenos Aires kwamba:Sinodi ni mzunguko, ni kutembea kwa pamoja na kukubaliana. Ametoa onyo la kuhepuka hatari tatu zinazozuia umoja wa Kanisa yaani ni suala la ukuhani, tasaufi za ulimwengu na masengenyo

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video tarehe 27 Oktoba saa 3.00 usiku masaa ya Ulaya, kwa Kardinali Mario Aurelio Poli, Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki la Buenos Aires nchini Argentina, ikiwa ni katika fursa ya Sinodi ya kwanza ya Jimbo, mwaka (2017-2019) ikiongozwa na mada, “kutembea kwa pamoja”. Hayo ni  maandalizi ya kilele cha  Jubilei ya miaka 400 ya jimbo, ambapo wanatazamia kufanya madhimisho hayo kunako 2020. Jimbo kuu  la Buonos Aires nchini Argentina linasimamiwa na Utatu Mtakatifu.

Sinodi ni mzunguko , kutembea kwa pamoja na kukubaliana

Katika ujumbe kwa njia ya video Papa anansema: “Ndugu wapendwa, Kardinali Poli ameniomba kama ningeweza kurekodi ujumbe kwa ajili ya Siku ya Sinodi, nami ninafanya hivyo kwa furaha. Ninafuatilia Sinodi hiyo nikiwa hapa kwa njia ya taarifa kutoka jimboni; na sasa kwa kuwa taarifa zimefika na picha, ninajuzwa vema na kutambua jinsi gani mnafanya kazi sana”. Pamoja na hayo Papa amewaeleza juu ya kufahamishwa juu ya kardinali tembelea karibu maparokia yote, katika kipindi cha Sinodi, hata kabla yake alikuwa amekwisha tembelea ili kuweza kuzungumza na wanaparokia.

Kwa namna hiyo, Papa anaongeza kusema, “inaonesha wazi ni jinsi gani palivyo na mzunguko. Ndiyo maana ya Sinodi; ndiyo maana ya kuzungumza, kutembea kwa pamoja na kukubaliana kwa pamoja. Ametoa Mfano Baba Mtakatifu:” Fikirieni unapotembea, unakutana na mtu, unazungumza naye, unamsikiliza na kutafakari na ndiyo maana ya kutembea ili kuwepo makutano, kusikiliza na kutafakari. Pamoja na hayo, Papa ametoa swali: “ni jinsi gani ya kusikiliza? kwa maana mwingine anapokuwa anazungumza, mimi ninakuwa tayari ninafikiria kile ambacho ninataka kusema”. Tendo la kusikiliza, kumbe linahitaji utulivu wa kusikiliza na baadaye uweze  kusema kile unachohisi,  lakini  kwanza ni sikiliza”. Na kwa kusisitiza zaidi, Papa ameongeza kusema: “huo ndiyo utume wa sikio”, na hivyo amewapa ushauri na ili kwamba, “wasisahau kamwe kwa maana ni muhimu!

Kanisa katika mchakato wa safari lazima libarikiwe

Baba Mtakatifu anasema: “Wakati wa mchakato huo Kanisa,  lazima libarikiwa, kwa sababu ya kutembea kwa pamoja  na ili kukua pamoja, na katika Kanisa kwa namna ya pekee linavutia baraka ya Mungu. Wakati wa mchakato wa safari yao watapata mambo mengi mema na siyo tu matamu, kwa maana anabainisha kuwa, kuna Matatizo matatu ambayo ni lazima kuzingatia wakatika wa safari hiyo.Matatizo hayo ameeleza kuwa ni suala la kujiona ukuhani hukuhani. Kutembea kwa pamoja maana yake ni kuvuta jumuiya nzima ya jimbo, parokia zote, au mikutano yote kwa mfano, katika shule huwa wanatembea kwa  pamoja kwa maana wote ni watoto wa Mungu.

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, “ inatia huzuni kuona wakati mwingine wapo waamini ambao huwa wanasikiliza tu anachozungumza padre peke yake na kwa jinsi hiyo, padre si  baba tena  bali anageuka kuwa mkuu. Lakini si wote amebainisha , japokuwa ameongeza swali: je katika parokia yako kuna baraza la uchumi?  Katika parokia yako kuna baraza la kichungaji? Au utasikia wengine wanasema hakuna maana kila kitu anafanya padre. Hapo Baba Mtakatifu anathibitisha: “Tazama hiyo ndiyo suala linaloitwa ukuhani ukuhani, kwa maana hiyo, Papa anawapa onyo  kuwa makini katika  suala la ukuhani ukuhani ambao ni kinyume  mwenendo wa kiungo cha Kanisa! Na watu wote wa Mungu, Papa anasema,  hilo ndilo Kanisa linalotembea pamoja. Ni kutembea ili kupata kile ambacho Mungu anapenda, kuonesha  kwa imani na kufurahia kwa imani. Kwa kusisitiza amethibitisha zaidi kuwa: “hatari ya kwanza iliyopo ndani ya Kanisa daima ni ukuhuni uhukuani na hivyo jilindeni!

Hatari ya  pili ni ubobezi wa tasasaufi ya ulimwengu

Akizungumza kuu ya hatari ya pili ni ile tasaufi ya ulimwengu na hivyo: “Kuishi Injili katika  dhamana ya ulimwengu, Baba Mtakatifu amesema hapan! Ni lazima kuishi Injili kwa mantiki ya kiinjili. Ni kuishi Injili  kwa thamani za kibinadamu ambazo Bwana alitupatia na thamani za kikristo ambazo yeye alituonesha na , kwa maana hiyo Papa metoa onyo kali la kuhepuka malimwengu. Hata hivyo amethibitisha kuwa hayo si mawazo yake tu, bali ni kile ambacho Yesu aliowaombea Mitume wake kwa Baba ya kuwa: “ siombi uwatoe ulimwenguni bali naomba uwakinge na yule mwovu na ili wasianguke katika roho ya ulimwengu”.

Ka kutambua hivyo, Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba, “roho wa ulimwengu inajiingiza kila sehemu, hasa katika mantiki ya kimitindo, na utasikia “ sasa ndiyo mtindo na wote  wanakwenda nyuma ya mtindo huo, au sasa mtindo wa mwingine wa kufikiria na wote hivyo hivyo”.  Kwa namna hiyo Papa amehimiza “kubaki macho wazi  na kwamba wasinywe chochote kile !  kwa maana, “ kuna neno moja ninapenda kulitumia sana. Kuweni makini na ukoloni wa itikadi”.

Ufafanuzi wa ukoloni wa kiitikadi: Papa Francisko ametoa mfano kuwa: “ Sisi tulitawaliwa na ukoloni, yaani Amerika ya Kusini  yote ilitawaliwa na ukoloni, Afrika ilitawaliwa na Ukoloni, Asia nayo pia,na  kwa maana hiyo tunafikiria jinsi  unapofika ukoloni, huchukua maeneo na kutawala, maana ni jambo lililotukia katika historia, lakini zzidi ya ukoloni ule, Papa anabainisha kwamba , kuna ukoloni wa akili, ukoloni wa kiitikadi, mahali ambapo mawazo mengine yanaletwa na mantiki ambazo siyo za kibinadamu, na si za nchi yako  hata kuwa za kikristo: hayo ndiyo malimwengu yaani kuishi kwa udhaifu na ndiyo hatari  ya pili ambayo ni ya malimwengu”.

Hatari ya tatu  masengenyo

Akiendelea na ufafanusi kwa upande wa Baba Mtakatifu amebainisha, hatari ya tatu kuwa ni ile ambayo inadhoofisha zaidi jumuiya za Kanisa  yaani ni umbea. Udaku ni kama ugonjwa wa surua unapokuingilia unakuwa ni shida kutoka mapema, hivyo ni masengenyo ambayo wengi wanashindwa kujizuia katika kuwasema wengine.  Papa anasisitiza : “Kuweni makini na udaku! Someni kile ambacho Mtume Yakobo anasema kuhusiana na udaku huo. Ni mara ngapi tunasikia: mwanamke huyo ni mwema, anakwenda Kanisani kila Jumapili na kusali misa za kila  siku, lakini ni mmbea! Papa anathibitisha, “ Kanisa litabarikiwa, iwapo litamsaidia mtu wa namna hiyo! Kuna lipizi lake  ili usiwe na umbea na hivyo Papa anasema kuwa ; nalo ni kujiuma ulimi! “Ndiyo utavimba lakini kwa namna nyingine utapona”. Unapotaka kuzungumza juu ya mtu au kumsengenya juu ya jambo fulani, jiume ulimi na omba Yesu akuondolee tabia hiyo. Hata hivyo ametoa mfano kwamba wao waliozaliwa Buonos Aires ni wambea, japokuwa ni tabia inayowatazama watu wote, lakini “umbea kidogo wanao na kwa maana hiyo, amesewaomba kwamba, “ katika mchakato wa Sinodi kila mmoja ajitahidi kuzungumza neno, kutoa tafakari lakini si kumdhuru mwingine”.

Hatari hizi tatu watakutana nazo katika mchakato wa safari: Baba Mtakatifdu amesisitiza kuwa, katika safari hiyo ambayo ni ya mkutano wa kusikiliza, na tafakari, hakika hatari tatu watakutana nazo, zile  za ukikuhani ukikuhani, kupenda malimwengu na umbea. Ameongeza kusema: “Ndiyo labda mnajitetea juu ya hilo”, lakini padre je uhakika huko wapi? Uhakika hamtaweza kuupata kabla ya safari. Hakuna bima juu ya maisha, hakuna bima katika njia hiyo. Kila siku ni lazima kukaa mbele ya Mungu na kutembea!

Usalama katika kutembea unahitaji tasaufi ya Heri

Baba Mtakatifu akifafanua juu ya uhakina na usalama amesema kuwa, “Kuna usalama wa aina mbili usio shindwa. Wa kwanza ni ule wa Heri.  Kwa maana hiyo anashauri : “Ingia katika tasaufi ya Heri!; Lakini  je ni Heri zipi?  Amewashauri kuchukua Injili ya Matayo na kusoma na iwapo wanataka ile fupi wachukue Injili ya Luka ambayo ni fupi, lakini tasaufi ni hiyo hiyo. Tasaufi ya Heri ni ile ambayo Yesu anamtaka kila  mtume yoyote yule awe nayo. Na ndiyo mambo mazuri ya uhakika wa usalama. Na katika upepo wa hali ya heri, Sinodo haiwezi kushindwa kwa uhakika, Baba Mtakatifu amekazia!

Uhakika mwingine, ni kusoma protokali juu ya kile tutakacho hukumiwa. Papa amabainisha kwamba hiyo: “ Ni protokali ambayo Yesu atatafakari juu ya Sinodi hiyo itakapomalizika. Na hiyo tayari wanayo katika katika Injili ya Matayo, Sura ya 25 inayohusu matendo ya upendo”: Lakini lazima kusikiliza jinsi anavyosema Bwana. Kila siku ni kusoma, kwa maana wale wanaotaka kutembea katika Sinodi, wasoma heri kila siku na Injili ya Matayo sura ya 25, hapo watakuwa na uhakika”.

Kutembea bila kusimama

Baba Mtakatifu akihitimisha ujumbe wake kwa njia ya video, katika Baraza la Sinodi ya Jimbo Kuu la Buonos Aires, amesema kutembee na si kubaki wamesimama, kutembea kwa ajili ya kukutana, kusikilizana na kutafakari kwa pamoja; kujilinda dhidi ya ukikuhani ukikuhani na dhidi ya malimwengu pamoja na masengenyeo, kujibidisha na tasaufi ya Heri na kusoma Injili ya Mtakatifu Matayo sura ya 25. Hayo yote pamoja na sala ambayo ni jambo muhimu zaidi ya yote aliyosema.  Na kwa upande wa sala: Baba Mtakatifu anashauri: “Sali kama Yesu alivyotufundisha. Salini kwa ajili ya wengine, kwa ajili ya wanaotembea na kwa wale wasio taka kutembea, kwa wale wanaotembea vibaya, walio mbali, kwa ajili ya Jimbo Kuu la Kanisa na kwa ajili ya Askofu Mkuu.  Katika roho hiyo ya sala kwa hakika Sinodi itakuwa na mafaniko. Bwana awabarika na wakati wanaendelea kusali basi wamkumbuke katika sala zao”.

 

29 October 2018, 12:40